Kazi kweli kweli!
Mi naamini hivi (kutoka katika historia ya Seif Sharrif Hamad) Maalim Seif haupingi muungano kwasababu anawapenda sana Wazanzibar, la hasha, huyu jamaa ana hamu na kiu kubwa sana ya kuitwa rais, asingependa afe bila kukali kile kiti pale Ikulu, kikwazo kwake ni hiki, Muungano, mara zote anahisi ameshinda uchaguzi (kwa hili hata mimi nakubali, hasa uchaguzi wa mwaka 1995, hadi DTV walitangaza hilo), serikali ya muungano ikiwatumia polisi wamekua wanatangaza matokeo tofauti, anaamini kua, nje ya muungano, hakuna polisi wa Kizenji mwenye uwezo wa kutangaza matokeo tofauti.
Kwa wasio jua, huyu ndio sababu ya Mzee Aboud Jumbe Mwinyi kunyang'anywa urais wa Zanzibar 1984 yeye ndiye inasemekana aliiba zile Nyaraka na kumpelekea Mwl, fumba na kufumbua, Mzee Jumbe wakiwa Dodoma anashangaa mwenyekiti wa chama, mzee Mchonga anakila kitu mkononi, hapa alilenga uchaguzi wa mwaka 1985, deal lilipo shindikana nae akachafua hali ya hewa, serikali ya wakati huo, i think rais alikua Mzee ruksa but mwenyekiti wa CCM bado alikua mzee Mchonga and remember, chama kilikua ndio kimeshika HATAMU za uongozi, nachosema hapa ni kua, kuwekwa kwake ndani kulikua na mkono mrefu sana wa mzee Mchonga.
Mwenye historia tofauri please!