CCM yachunguza mapokezi ya Mawaziri 'waliotemwa' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yachunguza mapokezi ya Mawaziri 'waliotemwa'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, May 22, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,786
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  [h=2][/h]


  Na Richard Makore  22nd May 2012  [​IMG]
  Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye


  Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinafanya uchunguzi ili kubaini wanachama wao wanaoshiriki kuandaa mapokezi ya kuwapokea majimboni wabunge waliokuwa mawaziri ambao walitemwa kutokana na tuhuma za mbalimbali.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema jana kuwa baada ya kuwabaini wanaweza kusema hatua za kuwachukulia.

  Wabunge hao ambao walikuwa Mawaziri, walitemwa na Rais Kikwete mapema mwezi huu, baada ya kutajwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Hata hivyo, Nape aliliambia NIPASHE kuwa ni vigumu kuwadhibiti watu wanaoandaa mapokezi hayo kumtaka mwandishi awaulize wao wenyewe kwa nini wanafanya hivyo.

  Alipoulizwa kama CCM kinatambua na kubariki mapokezi ya namna hiyo, Nape alijibu kwa kifupi kuwa waulizwe wanaoyaandaa

  “Mimi sijui sababu zinazowafanya wananchi hao kuandaa mapokezi hayo lakini sio wafuasi wa CCM pekee lakini naamini labda hao ni wapiga kura wa mbunge husika,” alisema.

  Alipoulizwa kwa upande wa wafuasi wa CCM wanaohusika kuandaa na kushiriki mapokezi hayo, Nape alijibu kwa kifupi kwamba suala hilo chama kitalifanya kazi na kuchukua hatua.

  Baadhi ya wananchi wanahoji kuwa iweje waziri aliyefukuzwa kazi kutokana na tuhuma kwa mujibu wa ripoti ya CAG, apokelewe jimboni kwake kama shujaa.

  Baadhi ya majimbo ambayo wananchi walionyesha nia ya kuwapokea wabunge wao ni pamoja na Sengerema kwa William Ngeleja na Tanga mjini kwa Omar Nundu.

  Ngeleja alikuwa Waziri wa Nishati na Madini na Nundu alikuwa Waziri wa Uchukuzi.

  Mei 4, mwaka hu Rais Jakaya Kikwete, alilifanyia mabadiliko Baraza la Mawaziri na kuwatema mawaziri baada ya kuguswa na ripoti ya CAG na taarifa za wenyeviti wa kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,742
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  hao mawaziri inajulikana walitolewa kafala sababu mwizi ni mkuu mwenyewe!
   
 3. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,786
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Watanzania umasikini sio uchumi,umaskini wa Watanzania ni akili zao kutumazwa na mambo kama haya, iwaje mtu kaondoka na mamilioni ya fedha za Umma(Taifa) ile anapokewa kutokana na masi alio lifanyia Taifa.

  Ndio Wazungu wakatuona sisi ni mafoolish nchi ina rasilimali nyingi na utajiri mkubwa lakini katika oroza ya nchi maskini watu wake yomba yomba na kusaidiwa hata na Internatiolal charity Tanzania ni muja wapo, Jee hizi rasili mali zilizopo wanafaidika nani ?.

  BORA MUNGU AKUNYIME UTAJIRI KULIKO KUKUNYIMA UJINGA.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,090
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mbona tunaambia CCM ndio wanaendesha chama chao kwa Demokrasia?
   
 5. k

  kuishi tabu New Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waanze kumchunguza jk ndo tutaona wanaakili
   
 6. m

  mmanga mswahili Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii inaoneshanni kuwa ccm kwa kisassai gani wanajali utawala bora na kuchukia ubadhirifu
   
 7. m

  mamajack JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,163
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  mapokezi hayana effect kwa watanzania,kuliko kuchunguza mapokezi,bora wangefanya ambayo yanafaida kwa watanzania,eti oh,wameitwa takukuru,oh,haki za binadamu zisikiukwe.mbona wanaohisiwa ni wezi ambao ni raia hawaangaliwi kwa vigezo hivi? hebu wasituzuge wezi wakibwa hao kuanzia nani mpaka nani wote tupa kuleee,eti wengine wanapongeza kisa takukuru wanawahoji,mwizi aliyekutwa na akiiba anachunguzwa,ili ujue nini?nia yake ya kuiba au?hao wachunguzaji wenyewe wezi watupu.mnatumia fedha za watanzania kuchunguza na kuhoji ukweli unaooneka. dc akiagiza ukamatwe hakuna cha haki za binadamu wala nini.
  kila chenye A kina Z yake.
   
Loading...