Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Katika wagombea 163 waliotia nia kugombea udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Manispaa ya Moshi ni 21 pekee wamepitishwa kuendelea na mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, sawa na asilimia 12.9 ya waliokuwa wakiwania nafasi hizo.
Aidha, nafasi za viti maalumu zimechukuliwa na wagombea wanane kutoka tarafa za Moshi Mashariki na Moshi Magharibi, kila upande ukiwakilishwa na wanne.
Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini, Frida Kaaya ameeleza hayo leo Agosti 16, 2025 katika ofisi za CCM Wilaya ya Moshi Mjini wakati wagombea walioteuliwa wakikabidhiwa barua za uteuzi kwa ajili ya kwenda kuchukua fomu za kugombea.