CCM yasaka ngwe mpya bila lolote la kujivunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yasaka ngwe mpya bila lolote la kujivunia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by M-mbabe, Jun 27, 2010.

 1. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  MILANGO ya kinyang’anyiro cha urais wa Jamhuri ya Muungano na ule wa Zanzibar, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefunguliwa katikati ya mazingira magumu ya maisha ya wananchi wengi.
  Hadi juzi Jumatatu, wanachama sita wa chama hicho, tayari walijitokeza katika kuchukua fomu ya kuwania urais Zanzibar. Miongoni mwao, ni makamu wa rais wa Jamhuri, Dk Ali Mohammed Shein.
  Wengine ni waziri kiongozi mstaafu, Dk. Mohammed Gharib Billali, Balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Abeid Karume, Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna na Kamishna wa Idara ya Utamaduni Zanzibar, Hamad Bakari Mshindo.
  Hii ni mara ya tatu kwa Dk. Billali kugombea urais wa visiwa hivyo. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2000.
  Pamoja na kwamba aliongoza kura za maoni ndani ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Zanzibar, lakini alishindwa katika kura zilizopigwa na NEC mjini Dodoma.
  Katika uchaguzi wa mwaka 2005, Dk. Billali alichukua fomu kumpinga rais wa sasa, Amani Abeid Karume, lakini alipozwa kama Kikwete alivyopozwa mwaka 1995 na kumwachia Benjamin Mkapa kugombea.
  Kwa upande wa urais wa Jamhuri, Rais Jakaya Kikwete amekuwa mwanachama wa kwanza wa chama hicho kuchukua fomu kutetea nafasi yake. Haitarajiwi kuwapo mwanachama mwingine kumpinga Kikwete.
  Iwapo atapitishwa na hatimaye kushinda katika uchaguzi utakaoshirikisha wagombea wengine wa upinzani, Kikwete atakuwa anakamilisha muhula wake wa pili na wa mwisho wa urais kwa mujibu wa katiba.
  Tayari mwanachama pekee “aliyejiapiza” kumtoa Kikwete katika kiti chake, John Shibuda, ametangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro cha sasa. Anasema hataki tena urais; badala yake nguvu zake amezielekeza katika ubunge.
  Ni Shibuda huyu aliyenukuliwa akisema kuwa akiwa kada anayekijua vizuri chama chake, anaona wazi kuwa CCM kimekuwa chama cha kisultani.
  Alisema hawezi kuwa mnafiki kwa kusema CCM ipo imara na imebaki katika mstari wake uleule ulioasisiwa na viongozi wake, wakati ukweli haiko hivyo.
  Hata hivyo, kinachofahamika kwa wengi, ni haraka ya serikali kumega jimbo la Maswa, ambalo Shibuda analiwakilisha bungeni kwa kuunda majimbo mawili – Maswa Mashariki na Maswa Magharibi.
  Ni umegaji huo, unaodaiwa na baadhi ya watu kuwa umechangia kumlainisha Shibuda. Kabla ya serikali kumega jimbo la Maswa, hali ya kisiasa ya Shibuda ilikuwa ya utata.
  Mara kadhaa Shibuda mwenyewe amelalamika kuhujumiwa. Ametuhumu katibu mkuu wa chama, Yusuph Makamba, mwenyeviti wa mkoa, Hamis Mgeja na viongozi wengine wa wilaya, kwamba “wanatengeneza njama” za kumuangamiza kisiasa.
  Hata kama Shibuda na wenzake, wangesukiwa zengwe kama ilivyofanyika kwa Dk. Billali mwaka 2005, lakini hatua yao ya kugombea angalau ingekisaidia chama chao.
  Ari ya wanachama na hata wananchi wa kawaida kukipenda chama ingepanda. Mijadala miongoni mwa wanachama na viongozi, ingeibuka. Nidhamu ndani ya chama na kati ya wanachama na viongozi, ingerejea kama awali.
  Lakini unafiki huu wa kumpitisha Kikwete bila kupingwa au kumuachia ngwe ya pili, hauwezi kukijenga chama, wala Kikwete. Utaangamiza chama na Kikwete mwenyewe.
  Haitakuwa ajabu iwapo huyu ndiye atakuwa rais wa mwisho kutoka CCM. Ni kwa sababu, hata miongoni mwa “wanafiki” walioogopa kumpinga, kuna wanaojua kuwa umaarufu wake umepungua, ikilinganishwa na mwaka 2005 na kwamba sasa ameonekana kushindwa kuongoza.
  Wanajua kuwa uchumi umeporomoka. Wafadhili wamekatalia misaada. Heshima ya serikali ndani na nje ya nchi imeshuka, tena kwa kiwango kikubwa.
  Matumizi ya serikali yameongezeka maradufu ukilinganisha na mtangulizi wake. Hata vipaumbele vya serikali yake haviko wazi.
  Je, kipaumbele cha serikali ni kutengeneza vitambulisho vya taifa, au kufufua Shirika la Reli (TRC)? Kipi cha haraka hapa?
  Nini kinachohitajika kwanza, kuboresha huduma za afya, shule, zahanati na hospitali au kuongeza majimbo mapya ya uchaguzi?
  Nini kifanyike sasa na kipi kifanyike baadaye. Serikali ijikite katika kukusanya kodi na kutumia kodi hiyo kwa kujengea miundombinu thabiti, au kukusanya na kutumbua kwa safari za nje zisizo na tija?
  Kwa mfano, nani anaweza kutetea Kikwete, kwamba safari yake nchini Jamaica ambako alionekana akibembea ilikuwa na tija. Je, ilileta misaada na ilichochea uwekezaji nchini?
  Nani anajua, kwa mfano, mkakati wa serikali ni upi katika kuzalisha ajira kwa kulinda viwanda na makampuni ya ndani? Uko wapi mkakati wa serikali wa kulinda viwanda vya ndani na makampuni makubwa ya kibiashara na usafirishaji?
  Kama Kikwete angekuwa na mipango thabiti ya kulinda makampuni ya ndani, mashirika ya serikali na taasisi zake, asingekubali kuona kampuni kubwa ya usafirishaji wa abiria na mizigo – Scandinavia ikiyumba.
  Ni lazima serikali ingesimama imara na kuitafutia mtaji na hata mkopo ili kuikoa. Ni ajira ngapi zinaweza kupotea, iwapo kampuni hii itaachwa kusambaratika? Ni kiasi gani cha kodi ambacho serikali itapoteza kwa Scandinavia kusitisha huduma zake?
  Ni wananchi wangapi waliokuwa wanategemea kampuni hii kimapato au kuwahudumia kwa kuwafikisha wanakotaka, ambao tayari wameathirika kwa kampuni kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi?
  Badala ya kusimamia haya, rais anakimbilia kuanzisha mikoa na wilaya mpya. Yawezekana akaeleweka kuwa amelenga kutoa ajira kwa marafiki zake watakaomsaidia katika kipindi hiki cha kampeni.
  Vinginevyo, katika hali ya kawaida, hakuna kipya kitakachopatikana. Serikali inasema inaanzisha mikoa mipya ili kuwezesha huduma kupelekwa karibu na wananchi.
  Hii hiatakuwa mikoa wala wilaya za kwanza kuwa ndogo. Kama hivyo ndivyo basi, mbona hadi sasa hakuna huduma katika mikoa midogo na wilaya ndogo zilizopo? Zinazoundwa zitapataje huduma na kwa miujiza ipi?
  Taifa hili limekuwa na mikoa 26 kwa miaka mingi sasa, lakini hicho kinachoitwa, “huduma za karibu na wananchi” kimekuwa mbingu na ardhi.
  Mikoa mipya itahitaji watawala, wataalamu na vitendea kazi. Kama serikali imeshindwa kuboresha vitendea kazi katika mikoa iliyopo sasa, itawezaje katika mikoa mipya?
  Leo, katika miaka minne ya utawala wa Kikwete, wafadhili wamekata sehemu kubwa ya misaada. Deni la taifa limepanda mara mbili, kutoka zaidi ya Sh. 5 trilioni hadi 10 trilioni. Kuna kila dalili kwamba nchi inarejea katika hadhi ya kutokopesheka.
  Ndani ya chama cha Kikwete, hakuna anayejua kama CCM inaendeshwa kwa kanuni na dira, au utashi wa viongozi. Ni kwa sababu, chama hicho kinahubiri kuondoa unyonge, lakini wakati huohuo kinashabikia unyonyaji.
  Hata misingi iliyowekwa na vyama hivi viwili – TANU na ASP, kupambana na “unyonyaji na usultani,” imeachwa na sasa CCM haionekani kutetea mfanyakazi na mkulima katika mazingira hatari ya unyonyaji mpevu.
  Katika mazingira haya, ambamo fomu zinachukuliwa kuwania utawala kwa kipindi cha pili cha utawala wake, Kikwete hawezi kutamka kwa uthabiti ile kauli mbiu yake ya “maisha bora kwa kila Mtanzania.”
  Hata viongozi wake hawana ubavu wa kusimamia kauli hiyo, labda wafanye hivyo kwa watu ambao hawajui kinachotendeka ndani ya serikali na katika chama. kwani gharama ya maisha kwa wananchi imepanda.
  Hayo yakifanyika, chama cha Kikwete kinaendelea kutota. Uhai wake ni kelele na ubabe wa kauli.
  Hali hiyo ndiyo iliyosababisha Makamba, katibu mkuu, kubeba wahamiaji kutoka vyama vya upinzani na kuwapa vyeo na kuacha makada waliokibeba chama chao kupitia mazingira magumu.
  Kikwete anajiandaa kwa uchaguzi akiwa anatuhumiwa na wenzake ndani ya chama kwa kukalia taarifa ya Kamati Maalum iliyoundwa na NEC na kupewa kazi ya kutafuta chanzo cha mpasuko ndani ya chama na katika Bunge. Ilikuwa chini ya Rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi.
  Kisa? Inadaiwa waliotajwa kuwa vinara wa mpasuko, ni maswahiba zake wawili – Edward Lowassa na Rostam Aziz. Hili nalo linaendeleza mpasuko ndani ya chama chake na kuongeza pia idadi ya makundi.
  Hivi sasa makundi hayo yamepanuka na kuingia katika ngazi ya ubunge. Vita kati ya Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Batilda Burian na mbunge wa sasa wa Arusha mjini, Felix Mrema, ni kielelezo kingine kuwa hali si shwari.
  Katika mkoa wa Mbeya, rais anajua kuna makundi yanayotokana na yeye mwenyewe kuendelea “kumbeba” Mkuu wa Mkoa, John Mwakipesile anayetuhumiwa kupambana waziwazi na mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe.
  Hivi sasa, vita imeongezeka kwa kumuingiza Profesa Mark Mwandosya ambaye alipambana na Kikwete mwaka 2005. Naye anadai kufanyiwa hila kwa malengo ya kumwangamiza kisiasa.
  Katika mazingira hayo, haikutarajiwa Rais Kikwete kupita bila kupingwa. Hatua hiyo ya kutopatikana angalau mtu wa kumkosoa na kuwaambia wanachama msimchague Kikwete kwa kuwa ameshindwa hili au lile, hakujengi chama chao
   
Loading...