CCM yakataa ombi la Spika Sitta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yakataa ombi la Spika Sitta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Sep 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimenawa mikono kuhusu ombi la mgombea ubunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta la kutaka mdahalo na mgombea urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kikisema hakihusiki na mgogoro baina ya wanasiasa hao.Hayo yametokea wakati mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete akizomewa na kikundi cha watu wanaosadikiwa ni wafuasi wa Chadema wakati akihutubia wilayani Mbulu.
  Sitta, ambaye ni spika wa Bunge linalomaliza muda wake, aliiambia Mwananchi katikati ya wiki kuwa yuko tayari kufanya mdahalo na Dk Slaa kuhusu ukweli juu ya uwezekano wa kutoa elimu bure kama Chadema inavyojinadi kwenye kampeni zake.

  Alitoa ombi hilo wakati CCM ikiwa imeshawaandikia wagombea wake wa ubunge na udiwani ikiwakataza kushiriki kwenye midahalo inayoendeshwa na kituo cha televisheni cha TBC1 hadi kwa maelekezo maalum.

  Ombi la Sitta, ambaye alidai kuwa Dk Slaa ni saizi yake, lilionekana akama ahueni kwa chama hicho baada ya Chadema na CUF kutaka mdahalo wa wagombea urais wa vyama hivyo pamoja na CCM.

  Lakini katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ambaye aliandika waraka huo wa kuzuia wagombea CCM kushiriki kwenye midahalo, alisema jana kuwa mvutano kati ya Dk Slaa na Sitta ni ni wao binafsi na si wa chama.
  "Sitta na Dk Slaa wana mambo yao wenyewe. Dk Slaa alimrushia Sitta tope, yeye akajipangusa akamrudishia," alisema Makamba.
  Aliuelezea mgogoro huo hauihusu CCM kama chama na hata wakiamua kufanya mdahalo, hautaingiliana na mpango mkakati wao wa kukataza wagombea wao kushiriki midahalo na wapinzani.

  Makamba alifafanua kuwa CCM imekataa midahalo kwa sababu hukusanya watu hovyo na hakuna mkakati maalumu ya kuiendesha kwa kujieleza na kukosoana kulingana na sera za vyama.

  Alisema CCM haiogopi midahalo bali isingependa kuona inashiriki kwenye midahalo kwa sababu zinaweza kuibuliwa hoja zisizo na msingi kwa makusudi kukichafua chama hicho tawala.

  "Tunataka mdahalo uwe wa sera. Sio unakusanya watu Kariakoo halafu anajitokeza miongoni ambaye jana alilala njaa halafu anasema jana CCM Ilitulaza njaa," alisema.

  Sitta alieleza kushangazwa na ahadi ya Chadema kuwa itatoa elimu bure, akisema suala hilo haliwezekani na kwamba hakuna serikali inayoweza kuendeshwa bila ya kodi.

  Kauli yake ilimfanya Dk Slaa kumjibu vikali akieleza kuwa kama serikali itaweza kudhibiti ufisadi na kukusanya kodi, elimu bure inawezekana na kwamba ndio maana Sitta na Kikwete walisoma bure.

  Dk Slaa alidai kuwa katika uongozi wake, Spika Sitta alizima kashfa nzito za ufisadi, likiwemo sakata lililotikisa nchi la zabuni ya ufuaji wa umeme wa dharura iliyokwenda mikononi mwa kampuni ya Richmond Development LLC, wizi wa fedha kwenye akaunti ya EPA, ufisadi wa kampuni za Deep Green Finance na Meremeta.

  Wakati huohuo, Makamba alisema jana kwamba CCM haitang'oa hovyohovyo mabango ya kumnadi mgombea wao wa urais ili kutekeleza agizo lililotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) baada ya kuonekana yanakiuka kanuni za uchaguzi.
  Badala yake, Makamba alisema kwamba wanatoa mabango maeneo yale tu ambayo Nec itasema kuwa kuna bango lenye tatizo.

  Alitaja baadhi ya mabango ambayo tayari wameyang'oa kuwa ni pamoja na ambayo Rais Kikwete alikuwa amepiga picha na maaskofu.

  Nec Ilikuwa Imetangaza kwamba mabango yote ambayo yanaonyesha mgombea huyo wa CCM akiwa Ikulu, ni kinyume na taratibu na yanapaswa kung'olewa mara moja.
  Katika hatua nyingine, aliyekuwa mwenyekiti wa chama kilichokufa cha CCJ, Richard Kiyabo amejiunga na CCM.
  Kiyabo alitangaza uamuzi huo jana mbele ya Makamba akisema ameachana na upinzani kwa sababu siyo makini bali unaeneza propaganda.

  Kutoka Mbulu, habari zinasema kuwa wakati Kikwete akihutubia mkutano wake wa mwisho mjini Mbulu, kikundi hicho cha watu kilichokuwa upande wa pili wa uwanja kilikuwa kikipiga miluzi na kuzomea, ambayo ilionekana kuudhi wafuasi wa CCM.

  Kutokana na kucheleewa kufika Mbulu, Kikwete alihutubia kwa dakika chache na baadaye kumtambulisha mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Phillip Marmo na baadaye kumaliza mkutano huo.
  Kutoka Monduli, katika hali isiyokuwa ya kawaida waandishi wa habari waliopo kwenye msafara wa mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete jana walizuiwa kuripoti habari za mgombea huyo kwenye Jimbo la Monduli ambalo linawaniwa na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

  Ratiba ya jana ya mgombea huyo ambaye yupo katika ziara mkoani Arusha ilionyesha kuwa angenza mkutano wake wa kwanza Namanga na baadaye Ngaramtoni, Monduli, Mto wa Mbu na kumalizia Mbulu.

  Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka mkoani humo zilieleza kuwa asubuhi ya jana waandishi hao waligawanywa katika makundi mawili; baadhi wakianzia Longido na wengine Namanga.

  Taarifa hizo zilieleza kuwa mara baada ya mkutano wa Longido kumalizika waandishi hao walielezwa kuwa waende moja kwa moja Mbulu na wale walioelezwa kuwa wangeanzia Namanga na kisha kwenda Monduli wakielezwa kuwa hawatakiwi kuhudhulia mkutano wa Monduli na badala yake waende moja kwa moja Mbulu.

  Taarifa hizo zilieleza kuwa waandishi maalum walichaguliwa kuripoti mkutano huo ili baadaye wawape wenzao taarifa za mkutano huo.
  Mjini Monduli, Lowassa alisema hakuna serikali iliyofanya maendeleo makubwa katika awamu zote zaidi ya serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Kikwete.
  Lowassa alisema serikali hiyo imetekeleza Ilani yake katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na kilimo, afya, elimu na mioundombinu.

  Lowassa ambaye ni mgombea wa ubunge wa jimbo hilo, ambaye alipewa nafasi ya kwanza ya kuongea mara baada ya Kikwete kutua Monduli na helkopta, alisema katika jimbo lake la Monduli serikali imetekeleza ilani kwa asilimia 99.
  Mgombea huyo alisema serikali imeondoa tatizo la maji kwa kutumia mradi uliogharimiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kujenga sekondari kila kata na sasa ipo katika hatua ya mwisho ya ujenzi ya sekondari tatu za kidato cha tano.

  Naye Kikwete aliuambia mkutano huo kuwa wakazi hawana budi kummchagua Lowassa kwani anawapenda.
  "Nyie mnajua Lowassa anawapenda naomba muendelee kumchagua kuwa mbunge wenu ili muendelee kupata maendeleo," alisema Kikwete.

  Katika mkutano huo, Rais Kikwete aliahidi Serikali yake kulipa kifuta machozi kwa wafugaji ambao waliathirika na ukame mwaka jana.

  "Tumesikia kilio chenu na ingawa hatuwezi kulipa fidia ya ng'ombe kama ng'ombe 200 wa Mzee Loiboki ambao walikufa kwa ukame, tutajitahidi walau kidogo ili kuwafuta machozi," alisema Kikwete.
  Viswani Zanzibar, wakati CCM inazindua rasmi kampeni zake kwenye Viwanja vya Demokrasia mjini Unguja, bado meneja wake hajawekwa bayana.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi kuu ya CCM Kisiwandui, katibu wa kamati maalumu ya Nec –Itikadi na Uenezi, Vuai Ali Vuai alisema watamtangaza meneja kampeni katika uzinduzi wa kampeni hizo leo.
  “Meneja wa kampeni atatangazwa baadaye, uzinduzi bado uzinduzi utafanyika kesho (leo) msiwe na haraka sisi tumekuja kutangaza uzinduzi wa kampeni zetu hayo mambo mengine yatajulikana huko kwenye kampeni,” alisema Vuai.

  Wakati akisema hayo, imebainika kuwa mabango ya kumnadi mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Ali Mohammed Shein yamebainika kuwa na kasoro.

  Kwenye bango lililobandikwa eneo la darajani lililo Manispaa ya Zanzibar, kuna picha ya sura ya Dk Shein, lakini maandishi yanasomeka chagua CCM, chagua Kikwete.
  Lakini Vuai alisema hana taarifa hizo na wala hajaona picha hizo, lakini akasema huenda ni bahati mbaya katika uchapishaji.

  “Mimi sijaziona hizo picha inawezekana ikawa ni bahati mbaya kwa kuwa walioandika nao ni binaadamu, lakini nasema kuwa tuna mabango aina mbili aina moja mabango yanayomnadi mgombea wetu Kikwete na yanayomnadi Dk Shein na tulikuwa tuna matayarisho na uzinduzi, lakini hatujazindua na hayo mlioyaona ni bahati mbaya tu.'
  Alisema yamebandikwa kutokana na hamu ya wafuasi lakini kesho nakuhakikishieni mtajua kuwa leo ni siku ya uzinduzi wa CCM,” aliahidi Vuai.

  Habari hii imeandikwa na Leon Bahati, Salma Said, Zanzibar, Boniface Meena, Karatu na Mussa Jumma, Monduli.

  chanzo: CCM yakataa ombi la Spika Sitta
   
 2. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Dr slaa kufanya mdahalo na samuel sitta ni kujishusha hadhi ...na itakuwa aibu kubwa kwa chadema.

  anatakiwa afanya mdahalo na kikwete,au lipumba ama wagombea wote wa ngazi ya u presida sio wagombea ubunge..!
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sitta akafanye mdahalo na mtu wa hadhi yake kama Halima Mdee, Zitto Kabwe, nk! Otherwise atuambie kwa nini aliweka kapuni issue za Deep Green Finance, Meremeta, etc? Kwa manufaa ya nani?
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  CCM hawataki mdahalo kwa kuwa wanajua kitakachowapata baada ya huo mdahahlo!!!

  Makamba anajua...
   
Loading...