Katika majimbo ambayo CCM hawaamini macho yao basi Iringa mjini limo. jimbo hili kumbukumbu zinaonyesha kuwa ilikuwa ngome ya CCM mwaka 2005, kwani Iringa ndo iliongoza kumpigia kura JK kwa nchi nzima. sasa mambo yamebadilika kwa CCM , wanaIringa wamewaambia wazi hawaitaki ccm toka alipokuja BILAL hadi JK mwenyewe. wana JF kinachoendelea sasa ni kituko, kama kawaida kwenye uzia wanapenyeza rupia ili wakubalike. sasa madereva wa dala dala vijana wa stendi wanavaa t shirt kwa kulipwa tshs 5000. kesho tetesi zinasema slaa anakuja, kwa tetesi hizo CCM wameshinda wakigawa kofia t shirt na vitambaa vyao. kali kuliko yote ni hawa madereva wa teksi na hiace, ccm waliwapa hela ili wapeperushe bendere zao lakini baada ya mda wakaona bendera za CHADEMA ndo zinapepea, kweli viongozi wa hapa wamechanganyikiwa. naomba pia ikumbukwe kuwa walianza kumleta malecela aje kumsaidia mama mbega lakini wapi, akaja lukuvi lakini wapi? sasa wanajidanganya kwa t shirt ambazo watu wamevaa.
Hali ya mawakala wa chadema nimeipenda mno, kuna wakala mmja tulikuwa naye dar jumapili iliyopita akapigiwa simu kuwa anatakiwa akalinde maslahi ya watanzania kwa kweli aliacha kila kitu kisha akaniambia YUKO TIYARI KUJITOLEA KWA KAZI HIYO BILA HATA MALIPO KULIKO KURA ZA WATANZAIA KUUBIWA. HAWA MAWAKALA WENGI NAWAFAHAMU SIFIKIRII KAMA WATADANGANYIKA.