CCM yanadi serikali mbili Misikitini - Singida

CCM yanadi serikali mbili Misikitini - Singida

KALOKAZA

Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
95
Reaction score
135
CCM yanadi serikali 2 misikitini



Na Mwandishi wetu


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinadaiwa kuwatumia baadhi ya masheikh kuhubiri muundo wa muungano wa serikali mbili misikitini.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, kampeni hiyo inasimamia na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye yuko ziarani mkoani Singida, akishirikiana na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.



Chanzo chetu kimedokeza kuwa, chama hicho kinatumia sherehe za Maulid kupenyeza ajenda yake ya serikali mbili na kuwaponda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wanaotetea serikali tatu zinazopendekezwa na rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


Inadaiwa kuwa katika sherere za kwanza zilizofanyika Kata ya Shelui wilayani Iramba, Sheikh Salum na baadhi ya viongozi wa dini hiyo, walitumia muda mwingi kuwaponda Ukawa wakitaka wananchi wasiwasikilize.



Alipotafutwa na gazeti hili, kufafanua tuhuma hizo, Sheikh Salum alisema; “ni kweli mimi nipo mkoani Singida kwa shughuli za Maulid, kuhusu mambo ya serikali tatu, ungewauliza wale waliokuambia wewe”.



Wakati Sheikh Salum akikwepea tuhuma hizo, mmoja wa masheikh mkoani Singida, alilalamika kuwa hawakutarajia viongozi hao wa dini kufanya siasa misikitini kwa kutumia mwavuli wa Maulid na kuanza kupinga rasimu ya tume ya Jaji Warioba, jambo alilodai linaweza kuleta mgawanyiko kati ya Waislamu wenyewe.
“Walahi mwandishi! Mimi nimechukizwa na kitendo cha Sheikh Salum kuwa mgeni rasmi na kuanza kupinga maoni ya tume ya Jaji Warioba.
“Na leo (jana) tuna Maulid nyingine katika Msikiti wa Mitunduruni, ambapo Kinana atakuwa mgeni rasmi, watakuwa pamoja na wale waliokuwa wanapinga serikali tatu,” alisema Sheikh huyo.
Kinana hakupatikana kujibu madai hayo, lakini Sheikh wa Mkoa wa Singida, Alhaji Salumu Mahami alithibitisha kuwa Maulid itafanyika usiku wa jana kuanzia saa tatu usiku katika msikiti wa Mitunduruni hadi saa saba, na mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Kinana.



“Maulidi itakuwepo, Kinana ni mgeni rasmi, japokuwa sisi hatukumpa mwaliko rasmi ila yeye aliomba tumteue awe mgeni rasmi na ahudhurie kwenye Maulid hiyo,” alisema Sheikh Mahami, ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Singida.


Sheikh Salum na Sheikh Mahami ni wajumbe wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Taifa, na msimamo wa baraza hilo tayari unafahamika.
Machi 30 mwaka huu, Bakwata lilisema Waislamu wanataka Katiba itakayojali maslahi kwa wananchi wa pande zote mbili Bara na Visiwani na kuhakikisha Muungano unadumu.
Aidha, Baraza hilo liliunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyotoa wakati wa ufunguzi wa Bunge Maalum la Katiba kuwa imewapa Watanzania upeo mpana zaidi katika kutafakari suala la upatikanaji wa Katiba.



“Baraza la Ulamaa la Bakwata linaona si sahihi Waislamu wote kubebeshwa fikra na mtazamo wa serikali tatu, sisi kama viongozi wa Kiislamu tunasema Katiba tunayotaka ni ile itakayoleta maslahi kwa wananchi wa pande zote mbili na kuhakikisha Muungano wetu unadumu,” alisema.


 
Huku ni kutapatapa watani zangu wamezidiwa kila kona sasa hata wakiona unyasi wanadhani utawasaidia Tangu lini mgeni rasmi akajiombea yeye mwenyewe!!? Aibu kubwa kwa Kinana na CCM pia loh......!!!?
 
Acha wajichanganye kwa kikombe cha kahawa lkn wajue katiba ya wananchi lazima na sisi waisilam na wakristo 2meungana
 
Kwa hili la rasimu ya Warioba imekula kwao na walianzishe vyovyote na mahali kokote lakini wasije lalamika hapo baadae
 
Kwa hili ccm imekula kwao bigtime,acha waendelee kuchochoa kunia mbichi

"UNAWEZA KUONGOZA WATU KWA MDA MREFU ILA HUWEZI KUONGOZA WATU MILELE"
 
Wakati mwingine ukiwafikiria viongozi wa ccm huwa wana ghani kama malaika lakini wanatenda kama mashetani wanywa damu.

1. rasimu ya katiba ni maoni ya wananchi, wananchi hao wako misikitini na kanisani, walio chagua muundo wa serikali tatu/mbili/nne wako misikitini na kanisani. Najiuliza; hivi kiongozi anajitoaje ufahamu na kwenda kuongea kwenye nyumba ya ibada mfumo anao utaka yeye huku akijua nyumba hiyo ya ibada kuna watu wenye itikadi na mawazo tofauti juu ya mfumo?! si kutafuta migawanyiko kwenye nyumba za ibada?!

2. Lukuvu alishafanya uchochezi mkubwa akiwa kanisani kwa kusema "Zanzibar niya waislamu watupu wakiachwa wenyewe wale ile inchi itageuka kuwa ya kidini..."; Najiuliza, kinana anajibu mapigo ya Lukuvi kwa kufanya siasa msikitini kwa kuwa Lukuvi alifanya siasa kanisani?! Ndivyo walivyo ambizana/kukibaliana kuwa sasa serikali mbili agenda inahamia kwenye nyumba za ibada?!

3. Kama wanaona kuwa serikali mbili zinafaa na ndio wananchi wengi wanazozihitaji, wanahangaika nini kwenye nyumba za ibada?! si wapitishe hiyo rasimu ya Warioba ambayo kwa maoni yao (ccm) ni mbovu ili sisi wananchi tuje tuikatae kwa kuwa imebeba mfumo wa serikali tatu ambao ni mbaya ili tupitishe hizo mbili wanazotaka wao?!
 
Hizi ni bangi zingine kwa bavicha kwa sababu mada imegusa uchochezi wa kidini hatutachangia sana lakini tungeweza kuwawekea video ambazo lipumba anafanya mambo yake msikitini na slaa kanisani lakini ujinga wa mada za kidini tumezisusa siku hizi pengine nikuwekee picha uone ccm inavyofanya kazi kwa watu wala siyo msikitini na kanisani.
 
Huku ni kutapatapa watani zangu wamezidiwa kila kona sasa hata wakiona unyasi wanadhani utawasaidia Tangu lini mgeni rasmi akajiombea yeye mwenyewe!!? Aibu kubwa kwa Kinana na CCM pia loh......!!!?
Kinana siyo mwepesi kama slaa ngoja mda ukifika mtajua alikuwa anafanya nini kwa watanzania hizi porojo zenu za uongo hata vitanda mlivyovitandika mtavitandua tu twendeni pamoja wakati utamati kabisa.
 
Acha wajichanganye kwa kikombe cha kahawa lkn wajue katiba ya wananchi lazima na sisi waisilam na wakristo 2meungana
Unazungumzia wanachi gani hiyo rasimu ni mawazo ya huyu mtu wala siyo mawazo ya wananchi ndiyo maana kwa sasa hana amani kanisa baada ya kulikoroga kwa kuleta mawazo yake.
 
Hizi hoja nyepesi za ukawa na bavicha mmemtumia kakobe hamjapata matokea mazuri sasa mnaanza uongo live subirini dawa iingie kinana ni mmoja lakini vyama vitatu vya ukawa amevitoa jasho sasa mnaweza uongo wa wazi kabisa.
 
Ukawa wamepwelewa aibu watakayovuna hawataamini watafute pakuficha sura zao hii zaidi kunyewa na bundi yani mbatia ,mbowe,lipumba,slaa na malimu sefu wote hawa kinana anawavuruga mpaka kufika hatua ya kutunga uongo kwani hapa kinana alikuwa wapi mtasema tena msikitini?View attachment 159695
 
Hizi hoja nyepesi za ukawa na bavicha mmemtumia kakobe hamjapata matokea mazuri sasa mnaanza uongo live subirini dawa iingie kinana ni mmoja lakini vyama vitatu vya ukawa amevitoa jasho sasa mnaweza uongo wa wazi kabisa.
Ili mjue kuwa alikuwa msikitini subirini alambwe kofi huko. Chezea wanaofata dini ya haki wewe. Muulizeni mwinyi
 
hata msikitini ni sawa tu, waumini ni wananchi pia, wanastahili kuhabarishwa na kuombwa mawazo yao pia, ili mradi isiwe kukandia dini nyingine.
 
Unazungumzia wanachi gani hiyo rasimu ni mawazo ya huyu mtu wala siyo mawazo ya wananchi ndiyo maana kwa sasa hana amani kanisa baada ya kulikoroga kwa kuleta mawazo yake.

Aunt buku 7 zinakutoa ufahamu kiasi hiki?
Hapo kwa huyu Mheshimiwa husogei hata nukta kaa mbali kabisa...
Halafu acha kuongopea watu Warioba ni kiongozi tu,
tunaelewa waliokuwepo kwenye tume na CV zao sio wewe pimbi maji.....Pambaf....
 
Back
Top Bottom