maguzu masese
JF-Expert Member
- Jan 22, 2013
- 283
- 141
Nina andika mada hii nikiwa najua kabisa kuwa itaniletea shida sana kwa wasiokubali Changamoto , hasa changamoto za mitazamo yenye ukweli ndani yake hasa katika jambo lililotokea kuaminiwa na wengi kwa muda mrefu na kwa kuwa na imani kubwa na waleta Jambo hilo. Lakini pia hata kama mitazamo ya namna hiyo haina ukweli ndani yake, itasaidia kuthibitisha ukweli wa jambo kwa uwazi zaidi.
Ninaandika nikiamini mchango wangu una ukweli ndani yake, inaweza ikawa ngumu kwa wapokeaji kutambua hili lakini kwa waletaji wanajua nini hasa kimo mioyoni mwao japo inawawia vigumu kusema wazi wazi kulingana na ukubwa wa Jambo.
Mahesabu ya SIASA ni lazima tukubaliane kuwa ni tofauti sana na mahesabu mengine yoyote uyajuayo.SIASA ni ngumu sana kwa asiyeijua na ni rahisi sana kwa anayeijua, Mengi ktk Siasa hayafundishwi darasa lolote dunia hii, hata nathubutu kusema kuwa wengi wanaojiita wana siasa na walio na majina makubwa ktk siasa kwa asilimia kubwa sana wengi wao HAWAIMUDU VYEMA ( HAWAJUI) wanajikuta wanakwenda tu kama maji kufuata mkondo na wengine wanajikuta wanakuwa juu kulingana na mabadiliko ya msukumo wa lazima wa umma ( ukweli mchungu lazima tuumeze)
Narudi kwenye Mada yangu.
Katika suala la Muungano, Wa Tanganyika na Zanzbar (KWA MTAZAMO WANGU), naona wote wanaoupigania kwa maana ya kutaka serikali tatu ( NIKIWEMO MIMI) hatuko wazi kwa wananchi, hatusemi ukweli, ukweli ni kwamba hapa tunatamani kila mmoja achukue HAMSINI ZAKE,wanaotoka VISIWANI wanatamani waachiwe Visiwa vyao sema wanaona noma tu kuiweka wazi, wanaotoka BARA, wanatamani waachiwe Tanganyika yao sema wanaona noma tu kuiweka wazi, hapa huenda inafanywa makusudi kutokana na HOFU ( sijui ni ya nini)
Hapa inakosekana sentensi ya moja kwa moja ya kwamba TUJITENGE , ama kila upande UJITEGEMEE, Na hii inatokana na Historia ya muda mrefu baina ya pande hizi mbili. lakini hili suala hata kama leo tutakuja na hizi 3, bado huko mbele kila mtu atadai uhuru wake, Mimi nitakuwa moja ya wafuasi ktk kundi la kudai kila mtu ajitegemee.
CCM, walilijua hili na wanalijua vyema na ndio maana hata ktk mchakato wa katiba suala la muungano liliwekewa mabano kiaina, na pia hii ya 3, wanayoikataa ni kwasababu wanajua kama zikipatikana 3, basi ndio mwanzo wa kudai MOJA kila upande na hiyo ya tatu inayounganisha hizi mbili lazima itakufa ( jaribu fikiria vizuri hapa utapata majibu mazuri)
CCM Wanapinga vikali kutokana na sabau nyingi sana na zenye manufaa kwao kwa uwepo wa muungano. Kama huu wa Tatu usingekuwa unaelekea kuzaa kila mmoja kudai uhuru wake wasingeweza kukataa bali wangeruhusu hizo 3, na ndio maana wanalazimisha 2 ili muungano uendelee kwa manufaa yao hata kama muungano huu una dosari kubwa.
CDM, na CUF wanataka 3 ili baadaye kila mmoja apate ku dominate upande mmoja maana CDM yuko vizuri sana BARA na CUF yuko vizuri sana VISIWANI, na hii ndio inapelekea kufa kwa ccm moja kwa moja maana wakipigwa ( TANGIZA) kote kote hawana pa kuponea, Pia CUF na CDM kuendelea kuwepo huu wa CCM wanaoutaka wa 2 Ni ngumu sana kuchukua nchi ( hii iko wazi) Huyu NCCR amejumuishwa tu katika hili hana faida ya moja kwa moja zaidi ya kuwa mpinzani mzuri wa CDM kwa bara hapo baadaye, kwa sasa ameungwa kama kuleta picha frani tu ili mambo yawe kama yanavyotakiwa kuwa.
Hata ningekuwa miongoni mwa STRATEGISTS wa CDM, CUF ama CCM, hapa ningecheza hivi hivi na hata zaidi ya hivi. Ila ningekuwa Strategists wa NCCR, huu pia ndio ulikuwa mwanya wa kutokea vizuri sana, maana lazima CUF ama CDM mmoja ningemliza akiwa anauguza maumivu mimi nashika hatamu, Siasa ndivyo ilivyo.
'' Katika siasa, kuna kipindi maadili ni lazima kuyaweka kando ''-Andrew Nkumbi