Certificates zingetolewa baada ya $300m kulipwa

Mzee wa hat-trick

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2016
Posts
1,730
Reaction score
2,394
Sio jambo baya kupewa certificates baada ya makubaliano yale, ila nadhani ingeleta maana zaidi kama wangepewa baada ya fedha hizo kulipwa. Hiyo ingeleta maana zaidi ya mafanikio.

Hii ni kutokana na fedha hizo kuwa na utata wa kulipwa au kutokulipwa, na kama itatokea hazijalipwa, yawezekana wakarudi tena mezani kwa ajili ya mazungumzo.

Na kama watalazimika kurudi tena, basi itakuwa ni kama wamepewa vyeti vya ndoa tu ambavyo hutolewa kabla ya kuingia kwny mchakamchaka wa ndoa yenyewe.
 
Tulia Mkuu Nchi inasonga mbele wewe unawaza Certificate.
 
Nawapongeza wamepewa vyeti ila watapeleka wapi

Ok congraturation
Ingawa mtoa mada upo sahihi
 
Wewe mchochezi. Utapimwa mkojo. Wakale wapi?
 
Nadhani watapewa na vingine tukilipwa hizo hela zetu
 
Hii ni kutokana na fedha hizo kuwa na utata wa kulipwa au kutokulipwa, na kama itatokea hazijalipwa, yawezekana wakarudi tena mezani kwa ajili ya mazungumzo
Nimeiona hii jana kupitia yale maandishi yanayopita chini ya tv ya Ruanda Acacia Unable to pay $300m
upfront to Tanzani je maana yake ni nini??
 
"Nguvu kubwa inayotumika kuonyesha mafanikio katika majadiliano inaonyesha something is wrong" Zitto Kabwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…