CCM yafuata nyayo za CHADEMA, CUF


Unajua unapojitaja kama unamtegemea Mungu uwe serious katika kumtegemea otherwise ni kujiletea laana tu. Movement 4 Change kwa kiswahili tunasemaje?naona CDM ndio leading party nw kwann wengine wawe na kauli mbiu za ku-copy?
 
alieleta hii habari ameichakachua mno.gazeti ht mi nnalo halijaandika ivo.

Unamawenge nn?,hyo habari nimecopy na sijaedit. Teh teh teh teh! Umefakamia sikukuu.
 

alieleta hii habari ameichakachua mno.gazeti ht mi nnalo halijaandika ivo.
 
*YAWATAKA WATANZANIA HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA
*YAWATAKA KUWA NA KIASI KATIKA SHAMRASHAMRA
* ASEMA USHINDI WA LEMA, NI ISHARA YA UTAWALA BORA WA SERIKALI YA CCM



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, baada ya kuutumia mwaka 2012 kupanga safu ya uongozi katika chaguzi za ngazi zote zilizomalizika hivi karibuni, mwaka ujao wa 2013 utakuwa wa kuchapa zaidi. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba (pichani) alisema, kazi itakayofanywa na CCM katika mwaka huo, ni pamoja na kukagua upya utekelezaji wa ilani ya CCM na kuhakikisha zile ambazo hazikamilika zinamalizwa.
"Mwaka huu wa 2012 unaomalizika tuliutumia zaidi kujipanga katika uchaguzi wa ngazi zote ili kupata safu nzuri itakayoisimamia serikali kutekeleza ilani ya CCM, sasa mwaka mpya wa 2013 utakuwa wa kazi zaidi za kusimamia serikali ili kuhakikisha mwaka 2015 mpiganaji wa CCM tutakayemteua kugombea urais anapita kiulaini", alisema Mwigulu.
Akizungumzia tukio la Mbunge wa Arusha Godless Lema kushinda rufani yake dhidi ya hukumu iliyomvua ubunge Aprili mwaka huu, Mwigulu alisema, ushindi huo ni ushahidi kwamba serikali ya CCM inaongoza kwa misingi ya utawala bora ambapo kila anayestahili haki anapata.
"Ushindi huu wa Lema, siyo kwamba anaakili sana au chama chake kina maarifa sana yaliyosababisha ushindi, ila ni kutokana na serikali ya CCM iliyopo madarakani kuheshimu na kujali haki na kwa kweli natumia fursa hii kuipongeza Serikali kwa kuthamini na kusimamia haki wakati wote.. Ninyi si mnajua katika nchi zisizo na utawala bora jinsi ambavyo mambo huwa kwenye kesi kama hizi. lakini hapa Tanzania ni tofauti kabisa", alisema, Mwigulu.
Aliwashangaa Chadema akisema, "Hawa ni watu wa aina yao, waliposhindwa katika kesi Arusha walisema Ikulu imeingilia na majaji hawajui kiingereza.. sasa leo wameshinda wanafurahi na kuona kwamba sasa majaji wanajua kiingereza na hawakuigusa Ikulu kwamba imeingilia, maana pale ilipotolewa hukumu umbali wake ni hatua chache na Ofisi ya Ikulu kuliko Arusha".
Mwigulu alitumia fursa hiyo kuwatakia heri Watanzania kwa sikukuu za Krismas na mwaka mpya na kuwataka kuzitumia sikukuu hizo kwa makini na kwa kiasi ili zisiwe chanzo cha matatizo kwao badala ya furaha.
"Chama Cha Mapinduzi kinawatakieni sikukuu njema za Krismas na mwaka mpya, lakini tunawaomba msherehekee kwa kiasi huku mkichunga usalama wenu na mali zetu", alisema Mwigulu.
 
Huyu si ndio alishindwa mambo ya uchumi akawekwa Mama Zakia? Sasa hapa anaota ndoto
 
Mbona anaumauma maneno ? Wananchi wangapi hawana uwezo wa kukata rufaa kama giant lema na wamedhurumiwa haki zao ? Utawala bora wa ccmizi hadi ukate rufaa ? Wewe zoba kweli, hiloooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo.
 
Ni kweli mwaka 2012 ccm ilitumia muda mwingi kusamehe kodi,kupambana na kina Dr.Ulimboka,Kutumia jeshi la polisi kuzima upinzani (kwa mujibu wa cnn,september,2012),kuwashitaki walimu (hatimaye tunaona shule zilizokosa wanafunzi wa kidato cha tatu huku darasa la saba wakifanyiwa standardization) ,Tumeshuhudia baraza la mawaziri likivunjwa kutokana na uwezo mdogo wa kiutendaji wa mawaziri wa ccm ikiwa ni pamoja na tuhuma za rushwa,tumeshuhudia ccm ikigawa mahindi kwenye uchaguzi wa Igunga huku viongozi wake (Aden Rage) akionesha bunduki ili kuwatishia wananchi wanaounga mkono upinzani kitu ambacho kilifanya mahakama itengue ubunge wa kada wao Dr.Kafumu, Pia tumeshuhudia ccm ikilazimisha Uranium ichimbwe wakati wananchi wanauelewa mdogo huku wakiwa hawajiridhishwa na mapato yatokanayo na madini mengine. Mwaka 2013,ni wa ccm kuchapa kazi ya kugombana na TUCTA waliotangaza nia ya mgogoro endapo mishahara haitaangaliwa upya. N.B:Nchemba amenena lakini,"ada ya mja hunena,muungwana ni vitendo"
 
Huyu jamaa kuna siku nilimsikia akihutubia hadhara kwa kutumia maneno yasiyo na adabu na busara kama mtu mzima. Kuanzia siku hiyo nimemdharau hata kwenye hadhara nikisikia yupo sihudhurii.
 
aiseeeee babayangu nimeiyona hiyo picha ya mwigulu bado kidogo nitapike nyama ya mbusi nilio kula hapa mamsira mkuu rombo
 
Teh teh teeeh teeheh.! Fill in the blank..! Kilaza mara zote yeye ni mtu wa ku-copy na (....)?
 
CCM ni majambazi. Nikisikia neno CCM napata kichefuchefu na kuona kinyaaa. CCM imepoteza uhalali wa kutawala Tanzania. CCM imeshindwa na imefeli kuleta maendeleo kwa watanzania, bali kimefanikiwa kuzalisha mafisadi na kuwatunza. CCM si chama cha watanzania halisi bali ni chama cha wahuni.
 

galatians 6:8..!
 
Ishiiii! wazee wa temeke mpo wapi hamjamtegea ile dawa ya kunatana
 
Usilitaje bure jina la Mungu wako! Kwa wale waliopitia mafunzo ya kipa imara mwaweza kutusaidia ni amri ya ngapi hii?
Aisee hata mimi ndo nilikuwa napost hivyo hivyo. Labda mungu wa Kolelo(mzimu)lakini si huyu ninaemuabudu na kumtukuza Allah Subhana wataalah
 
siasa ni kazi kama kazi zingine,tofauti yake siasa ni uongo unaofanana na ukweli ambao unacheza na akili (saikologia) za watu tu.mara nyingi wanasiasa wetu huwa wanaamini kwamba wao wanaakili sana kuliko watanzannia wote,yaani yanayosema na kuyafanya ni mambo ya ajabu sana kumbe hapa.Tunawafahamu sana acheni ubabaishaji.mpo madarkani kwa sababu ya pesa za walipa kodi na rasilimali za taifa hili,hakuna kiongozi yeyote ataleta maendeleo ktkt nchi akitoa pesa mfukoni mwake.
 
Usalama wa raia na mali zao
Huduma za jamii - afya, shule,
Gharama, Maisha magumu - hela haikamatiki kama ulivyo mfumuko wa bei.

mwaka mzima mko likizo kwa ajili ya uchaguzi......
 
Huyu Mwigulu kwa kuropoka jamani! Angelikuwa kwangu ningempa kazi ya GermanSherpherd manake anaiweza sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…