CCM yatafuta kick Moshi

Malata Junior

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Posts
3,108
Reaction score
2,553
Heshima mbele wadau.
Baada ya chama cha mapinduzi kufutika kabisa katika ramani ya kisiasa manispaa ya Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla sasa wanajaribu kutafuta kiki ya kutokea kupitia mlango wa madhehebu ya dini.

Chama cha mapinduzi kimeandaa 'maombi' ya kumuombea Rais Magufuli jumamosi 20 Februari 2016 yatakayotanguliwa na maandamano yatakayoanzia katika ofisi za CCM mkoa na kuishia stendi kuu ya mabasi mjini Moshi ambako 'maombi' hayo yatafanyika!

Katibu wa CCM mkoa ndugu Ruta amesema maandamano na 'maombi' hayo hayana itikadi na kuwaomba wananchi wote washiriki lakini cha kushangaza shughuli zote zinaratibiwa na CCM na gari la CCM ndiyo linatangaza 'maombi' hayo!

Hata hivyo viongozi wa madhehebu yanayoheshimika mkoani Kilimanjaro kanisa katoliki,KKKT na Bakwata wamegoma kushiriki kwenye maombi hayo kwa madai kwamba hawashiriki shughuli za kisiasa na kuwa kama ni maombi kwa Rais wetu yanapaswa kuratibiwa na madhehebu ya dini yenyewe na kufanyika sehemu inayostahili na siyo stendi ya mabasi ambako kuna walevi na wahuni wa kila aina ambao wanaweza kupelekea uvunjifu wa amani na kudhalilishwa kwa viongozi wa dini.Kwa sababu hiyo 'maombi hayo yataendeshwa na madhehebu ya 'uchochoroni'

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa mkoani hapa wanasema kitendo cha CCM kuandaa 'maombi' stendi kunatokana na hofu ya kukosa mahudhurio endapo yatafanyika sehemu rasmi,hii inatokana na CCM kutokukubalika kabisa mkoani Kilimanjaro. Pia wamemtaka Kamanda wa Polisi RPC kuzuia 'maombi ' hayo ili kuepusha kero kwa abiria badala yake wayahamishie kwenye viwanja vinavyotumika kwa mikutano ya kisiasa na kidini ambavyo viko vingi mjini Moshi.
 
Baada ya hayo maombi..UKAWA waruhusiwe kuwashukuru wapiga kura wao na wafanyie mbali na mjini kama vlie viwanja vya Memorial karanga.Mgeni rasmi awe Lowassa.Kikwete pia akaribishwe.
 
Kwanini wasifanyie hayo maombi yao ktk ofisi za ccm koa?na wamwombe mwigulu aongoze hayo maombi yao
 
Baada ya hayo maombi..UKAWA waruhusiwe kuwashukuru wapiga kura wao na wafanyie mbali na mjini kama vlie viwanja vya Memorial karanga.Mgeni rasmi awe Lowassa.Kikwete pia akaribishwe.
Daaaaaaa,hapo naona umejitafutia mitusi toka kwa viwavi subiria mkuu
 
tunaomba hayo maandamano yaruhusiwe na kupewa baraka zote na yalindwe na polisi ila wasije wakagomea kuruhusu maandamano ya kupinga uchaguzi wa Zanzibar
 
Yaan kwa hapa Moshi ccm wana kazi kubwa sana .....kama kuna pesa watapata wafuas wengi sana
 

Yangekuwa hayana Itikadi yangeanzia mahali neutral na si ofisis za chama.
 
Lowasa kuwashukuru wananchi wake kwa kumpigia kura ni dhambi chama cha majangiri kuandamana kuwaombea majangiri waibe vizuri si dhambi kweli kuishi na hiki chama bora uisha na makaburi.
 
CCM sio moshi2...ni TZ nzima hakina nafas....ila wizi unawaweka madarakani..
yanamwisho hayo.
 
Mkuu uliyosema kimsingi yana ukweli, lkn je ni hilo tu ulililo liona juu ya ccm?hujawahi kuona mambo mengi machafu zaidi ya hayo yanayo andikwa na wana ccm juu ya viongozi wa upinzani?tena maneno machafu kabisa nashindwa hata kuyaandika hapa jukwaani hujayaona?nakama umesha yaona mbona hujawahi kukemea kama ulivyokemea hili?
 
Lowasa kuwashukuru wananchi wake kwa kumpigia kura ni dhambi chama cha majangiri kuandamana kuwaombea majangiri waibe vizuri si dhambi kweli kuishi na hiki chama bora uisha na makaburi.
Inasikitisha sana mkuu
 
UNASEMA KINYUMENYUME, NI MOSHI NDIYO INAYOTAFUTA 'KICK' CCM!
 
Wanatafuta kiki kama idri. na wem.,kaskazini tunasema mama "jeni" bai bai [ccm]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…