security guard
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 799
- 603
"Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya mlipuko wa bomu kwenye kanisa mjini Arusha,pia kinatoa pole kwa wafiwa na majeruhi,pia kina LAANI vikali wale walio husika na tukio hilo na kinalitaka jeshi la Polisi lichukue hatua kali kwa wote wanaohusika"_A.Kinana(Katibu Mkuu-CCM)
ni bora wangeliacha tamko ra Mwenyekiti likasimama juu ya haya yote maana huyu aliyetoa hili tayari amekuwa gumzo bungeni na mtaani kwa juma lote lililopita, na naona wachangiaji hapa tayari wana hasira na mjadala wa juma lililopita!Hivi KULAANI VIKALI ndo kufanyaje? Hiki si ndicho chama dola? Mnafikiri kuja na matamko ya kulaani vikali pekee bila kuchukua hatua stahiki mlizoambiwa na viongozi wa dini, inatosha? Mwenyekiti wenu alishaambiwa kuwa mambo haya hayajaanza bila maandalizi, hadi akapewa ushahidi wa CD na DVD zikionyesha waislamu kupitia Sheikh Ilunga alivyoamrisha waumini wake kuua Wakristo kote nchini, lakini bado mnacheka cheka tu kama mazuzu na shehe yupo mtaani anapeta tu!
KAMA KUNA MTU BADO ANAKUMBUKA OMAR MAHITA NA 'TOROLI YA VISU VYENYE TOMATO SAUCE', KILE KINACHOITWA 'UGAIDI' JIJINI ARUSHA UNA MALENGO YA KISIASA KUGAWA JIJI HILO KIDINI KUNAKOELEKEA UCHAGUZI WA MADIWA. WaTanzania wala tusipumbazwe kama mazezeta hivi; hakuna cha(1) Sheikh Ilunga, (2) Al-Shabaab, (3) Al-Qaeda wala nani anayewadhuru wananchi kwa malengo ya kuleta hofu na hali ya kutokuaminiana kati ya Wakristo kwa Waislamu nchini. Kwa kufuatilia matukio ya 'Ugaidi wa Kuchonga' na matukio ya hivi karibuni jijini Arusha lazima ujiulize kwamba kati ya watajwa watatu hapo juu na (4) Serikali ya CCM, ni yupi kati ya wote mwenye kuweza KUNUFAIKA kisiasa na ulipuaji ovyo wa mabomu A-Tauni??????? Na kwa mtindo huo ndio maana kati ya michango yote juu ya tukio hili la kusikitisha sana, hakika nimeweza kumtambua mwenzetu huyu, Mkuu Lyamunda, kuwa kweli ni great thinker mwenye uwezo mkubwa kuona ujumbe ilioko nyuma ya ujumbe unaoonekana wazi kwa kila mtu. Ni masikitiko yalioje kuona jinsi gani serikali ya CCM inavyotumia dhana ya 'Ugaidi' kwa maslahi kisiasa kwa mtindo ambao sio kabisa. Wakristo kwa Waislamu kote nchini, tafadhalini kaeni mbali sana na hizi mbinu chafu za CCM na serikali yake kutumia hizi mbinu za ki-Nazi kutafuta kutugawa kwa misingi ya kidini kwa kutumia silaha yao mpya ya 'Ugaidi unaosimamiwa na vijana wake'.
Nilitegemea zaidi ya hapa, nilitegemea CCM ishauli polisi wakafanye upekuzi kule kwenye jimbo lililopewa mamlaka ya kujitawala Loliondo chini ya UAE wanaweza kuwa ndio waliotoa msaada wa bomu!."Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya mlipuko wa bomu kwenye kanisa mjini Arusha,pia kinatoa pole kwa wafiwa na majeruhi,pia kina LAANI vikali wale walio husika na tukio hilo na kinalitaka jeshi la Polisi lichukue hatua kali kwa wote wanaohusika"_A.Kinana(Katibu Mkuu-CCM)
ASIFU WA LUKOSINa sisi watanzania tulaani UJANGILI WA KINANA dhidi ya Tembo....
View attachment 92664
Kinana Strikes Again