Huyu mama aliyebeba bango la Ufisadi, Hakya Mungu anaitukana CCM kwa staili ya rejareja
CCM kazi mnayo
Chama tawala na maandamano ya nini huu ni wakati wa kushughulikia matatizo ya wananchi na kutekeleza ahadi badala ya kuandamana.
Kumbe na Sumbawanga kuna lami.!!! Any way nawashukuru CCM kwa kuanza kuicheza ngoma ya CHADEMA vizuri, na hii ndo hakuna kurudi nyuma mpaka tutakapowatoa ikuru latest 2015.
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa uchumi na fedha Mwigulu Nchemba wameongoza maandamano leo kutoka ofisi ya CCM wilaya ya Mpanda kwenda kwenye Uwanja wa Shaulili ambapo wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya watu. Hakika wana Mpanda wameikubali sana CCM.
Kweli kaka wewe umenena naona wanaichi wa kawaida hawana hata mguso wa mfisadi sasa kinachoonekana hawa si watu wa mpanda pekee, ni watu walioletwa kutoka maeneo mbalimbali kuja kuokoa jahazi tena ni wanamagamba haohao. mini naona lile lorry ndilo lililowaleta.Mbona wote wamevaa Kijani kuonyesha wamejipanga? Kwa wale mnaojua kusoma picha mtagundua kwamba pembeni kuna watu wanaoendelea na shughuli zao kuonyesha ni mafisadi wachache tu waliovalia nguo za kijani . CDM ikiwa na maandamano hadi maduka huwa yanafungwa including wauza magenge na huoni mtu anayeendelea na shughuli nyingine pembeni mwa barabara kama ilivyo hapa.
Nape Karibu sana Arusha na Moshi tuna hamu na wewe**********!!!!!!!!!!!!!!!!!
Wanapaswa kuhurumiwa hawa wala si kuwalaumu maana hii siyo hali ya mtu mwenye akili na uwezo wa kuamua mambo yake mwenyewe, wanaburuzwa.Mbona wote wamenuna, au hawajapewa sitting allowance???
Kweli kaka wewe umenena naona wanaichi wa kawaida hawana hata mguso wa mfisadi sasa kinachoonekana hawa si watu wa mpanda pekee, ni watu walioletwa kutoka maeneo mbalimbali kuja kuokoa jahazi tena ni wanamagamba haohao. mini naona lile lorry ndilo lililowaleta.
Kama kufunika ndio hivi basi wale chadema huwa wanalipua wala hawafuniki!!! watu 155 hawa ndio funika!!!