Taasisi yakutathmini utawala bora ilipokutana na CCM, Shibuda kama mwanachama wa hiyotaasisi, baada ya mazungumzo rasmi, alitaniana na Kikwete na akamwambia anatakakuwa mgombea binafsi na yeye Kikwete amuunge mkono.
Na ni kutokana na utani huondio maana kikwete kazungumzia mgombea binafsi. Watu wote waliopo karibuwanasema Shibuda hajazungumzia kugombea urais kupitia CHADEMA.
Lakini kauli ya Shibuda imepindishwa kuwavuruga wapinzani. Na BAVICHA kwa kukosa umakiniimeanza kupiga kelele kutokana na kile ilichosoma katika magazeti kama vilemagazeti yetu siku zote yanaandika ukweli.
Sitegemei Shibuda kulifafanua hilikwasababu na yeye kama binadamu wengine ana-pride yake, kwanini BAVICHA HAWAJAWEZAHATA KUMPIGIA SIMU. Huu ni mfano wazi wa kukosa umakini. Na inawezekana huyo Heche ambaye CHADEMA wasiokuwa na upeo wanamsifia ni usalama wa taifa, kwanini kitu kilichozungumzwa katika maudhui ya utani akakipaisha juu kila mtu ajuwe, kwanini viongozi wa kitaifa wa CHADEMA hawajamdhibiti huyo Heche, hivi wanafikiri anasaidia chama au masilahi yao binafsi. Kuna uwalakini katika hili la kumuachiaHeche (BAVICHA) amuandame Shibuda kwa kauli ambayo haijathibitishwa, na ulakinihuo utafanya watu wakae upande wa Shibuda. Ni mpango uliokosa umakini hata kamailikuwa nia ya Mbowe kumuangamiza Shibuda kisiasa.
Why BAVICHA (CHADEMA) IS SO EASY TO BE MANIPULATED BY MEDIA AU CCM?
Ingawa Shibuda hakuzungumzia kugombeakupitia CHADEMA bali kupitia mgombea binafsi anayo haki ya kuhoji kuna ubayagani yeye kutangaza nia ya kugombea.
Hiki ni kitu kidogo lakini kimekuzwa kwakukosa umakini, kwasababu mtu akitangaza nia sio maana yake jina lakelitapitishwa na CHADEMA, lakini ukweli unabaki Shibuda alizungumzia mgombeabinafsi na sio kugombea kupitia CHADEMA, haya mengine yote yametengenezwa navyombo vya habari pamoja na BAVICHA kama sio CCM.