CCM yakanusha tuhuma za CHADEMA

Nape afadhali umekanusha Kaka ! Sasa naomba nikuulize swali la kizushi , Hivi ni kweli kwamba ulipanga kuzunguka na Juliana nchi nzima ? Kwa nini usizunguke na Mbabe wako Lowasa ? Mbona huyo ni maarufu sana kuliko Juliana ! Si umeona juzi ubwabwa wake ulivyopata wafuasi wengi !
 

hii ilitakiwa kuwa topic ya kujitegemea
 
Kwani nani alitegemea akubali kwamba wanashirikiana kuhujumu. You dont need to use your resources to deny facts meeen!!! Kuna mengine mengi tu ya kutolea maelezo. Kesho utamsikia Mwigulu naye anajibu!!! CC-M-ajamabazi bwana!!!
 
Ngoma ikivuma,ikavuma,ikavuma tena,vuvuu,vuvuu mwisho upasuka R.I.P CDM

Toka Burton sat shop.


Ndugu yangu siasa ni sayansi na si ushabiki tu wa kipropaganda.Hata mpira wa miguu ni sayansi pia wala si ushabiki tu , inahitaji utekelezwaji wake kuwa madhubuti.Hakuna chama kilichojipanga kimkakati kama CDM na ndo maana kinapendwa.Jiulize miaka kama kumi CDM ilikuwa na wabunge wanne leo ina wabunge 49.Huo ni mkakati mkubwa wa kupongezwa.Jamii pia inazidi kuiunga , angalia mikutano yake na maandamano utaona jinsi jamii inavyoiunga mkono CDM.mfano mzuri uchaguzi arumeru mashariki , NASARI ni kijana mdogo sana, alishinda kwa nguvu ya umma kumuunga mkono , hivyo kusema CDM itakufa hizo ni posho za nape.Nakukumbusha kikao tendaji cha BAVICHA kimewafukuza uanachama akina SHONZA kukiwa na ushahidi tosha , kiasi kwamba waliotajwa kama s.wasira na shibuda wametajwa.Si hao tu hata ccm imetajwa.CDM huwa haikurupuki , jifunze nawewe kutokurupuka CDM haiwezi kufa kwa mikakati isiyo na tija.NAPE kukanusha ni blabla anajua ukweli.
 
UMENIFURAHISHA, KWELI IVO NDO VITUKO VYA NEPI VUVUZELa

Ni kupoteza muda kuwasikiliza propagandist kama nape. Unaweza kuendelea kukisikiliza chama ambacho kimeua miiko ya uongozi na kuleta umasikini kwa watz. Jambo muhimu ccm na viongozi wake kutambua ni kwamba hata cdm ikifa leo haimaanishi ndio ccm kupendwa na wananchi....! Watz makini na wazalendo hawawezi kuwaambiwa porojo na uzushi wa ccm wakakupa nafasi ya kukusikiliza. Ni watz wale tu wanaofaidi ufisadi na hujuma zinazofanyika dhidi ya raslimali za nchi wanaounga mkono ulaghai wa ccm kwa raia wake masikini hasa kule vijijini pale chaguzi zinapokaribia.
 
hapo mwanangu umesema kweli nakuunga mkono, uzushi utakaofuata wa wanamagamba ni kutangaza kwamba Chadema ni chama cha Wakristu ili kuwaadaa waislamu,au watasema kwamba ni chama cha wachaga.
 
hapo mwanangu umesema kweli nakuunga mkono, uzushi utakaofuata wa wanamagamba ni kutangaza kwamba Chadema ni chama cha Wakristu ili kuwaadaa waislamu,au watasema kwamba ni chama cha wachaga.

JAMAN TNAHITAJI KUJIAMIN, KWA SASA CHADEMA IS V STRONG, CCM WANAUMWA KWA NGUVU HII, WAFUATILIE KILA MWANACCM ANAHOMA INAYOITWA CHADEMA, KOKOTE WAWAPO CHADEMA NDO NENO LAO MDA WOTE, NA HAKUNA PIGO KUBWA TMEWAPA CCM KM KUWATIMUA AWA MASALIA WASALITI, NI USHUJAA WA AJABU UMEFANYWA NA BAVICHA, TUWAUNGE MKONO KWA MAAMUZ AYA, KWANI NAAMINI NAPE, WASIRA, MCHEMBA NA WENZAKE WALIWEKEZA PESA NYINGI KWA AWA WASALITI NA SASA WAMENG'OLEWa, RIL TMEWAPA PIGO KUBWA, WAT WE NEED NI MSHIKAMANO NA IMANI KWA VIONGOZ WETU, VIVA CHADEMA VIVA M4C
 
 
Mi naona ni kweli mchwawi wa CDM yuko CDM. masalia na PM7 wapo ndani ya CDM na siyo CCM.Kamati kuu ifanye maamuzi mazito dhidi ya uasi ndani ya chama.
 

Anasahau kwamba baadhi ya viongozi wa serkali ,ambao ni wana-CCM wamesikika mara kadhaa wakitangaza hadharani kuwa CDM itasambaratishwa kabla ya 2015 (WASSIRA).
Huo ni mkakati wao na hawawezi kamwe kukiri hilo.
 

ukweli umeuficha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
ATI BETLEHEM, FISADI, MWIZI PIA JAMBAZI MKUBWA WEWe
thibitisha kauli yako kwa ushahidi madhubuti.ukithibitisha nitakubaliana na wewe usipothibitisha ntakushauri uache fitna na ushabiki kwenye mambo ya msingi kwani fitna ni dhambi miongoni mwa madhambi mazito.
 
Ukweli, mimi nitashangaa sana kuona hapa jamvini watu wanamlaumu NAPE, WASIRA na huyo MGUU WA CHEMBA, hvi tunategemea wao wafanye nini? Siasa ni ushindani ingawa theorically ni ushindani wa hoja lakini kwenye grass root si hivyo bali ni ushindani wenye mbinu chafu tena wakati mwingine za kutisha sana. Ili kuweza kuongoza nchi ni lazima uwe na mifumo wenye nguvu na weledi, mfumo wa chama chetu cha CDM wa kuchukua wanachama hovyo hovyo kwa kudhani kuwa wingi wa wanachama ndio wingi wa kura ni UPUUZI unaokigharimu chama. Ni lazima CDM itengeneze mifumo yake ya kuendesha chama na kwa hali ilivyo sasa kwani mfumo wa CDM na vyama vyetu vingine ni 95% unafanana na CCM hivyo ni lahisi sana CCM kuwasambatisha kwa sababu wao wana uzoefu wa mfumo huo kwa zaidi ya miaka 50 lakini CDM hata miaka ishirini tu bado. Huwezi anzisha TIMU ukaiga mfumo wa uchezaji wa mwenzako mwenye uzoefu, wachezaji wenye vipaji, rasilimali, marefa, uwanja na uzoefu alafu eti utegemee USHINDI. Hiki ndicho kipindi cha kuangalia uwezo wa viongozi wetu, hatuwezi kupima uwezo wa viongozi kwa kuangalia uwezo wa kusema jukwaani tu, HAPANA ni pamoja na uwezo wa kuplan, kutengeneza mifumo bora ya uendeshaji wa chama kwa ujumla na jinsi ya kupambana na changamoto. Binafsi nachukia sana huu mfumo wa kila kitu kusubiri sijui kamati kuu ikae mara sijui kikao gani? HAPANA ni lazima mfumo uwape FURSA ya kutosha viongozi wetu watendaji kufanya kazi na vikao vya juu vibaki na kazi ya kubariki implementation tu. Haya mambo ya kamati kuu kuwa kama direct implementer ni mambo ya CCM. Ni lazima tufanye tathmini yamifumo yetu ya uendeshaji wa chama, tuangalie kanuni zetu vizuri na kuzitengeneza vizuri ziweze kuwabana wasaliti, Haiwezekani leo eti makam mwenyekiti wa BAVICHA anamkashifu kwa maandishi katibu mkuu wa chama tena hadharani pasipo kujificha eti unafanya uchunguzi wa tuhuma na kupeleka maazimio kwenye kikao na kuwapa fursa wajumbe ndio waamue adhabu tena kwa kupiga kura HUU ni utaratibu Mbovu sana na unatoa fursa kubwa ya RUSHWA, UONEVU na MAKUNDI ndani ya chama, kwa kesi kama hii kanuni tu zinapaswa kumuondoa then yeye ndie akakate rufaa huko kwenye vikao vya juu wakati akiwa pembeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…