CCM yameguka vipande | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yameguka vipande

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Jan 20, 2012.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kundi la mafisadi lajigamba kukiteka chama
  Siasa za chuki, visasi, kuchafuana zashamiri
  Wapinga ufisadi ndani ya CCM wahofia usalama wao

  Waandishi wa habari, viongozi wa dini nao watumika

  INGAWA imebaki miaka mitatu mpaka kufanyika uchaguzi mkuu mwingine nchini, mbio za Urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinaendelea kukimaliza chama hicho tawala, huku genge la mafisadi likijitangazia ushindi baada ya CCM kushindwa kutekeleza azma ya kujivua gamba.


  CCM yenyewe imekiri hadharani kuwa kuna makundi kadhaa ndani ya chama hicho ambayo yanapiga kampeni kuhakikisha kuwa mgombea wao anaibuka Rais wa Tanzania kwenye uchaguzi wa 2015.


  Uchunguzi wa KuliKoni umebaini kuwa hali si shwari ndani ya CCM kutokana na mvutano mkubwa wa chini kwa chini unaoendelea, huku genge la wanasiasa waliohusishwa na ufisadi likijitangazia ushindi ndani ya chama hicho.


  Hii inatokana na CCM kushindwa kutekeleza azma yake ya kufukuza wanasiasa wenye tuhuma za ufisadi, maarufu kama "kujivua gamba," huku kundi la wanasiasa wanaopinga ufisadi ndani ya chama, maarufu kama "Wapambanaji," wakionekana kuishiwa nguvu
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  SIASA ZA KANDA


  Zimeibuka siasa ndani ya CCM za kudai kuwa sasa ni zamu ya kanda fulani kutoa Rais wa Tanzania. Kanda kuu zinazopingana ni Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kusini, Kanda ya Magharibi na Kanda ya mikoa ya kati.

  [FONT=&quot]"Kanda ya ziwa inajumuisha mikoa yenye nguvu kubwa kisiasa kama Mwanza, Shinyanga, Tabora, Mara na Kagera. Kuna baadhi ya watu wameshaanza kudai eti ni zamu yao kutoa Rais kwani licha ya mikoa hiyo, ukiondoa Mkoa wa Mara kuwa na idadi kubwa ya watu, hawajawahi kutoa Rais tangu tupate uhuru miaka 50 iliyopita," [/FONT]
   
 3. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  SUMU YA DINI


  Kundi lingine ndani ya CCM linasema kuwa Rais ajaye lazima awe Mkristo kwa madai kuwa eti kuna utaratibu usio rasmi wa kupokezana Rais kati ya Waislamu na Wakristo.

  Kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete ni Muislamu, basi wengine wanataka Rais ajaye lazima awe Mkristo na kusema hawako tayari kwa Rais Muislamu mwingine.


  Hata hivyo, kwenye kundi la kudai Rais Mkristo kwenyewe kuna mgawanyiko huku Walutheri na Waanglikana nao wakidai sasa ni zamu yao kwani marais waliopita Wakristo walitoka dhehebu la Katoliki.
   
 4. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  NAFASI YA MWANAMKE


  Kundi jingine ndani ya CCM ni lile linalodai kuwa sasa ni zamu ya mwanamke kuwa Rais kwa kutumia mfano wa Rais wa Liberia, Ellen Sirleaf.

  "Unajua, ujanja ule ule uliotumiwa kumwengua Samuel Sitta kama Spika wa Bunge unaweza kutumika kuwaengua wagombea wengine na kupitisha mgombea wa kike pia," alisema mwana CCM mmoja.

  "Tayari wapo baadhi ya wanasiasa wanawake ndani ya CCM wanatajwatajwa kuwa wanaweza kuwa Rais 2015."


  [FONT=&quot]Hapa wanatajwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, na Spika wa Bunge, Anne Makinda, kama wanawake wanaoweza kugombea Urais [/FONT]
   
 5. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  SASA ZAMU YA ZANZIBAR

  Hakuna mahali popote ambapo imeandikwa kwenye katiba au kanuni za CCM kuwa Urais ni wa kupokezana kati ya Bara na Zanzibar, hasa ikizingatiwa kuwa kwa mfumo wa muungano uliopo, mtu wa kutoka Tanzania Bara kamwe hawezi kwenda kuwa Rais wa Zanzibar.

  Hata hivyo, wanasiasa wengi wa Zanzibar wanadai kuwa sasa ni zamu yao kutoa Rais ajaye kwa kuwa marais wawili mfululizo wa CCM wametoka Bara, yaani Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.

  Wana CCM wengi kutoka Zanzibar wameapa kuwa watasimama kidete kwenye vikao vya chama kutetea hoja yao.

  Wazanzibari wanaotajwa kumrithi Kikwete kama Rais ni pamoja na Waziri wa Ulinzi, Dk. Hussein Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Billal, Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Rais wa sasa wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein. Uchunguzi unaonesha kuwa Shein ndiye anayepewa nafasi kubwa zaidi ya kuwa rais ajaye.
   
Loading...