Kila kitu mbona kipo okey, jambo ambalo limekwamisha hadi sasa ni mazungumzo juu ya mgogoro wa kikatiba tuu, Maalim Seif atakuwa ni Rais wa aina gani? hilo ndio suali ambalo maalim lililompeleka kwa Magufuli, wao CCM wanataka awe kama hawa wengine waliopita, yaani ZNZ tuwe hatuna mamlaka kamili, serikali ziwe hizi hiz 2 na maalim aingie ktk baraza la Magufuli akiwa kama wazir asie na wizara maalum na asiingie kama makamo wa rais kama ilivyokuwa katiba ya mwanzo ambayo ilimpa mamlaka rais wa ZNZ kuwa makamo wa rais wa Jamuhuri ya Muungano, sasa maalim yy kama yy kakataa hivyoo.Mwenyew anasema kama Munataka Seif awe rais tuu basi mungekuwa mushasahau wazanzibar lkn rais asokuwa na mamlaka yyte yaleee.Kwa taarifa za ndani ni kuwa ilifika wakati viongozi wote wa CUF walikuwa wameshambadilikia maalim Seif juu ya kuzorota kwa wao kupewa serikali na ikawa mzozo mkubwa mnoo juu ya viongozi hao na maalim seif kwani wao walimtaka maalim awaache wananchi wadai haki yao wenyewe kama ameshindwa kwa njia ya kidiplomasia na ndipo hapo maalim ikabidi awape ukweli wa mambo ulivyoo.Na hata kikao cha juzi baina ya watu watatu Ikulu ua Bara kilikuwa na ajenda ya kumshawishi Samiya aachie nafac hiyo na awe nayo maalim atakapokuwa rais wa ZNZ kilichoafikiwa bado ni siri juu ya mzozo huo.Lkn suali la maalim kuwa rais mbona hilo limemaliza lkn ndio kuna hayo mazungumzo juu ya mgogoro wa kikatiba tuu na kwa taarifa kuwa tayari wameshalipatia muarubaini wake kwani Magufuli kashawambiya kuwa mtu awe rais halafu asiwe na mamlaka hilo haliwezekani kabbisssa kwa hiyo tukae mkao wa kula Mwaka mpya na Rais mpya.Hili pia limethibitishwa na Wazir wa mambo ya ndani wa Tanz juzi alipokuwa akiongea na mabalozi wa nchi mbali mbali kuwa suali la ZNZ limemalizika kwani matokea yalisitishwa na hayakufutwa na muda si mrefu yataendelezwa kutangazwa hili lilitokana na mabalozi kutowa muda wa wiki moja juu ya suali la znz kinyume na hivyo wataondowa mabalozi wao wote nchini Tanzania na ndio ikabidi haraka haraka awaite na kuongea nao.Pia kama hiyo haitoshi wazir huyo huyo wa mambo ya nje alipotumwa na Magufuli aende akasuluhishe mgogoro wa Burundi, Kufika tuu akaambiwa ya kwenu yanawashinda kwanza nenda kasuluhishe ZNZ ndio halafu uje kwetu hapo ikabidi na wao awaambie ukweli kuwa kwetu kila kitu kimemaliza na ndio maana nikaja huku isipokuwa kuwa mambo madogo tu juu ya Mfumo wa uendeshaji na tayari tumeshakubaliana kwa hiyo muda sio mrefu mutapata taarifa njema juu ya mgogoro wa ZNZ. Mambo yamekwisha jamaniii kimya kingi tu hicho lkn kina ......................................!!!! INSHAA ALLAH!!!!