UBIA WA KWELI KUTUKOMBOA NA MAFISADI TANZANIA NI
ULE KATI YA CHADEMA NA WATANZANIA WAVUJA JASHO MOJA KWA MOJA!!!
Kwa mazingira ya siasa yalivyochafuliwa kwa Mafisadi kuanzisha vyama vyao vya upinzani kibao nchini, mimi ninaamini leo na nitaendelea kuamini kesho kwamba Chama Cha Siasa cha kuweza kuleta mabadiliko ya kweli ni sharti ikwepe kabisa mtego wa ushirikiano ghiliba na vyama vingine vya siasa isipokuwa wasisitize zaidi Ubia wa Moja kwa Moja na sisi Wapigakura bila udalali!!
Je umewahi kujiulizakwamba pale uchaguzi mkuu kati ya Mhe Augustino Mrema wa The then Mighty NCCR-Mageuzi ilioonyesha kushinda kwa mbali dhidi ya Mhe Benjamin Mkapa na KIMAZINGAOMBWE TU kule kuitishwa kurudiwa uchaguzi Mkoa wa Dar es Salaam ndipo USHINDI WOTE WA UPINZANI ukatowekea kama theluji jua linapochomoza; na wala tusisikie Mhe Mrema mwenyewe akilalamikia hilo wala kufungua shitaka popote??
Je bado kwenye kumbukumbu zako utakua anatafakari kwenye uchaguzi uliopita jinsi CUF walijichagulia kunyamaza katika kipindi cha uchakachuaji ambapo kimsingi walionekana kuwa na jukumu la kulikemea (How CUF Dishonoured their Duty to Stand for the Truth and Speak uprightly at the greatest time of Need) badala yake wakaamua kutekeleza kwa dhati sera yao mpya ya kula mabua kwa pamoja na nguruwe???
Kama haya machahe tu hayatoshi, unakumbuka kilichofanywa bungeni hadi Chama kilichokidhi maelekezo ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CHADEMA) kuitwa chama rasmi cha upinzani bungeni kilipotoweshewa haki yake ya kikatiba kushika uenyekiti wa Kamati mbali mbali za bunge kwa maana ya KUTEKELEZA JUKUMU LA MSINGI KUISIMAMIA UTENDAJI WA KILA SIKU WA serikali kulivyopindishwa hadi vyama vyenye mbunge mmoja mmoja bungeni ndivyo vikajimegea Uenyekiti wa kamati hizo huku Mwana-CHADEMA Zitto Kabwe akijiamulia kujipigia TIKITAKA KUPITIA IKULU ndipo akajifariji na kakijikamati kamojawapo???
Hakika ndugu, wahenga waliona huko nyuma kwamba UMOJA NI NGUVU na kwamba utengano ni udhaifu mkubwa sana. Lakini kule kudiriki kuunda Umoja wa Kambi ya Upinzani kati ya chama halisi cha upinzani na utitiri wa Vyama vya Upinzani-CCM Aaa, Baa, Chaa, Daa na kuendelea yote ni kupoteza wakati bure kabisa.
Laiti CHADEMA tungaligundua na kutii ukweli huu na kuzingatia mapema maelekezo ya upole na busara kubwa mno wa mwandishi ya wa Vitabu vya Michezo ya Kuigiza, Henri Ibsen mnamo mwaka wa 1882 kwenye kitabu chake cha
'An Enemy of the People'' ambapo mhusika mkuu Dr Stockmann (kama kilivyo CHADEMA hivi sasa machoni mwa mafisadi na mawakala wao nchini) kwamba "The strongest man (political party) is he (it that) who stands alone" basi Wa-Tanzania leo hii wasingalikua wakiteseka kiasi hiki mikononi mwao MAFISADI watumiao DONARI 30 kila kukicha kutugawa mithili ya nyama buchani!!!
Hakika Wa-Tanzania tumedhalilishwa sana kila wakati kukijaribu kupitia hiyo njia iliozoeleka la ushirikiano wa Vyama vya Upinzani kondoo na vyama vya Upinzani Chui; nasema kura zetu halali zichakachuliwa mno kwa miaka mingi sana kwa njia hii, wazalendo tuzulumiwa mno haki zetu na rasilmali za taifa kumiminikia tu katika mifuko binafsi ya hawa wazandiki na makuadi wao.
Kwa kweli Ndugu Kingwele japo ninakawaida ya kuwaheshimu sana Wana-JF mliotutangulia humu jukuani pamoja na akina MM Mwanakijiji, lakini naomba nami walau unipe japo nafasi neseme kwa nini CHADEMA kisimtafute ushirika akina Augustino Mrema (Mzee wa Kiraracha Mwenye Talanta nyingi zisizopuuzika lakini zikizidiwa zaidi na ule Utaalam wake wa Kuua Vyama vya Upinzani nchini kwa faida ya Chama ambacho hadi kesho yeye hajafuta Ukada wake).
Ndio, ninakuomba kwa heshima na taadhima kabisa unikubalie kwamba CHADEMA kisimtafute ushirika John Mimose Cheyo (Mzee Mapesa lakini iendayo kwenye mfuko binafsi kwa kufumbia macho ufisadi kwenye kamati yake kule) kwa kuwa ufisadi wa kutisha nchini ambayo hivi sasa umeongeza maradufu maumivu kwa wananchi umetokea ndani ya kipindi chake akiwa ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kusimamia mapato na matumizi sahihi ya serikali; upekuzi wangu wote umenielekeza kwamba Mzee Mapesa haswaa ni sehemu ya ufisadi wote nchini kwa kuwa hakuna hata rekodi moja inayoonyesha kama aliwahi kuona na kupigia kelele ufisadi wote wa EPA, Meremeta, Richimondi, Dowansi, Ndege ya Rais, Radar na nyinginezo kibao tu.
Lakini akina hao wengine akina James Mbatia wa kilichogeuka kuwa NCCR-Manunuzi, CUF-Maslahi Binafsi na hivyo vyama vingine visivyojulikana zaidi ya mita 20 ya mitaa vyilikopata ofisi, nisivizungumzie kwa leo.
Ubia wa kweli na wenye mafanikio kotekote ni ule wa moja kwa moja kati ya CHADEMA na sisi Vijana wavujajasho tuliowengi Tanzania na wala si vinginevyo!! Maoni yako zaidi tafadhali.
Nimekaa kimya kwa muda bila kuchangia...tangu nilipojiunga enzi ile Forum hii adhim ikiitwa Jambo Forums..tukiwa na magwiji wakiongozwa na E.S, Dr. Who, Kichuguu, Mkandara..n.k. JF imekuwa ni kisima cha elimu.
Nianze kwa kutoa ...
Kingwele wa Kingwele.
Kijijini, Kwegole-