Cha kuzingatiwa kuhusu Makontena

Cha kuzingatiwa kuhusu Makontena

mchumihalisi

Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
28
Reaction score
98
Nimejaribu kupitia mijadala mbalimbali juu ya issue ya Makontena yanayotajwa kuwa ya RC dhidi ya tuhuma za Kodi zinazomkabili..! Watu wengi wanasema busara itumike busara itumike lakini ukiangalia hili sakata toka mwanzo kwa RC hakukua na busara leo Twitter nmeona clip fupi inazunguka RC akisema kuanzia TRA,Kamishna mpaka Waziri 'Wao' wa Fedha nitawasemea kwa Rais.

Kibusara sidhani kama RC alipaswa kuongea hayo tuseme alipitiwa je aliwahi kumtafuta Waziri na kuzungumza nae? Mbona mwanzoni aliyakana? Sera ya Nchi kwa sasa ni kuwa-impower wazawa kwenye masuala ya Fenicha sasa je alishirikisha serikali mwanzoni mwa mchakato huu?? Pengine kuliko kubeba samani kutoka Huko nje ya Nchi wale watu zile pesa wangechanga wangezituma Bongo na wangepewa ndugu zetu wa Suma JKT na wangetoa vitu vizuri kwa ajili ya Walimu na Wanafunzi wetu mashuleni..

Kwenye hili kuna mmoja anafata sheria na kuna mwingine anaamini yuko juu ya sheria, leo Le Mutuz anatoa confidential Letter kuhusu sakata hili na kumtuhumu Waziri, Swali Waziri akiamua nae kujibu mapigo itakuje? Inavyoonekana RC ameanza kumchokoa mapema kidogo Waziri mpaka kauli ya kwamba ataenda kusema kwa Rais inamaana mpaka leo RC hajui na haamini kama Rais ana taarifa za huu mzigo mpaka akamwambie yeye? Muda mwingine ni vema tukaacha kufanya vitu binafsi (personal) na kutengeneza public sympathy ili yako yaende.

Leo zimeanza kutoka picha za watoto wakiwa wamekaa chini kisha maelezo kuwa vifaa vimezuiliwa lakini kwenye vifaa hivyo hakuna madawati wala vitu ambavyo wanafunzi wa shule za kata wangeweza kutumia, Haya hapo hapo vifaa alisema si kwa ajili ya Wanafunzi bali Walimu Je kuna walimu wanakaa chini??

Kuna mahali tukiparekebisha tutasonga mbele zaidi.

MCHUMI HALISI.
Aug 29 2018
 
Kwani ina maana rais hajui hii habari kilichoendelea au "eti anaenda kumwambia"
 
Amezoea kubebwa sasa anafikia hatua ya kujiona kwamba hakuna wa kumugusa kwakuwa rais anamkubali, bila kujua kuwa rais huyo huyo keshamwona anaboronga asipochukua tahadhari atakuja kupigwa chini. Atumie busara badala ya kupayuka na kurafuta sympathy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom