Mathias Raymond Nyakapala
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 2,181
- 1,493
Create Date: 5/15/2017 23:52
CDA UNABII WAO WATIMIA LEO 15/05/2017
Na:Mathias Raymond Nyakapala
-Kumbuka NENO LINAUMBA
-Nawasalimu wote kwa Jina la Mungu aliye juu,naweka kumbukumbu sawa niliwahi kuandika andiko langu linalosema CDA DODOMA NI TATIZO wapo walionipinga na kusema sijui sheria na wapo walioniunga mkono lakini lengo langu lilikuwa ni kusema maumivu kutokana na tunayoyapata juu ya hawa CDA
-Naandika hili andiko kutokea katikati ya Nchi yetu ya Tanzania,Katikati ya Mkoa wetu wa Dodoma yaani Dodoma manispaa naomba Watanzania wote wajue FURAHA YETU DODOMA juu ya Mamlaka ya ustawishaji makao makuu(CDA)kufutwa RASMI na kuwekwa chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma sio kwa utashi wa Mtu ila ni Mungu.
-CDA ni nini labda kama unataka kujua japo sio lengo langu sana kuwaambieni hilo kwani halina umuhimu tena kwasasa,chenye umuhimu ni kwamba hayo Mamlaka waliyokuwanayo ambayo waliyatumia vibaya kwa kupora Ardhi za Wananchi wa Dodoma hawana tena na waliosema sana kuhusu jambo hili bado wako hai hawajafa hata mmoja.Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu(CDA) ilianzishwa mwaka October.1973 baada ya Serikali kuweka adhima ya kuhamisha Makao Makuu kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma na miaka michache baadae CDA walianza kufanyakazi ambayo ilikuwa kinyume na Maelekezo waliyopewa
mfano:-kazi yao kubwa ilikuwa ni kupima ardhi,kupanga miundo mbinu na kuikabidhi Halmashauri wao ndo watagawa viwanja(hii walifanya maeneo ya area C na nkuhungu)kinyume na hapo CDA wakageuka mwiba na kuanza kupora Ardhi ya wananchi kuwanyanyasa na kujiweka juu ya Halmashauri wakijiita wao ni Serikali kuu kwani Azimio limesainiwa na Rais na hata kiutendaji wapo chini ya Serikali kuu.Sasa naomba turudi kwenye UNABII niliosemea maana haya mengine sio dhumuni langu kuyaandika.
-BENSON SINGO KIGAILA(aliyekuwa mgombea wa ubunge Dodoma mjini kupitia Chadema/Ukawa 2015,nauona unabii hapo)tofauti na vyeo vyake na uzoefu wake kwenye chama pia namfahamu kama mwanzilishi wa Harakati za kuwaondoa CDA hapa mjini,waulize wananchi wa Msangalale,Chidachi/Chinyoya,Dodoma Makulu,Mji Mwema Chang'ombe,Mbuyini Kizota na sehemu nyingi nyingine ambazo walisumbuliwa na CDA kwenye Ardhi zao na alipokuja KIGAILA alisema tuondoe KICHAA NA MAKOPO YAKE,hii ilikuwa kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wala Uchaguzi Mkuu
UNABII WA BENSO SINGO KIGAILA
-Wakati wa mikutano na Vikao vya ndani kabla ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu na ule wa Serikali za mitaa alikuwa akisema mara kwa mara maneno haya nanukuu
"Mkinichagua kuwa Mbunge wenu,Mkachagua Madiwani tikaunda Halmashauri na Kumchagua Mh Lowassa kuwa Rais wa Tanzania,baada ya kuapishwa nitakuja na tutaandika MABANGO MANNE LA KWANZA TUTAWEKA MTUMBA,LA PILI TUTAWEKA MAKUTUPOLA,LA TATU TUTAWEKA MSEMBETA NA LA NNE TUTAWEKA MPUNGUZI,TUTAYAANDIKA DODOMA CDA MARUFUKU"mwisho wa kunukuu
-Maneno haya niliyo nukuu yalikuwa ni Ajenda ambayo iliugwa mkono sana Dodoma kutokana na matatizo ya CDA na wananchi wetu,japo BENSON hakushinda Ubunge lakini kwa namna yalivyougwa mkono Mawazo yake juu ya CDA leo tumeona wameamua kuwaondoa CDA sio kwa kuwa hawatendi haki maana wamekuwa hivyo miaka yote ila wamewaondoa kwakuwa wanaogopa uugwaji mkono aliopewa Benson na wana Dodoma.
MADIWANI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA DODOMA WANAOTOKANA NA CHADEMA
-Dodoma mjini tuna Madiwani WANANE tu ambao SITA madiwani wa kata na WAWILI ni Madiwani wa Viti maalumu naomba tuwatambue kwa Majina yao
1.PASCAL MATULAH( Dodoma Makulu)
2.HEZRON KUDUGWA(kata ya Iyumbu)
3.JAMAL NGALYA(kata ya kizota)
4YONA E KUSAJA(kata ya Kikombo)
5.ROY MBALAY(viti maalum)
6.SAID L KITEGILE(kata ya madukani)
7.SAMWELI MZIBA(kata ya Hazina)
8.HADIJA MAULA(viti maalum)
-Hawa nao kuanzia kipindi cha Kampeni za Uchaguzi Mkuu walikuwa wakisemea sana swala la CDA kufutwa na kuondolewa maana wamekuwa wakinyanyasa sana Wananchi wa Dodoma,baada ya Mashinikizo ya Madiwani wa CHADEMA mpaka baraza la Tarehe 02.May.2017 Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya dodoma(KUNAMBI)aliamua kutangaza kuwa wataitisha baraza maalumu la Madiwani ili kuiazimia CDA kuondoka Dodoma.hapa napo UNABII wa Madiwani wetu umetimia!
KUNTI MAJALA YUSUPH(mh Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Dodoma) pamoja na namna ambavyo alipambana kupigania haki za wanadodoma tangu miaka ya nyuma lakini pia kuachilia mbali cheo chake kwenye chama lakini yeye pia ni Mkazi wa Dodoma na ameonja Adha ya CDA na kwenye hili bunge linaloendelea la Bajeti(bunge hili la Kumi na Moja)kwenye kipindi cha kumuuliza Waziri Mkuu maswali ya papo kwa hapo alimuuliza Waziri Mkuu kuhusu maswala ya CDA,inawezekana wengine hamkuona umuhimu wa swali lile lakini sisi hapa Dodoma tiliona ametutendea jambo kubwa na la kiugwana ambalo linanyanyasa asilimia kubwa ya wanadodoma.Huu nao ulikuwa ni UNABII ambao leo umetimia na Mh Kunti ameingia kwenye Historia yetu Dodoma kupigania CDA iondoke japo yapo mengi anayopigania ila hili ni kubwa kwasasa.
RAIS KUIFUTA MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU(CDA)
-Asante kwa kuiondoa maana ni jambo lililokuwa kwenye mamlaka yako lakini mimi binafsi najua nia haikuwepo tangu mwanzo ndo maana Bwana Rais ALIAMUA KUMTEUA KAIMU MKURUGENZI KUWA MKURUGENZI na hii aliifanya baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015,sasa kilichomsukuma leo kuifuta CDA inawezekana kabisa ni NENO LIMEUMBA walivyosema baadhi ya watu kama nilivyotangulia kueleza au shinikizo kutoka kwa Madiwani wa CHADEMA Dodoma Mjini au Mbunge Viti Maalum Dodoma.
UNABII WANGU SASA kwakuwa CDA imeondoka na sasa Dodoma Jimbo limeondoka asubuhi na mapema
NB:
WAOGA NA WASIO WAOGA WOTE WAKIKOSA USALAMA NA KUDHURIKA WANAWEZA KUFANYA MAAMUZI KWA UJASILI MARA MBILI ZAIDI YA ANAYE WATISHA
Tanzania naipenda sana,Dodoma naipenda sana mimi ni muumini wa HAKI