Kama unataka kutumia kiasi kikubwa na una kampuni ya ujenzi wa nyumba za maghorofa manne kwenda juu, basi ni heri uchue hiyo Cement, changanya na kokoto (Concrete) kwa Ratio watakayosema watengenezaji cement na chukua mawe safi, maji safi na mchanga safi na tengeneza Zege lako na utengeneze Cubes na kisha upeleke UDSM kuzi-Crush.
Matokeo utakayopata yasipishane sana na kiasi walichosema wao. Kumbuka kwamba kwenye SITE, utatumia quality mbaya na hutakuwa na muda wa kutosha kufanya kama ilivyo kwenye SAMPLE.
Ila kwa jengo la ghorofa kuanzia nne kushuka chini, msiwe na wasiwasi, hata hiyo ya 35 sijui mnaweza kuitumia ila cha muhimu mhakikishe mnapima vizuri kokoto mnazoweka na msizidishe maji wala kuweka maji kidogo na kuhakikisha mnashindilia vizuri. Jengo litakuwa poa tu.
Kuna maghorofa nilishaona yamejengwa kwa matofali ya kuchoma na yapo imara tu. Ila kuta zake zinazobeba uzito ni nene sana maana kwa jengo la ghorofa nne, ukuta una kama upana wa mita moja hivi.
Tafadhali kila panapowezekana, tumia Matofali ya kuchoma na epukaneni na Cement maana huwa zinatoa Radiations ambazo si nzuri kwa afya zenu. Na kama walivyosema wengi, CEMENT NUNUA iliyoandikwa MADE IN TANZANIA.
Tuisaidie Nchi yetu kwa kununua vitu MADE IN TANZANIA.
Nakuona fundi mchundo uko kazini.
wadau wastan wa tofali ngapi naweza fyatua kwa mfuko?
tofali 40
Ni nzuri sana hasa hiyo rhino na lucky inatengenezwa pakistan pia arabuni hapa dubai ghorofa nyingi sana ikiwemo burj kharifa (ghorofa refu kuliko yote duniani)limetengenezwa na hiyo lucky..ni nzuri sana ata mimi nimeshaitumia....hapa dubai inauzwa tsh 3500 kwa mfuko mmoja..nunua ni nzuri
Kama unataka kutumia kiasi kikubwa na una kampuni ya ujenzi wa nyumba za maghorofa manne kwenda juu, basi ni heri uchue hiyo Cement, changanya na kokoto (Concrete) kwa Ratio watakayosema watengenezaji cement na chukua mawe safi, maji safi na mchanga safi na tengeneza Zege lako na utengeneze Cubes na kisha upeleke UDSM kuzi-Crush.
Matokeo utakayopata yasipishane sana na kiasi walichosema wao. Kumbuka kwamba kwenye SITE, utatumia quality mbaya na hutakuwa na muda wa kutosha kufanya kama ilivyo kwenye SAMPLE.
Ila kwa jengo la ghorofa kuanzia nne kushuka chini, msiwe na wasiwasi, hata hiyo ya 35 sijui mnaweza kuitumia ila cha muhimu mhakikishe mnapima vizuri kokoto mnazoweka na msizidishe maji wala kuweka maji kidogo na kuhakikisha mnashindilia vizuri. Jengo litakuwa poa tu.
Kuna maghorofa nilishaona yamejengwa kwa matofali ya kuchoma na yapo imara tu. Ila kuta zake zinazobeba uzito ni nene sana maana kwa jengo la ghorofa nne, ukuta una kama upana wa mita moja hivi.
Tafadhali kila panapowezekana, tumia Matofali ya kuchoma na epukaneni na Cement maana huwa zinatoa Radiations ambazo si nzuri kwa afya zenu. Na kama walivyosema wengi, CEMENT NUNUA iliyoandikwa MADE IN TANZANIA.
Tuisaidie Nchi yetu kwa kununua vitu MADE IN TANZANIA.
Anachosema ni kweli kabisa building materials kwa Dubai ni very cheap na all merchandise kwa ujumla bei inapanda kutokana na boarding revenues profiting na tending charges pale bandarini.Thibiitisha kama uko Dubai,dhibitisha hiyo tsh.3500 kwa mfuko!
Mkuu hiyo maneno ya tofali za cement kutoa radiation mbona ni habari mpya? Hebu tusaidie vizuri hapo hasa ambao ndo tumemaliza msingi tunapiga mawazo ya kupandisha za kuchoma au za cement
Wadau na me napenda kujua nyumba ya ghorofa moja ya vyumba vitano master bedrooms inachukua mifuko mingapi ya cement.
Natanguliza shukrani.
Mkuu, swali lako ni kama kuuliza (kwa mfano Mayweather na The Big Show wana umri sawa) kuwa hawa Mibaba wenye umri sawa na wote wanacheza michezo ya kutumia nguvu, watakula kilo ngapi? Sidhani mlo wa The BigShow, Mayweather atamaliza hata nusu yake. Swali lako halijibiki bila data kamili.
Ila kama unataka kujenga ghorofa na unauliza idadi (gharama) basi achana nalo maana litakushinda.
Soma hapa: Radiation exposure, building material
Mengine wewe niamini tu maana nimesoma kuhusu ujenzi na Chemicals in Bulding Materials.
Ila si kubwa sana kivile. Lakini kama unaweza kuiepuka, basi ikimbie au ipunguze.
Luka 14 : 28 - 30
14.28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?
14.29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,
14.30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.
Unanitisha kwa kagorofa kamoja hivyo ningekuambia malengo yangu baada ya miaka 10 si ungesema mi ni mwehu.
Usilolijua litakusumbua.
Ukimaliza kujenga, kwenye finishing kama kupaka rangi, mabomba, sakafu, ngazi, umeme nk ndiyo utakuja kukumbuka maneno yangu. Ningelikujibu ovyo ila nakuacha kwa leo na kuombea malengo yako ya miaka 10 ijayo yatimie maana mie sina roho korosho kama unavyoonekana wewe. Sasa hivi huna kitu, unasubiri miaka ijayo na unasema niachane na wewe, ukipata hizo fedha zako miaka 10 ijayo, sijui itakuwaje?
Diana Ross aliimba, more money, more problem.
umeuliza swali zuri sana...mimi ni civil engineer na ninajua ubora wa cement mbalimbali...........ukweli ni kwamba watu wengi sana wanauziwa cement zenye ubora mdogo pasipo wao kujua..................kuna cement za barabarani ambazo huwa zinamwaga ili kufanya soil stabilization ambazo mara nyingi ubora wake ni mdogo ambao ni 30.2N hadi 32.5N kwa kiwango cha kiutalaam na watu wamekuwa wakiuziwa hizi cement na kujengea nyumba pasipo wao wenyewe kujua.Cement ambazo unatakiwa ujengee nyumba inatakiwa iwe 40N au 42N.Mimi katika mtaa ninapoishi watu wengi wanachakachuliwa cement pasipo wao kujua.Unakuta mtu anauza cement ambazo amezichanga na zile za barabarani ili apate faida kubwa.ukweli ni kwamba cement za barabarani bei yake ni ndogo kwa hiyo akizichanganya anapata faida kubwa.
NB:JITAHIDI UKIENDA NUNUA CEMENT SOMA MFUKO HADI UONE 40N AU 42N UBORA WA CEMENT.MAFUNDI WENGI HAWAJUI KIINGEREZA NDIO MAANA HAWAWEZI KUJUA LAKINI WANAWEZA ANGALIA HIYO NUMBER 40N AU 42N.