CECAFA hii waamuzi wetu wamo?

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Mashindano ya CAF na yale ya FIFA waamuzi wetu wa soka huwa hawachaguliwi kuchezesha mechi.

Je, kwenye haya mashindano ya CECAFA yanayofanyika nchini wamebahatika?
 
Chonde chonde TFF! Msimsahau yule mwamuzi wenu maalum kwa ajili ya kuipa ushindi Simba! Ameisaidia sana Simba kwenye Kombe la Shirikisho la Azam.

Lipeni fadhila tafadhali.
 
Aisee waamuzi wetu wawe wapo au hawapo wana kitu kikubwa sana cha kujifunza kwa mwamuzi aliyechezesha mechi ya jana kati ya Yanga na Big Bullets. Yaani yule mwamuzi nimemkubali sana hapepesi macho yaaani kama ni faulu ni faulu tu, kama ni kadi nyekundu ni kadi nyekundu, kama ni penati ni penati tu. Jana ndio nimegundua kwa nini waamuzi wetu wanaishia kuchezesha ndondo na wakifanikiwa sana ni kuchezesha VPL basi.

Hebu fikiria mwamuzi anachezesha mechi kubwa kati ya Simba na Yanga halafu mchezaji kachezewa rafu ndani ya "box" refa hatoi penati kwa sababu eti mechi ndio kwanza ipo dakika za mwanzoni. Au anaogopa kutoa kadi nyekundu eti ataharibu ladha ya mchezo. Sijui waamuzi wetu wanatumia mtaala upi kujifunzia ambao upo tofauti na waamuzi wengine duniani. Yaani Rwanda na Burundi ni nchi ndogo sana ukilinganisha na Tanzania lakini mara nyingi sana utaona waamuzi wao wakichezesha mechi kubwa duniani.

TFF na chama cha waamuzi mna kazi kubwa sana ya kufanya kwa waamuzi wa Tanzania ili wafikie viwango vya kimataifa.
 
Kama hawamo ni vema ili tuone Utopolo wanaoshiriki watamlalakia nani,manake wamezidi kuwalaumu marefa na tff,huko ni CECAFA tu.
 
Aisee waamuzi wetu wawe wapo au hawapo wana kitu kikubwa sana cha kujifunza kwa mwamuzi aliyechezesha mechi ya jana kati ya Yanga na Big Bullets. Yaani yule mwamuzi nimemkubali sana hapepesi macho yaaani kama ni faulu ni faulu tu, kama ni kadi nyekundu ni kadi nyekundu, kama ni penati ni penati tu. Jana ndio nimegundua kwa nini waamuzi wetu wanaishia kuchezesha ndondo na wakifanikiwa sana ni kuchezesha VPL basi.

Hebu fikiria mwamuzi anachezesha mechi kubwa kati ya Simba na Yanga halafu mchezaji kachezewa rafu ndani ya "box" refa hatoi penati kwa sababu eti mechi ndio kwanza ipo dakika za mwanzoni. Au anaogopa kutoa kadi nyekundu eti ataharibu ladha ya mchezo. Sijui waamuzi wetu wanatumia mtaala upi kujifunzia ambao upo tofauti na waamuzi wengine duniani. Yaani Rwanda na Burundi ni nchi ndogo sana ukilinganisha na Tanzania lakini mara nyingi sana utaona waamuzi wao wakichezesha mechi kubwa duniani.

TFF na chama cha waamuzi mna kazi kubwa sana ya kufanya kwa waamuzi wa Tanzania ili wafikie viwango vya kimataifa.
Mkuu, mechi hiyo japo niliitazama kipindi cha kwanza tu ndo nkajiuliza marefa wetu wamo katika shindano hili?
 
Utopolo mtapigwa sana hadi mkose nyimbo za kuimba.

Simba timu ya nchi

Back
Top Bottom