CCM ya watanzania, Chadema ya wateule

CCM ya watanzania, Chadema ya wateule

siku zinavyozidi kusonga mbele kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2014, ikiwa ni jaramba la uchaguzi mkuu 2015; chama kisicho na demokrasia kimezidi kupungukiwa wapenzi huku wakiambulia kapa mahakama ya rufaa kuhusiana na majimbo ya ubunge ya igunga na sumbawanga mjini. Hali katika mikoa ya dsm, pwani, mjini magharibi, kaskazini unguja, arusha, kilimanjaro, mwanza, kusini unguja, mtwara, mbeya, iringa, lindi, tanga, ruvuma, morogoro, singida, rukwa, tabora, shinyanga, simiyu,geita, kagera, mara, njombe na makao makuu ya nchi - dodoma ni kushamiri kwa rangi ya kijani iliyo maarufu kwa ccm. Hali imekuwa ngumu katika mikoa hiyo kwa chadema huku wakishuhudiwa uwingi wa wafuasi wao kauchana na chama hichona kurejea ccm kutokana na kuchoshwa na siasa za chadema zilizoegemea kwenye mgawanyiko na upendeleo kutegemea na udini, ukanda, ukabila na ukoo. Yote kwa yote ofisi za chadema zililzokuwapo katika maeneo hayo zimegeuzwa kuwa maskani ya vijana wa ccm walioachana na cdm.
Dalili zipo wazi kuwa cdm haitaweza kushiriki katika uchaguzi wa mwakani katika maeneo makubwa ya mikoa hiyo kwa vile hawajawa na misingi ya kuendeshea siasa katika mikoa husika. Hiyo ni kuashiria ccm itajihakikishia kupata ushindi wa asilimia 85% ya uchaguzi wa serikali za mitaa huku vyama vya upinzani vikigawana asilimia zilizobaki.

Watanzania wapenda amani mlioko nje ya nchi mkae kwa amani, mkijua ccm itazidi kutesa katika anga za siasa za tz .vijana wa cdm ni mahodari kwa kupiga proganda katika mitandao huku wakisahau kuwatembelea wapiga kura mikoani. Kutokana nakukata tamaa, cdm imeamua kuleta vurugu katika mikutano yao ya siasa, bungeni na mabaraza ya halmashauri.

ccm oyee!
nyooooooooo
 
Dah ! Kweli hela ya Lumumba inaliwa kijinga sana ! Yaani we jiandikie ujinga wowote tu , halafu nenda ofisi ndogo , siku imeisha ! Naomba kuuliza swali dogo , Hivi maudhui ya Uzi yana uhusiano wowote na Elimu ya Mwandishi ?
 
Kucomment mada uchovu kama hizi unaweza ishia kupigwa BAN.
 
Wewe ni mvibu wa kuelewa: Kuwa mwerevu ni jimbo lipi mkoani Dodoma lililo chini ya Chadema:

CCM inaongoza Dodoma Mjini, Mtela, Kongwa, Mpwapwa, Bahi, Kondoa nk. Waambie viongozi wako wabadili mikakati ya kisiasa vinginevyo mtaishia kugombana na Ndugai na Makinda bungeni badala ya kueneza chama chenu vijijini

kwa kigezo hicho cha ubunge,inamanisha mikoa yote hiyo uliyoitaja hakuna mbunge wa chadema? Hujitambui wewe,hebu njoo Simiyu ujionee. Kuna wabunge watatu wa majimbo ya Maswa(2) na meatu(1). Usiwe unaropoka tu wakati kila uchaguzi mdogo mnapigwa chali na hasa wa vijiji.
 
Hata anguko la KANU, wanachama wake hawakuwai kuwaza au kufkiria kama ipo cku watabaki kuwa wapinzani ila leo hii tunawaona wameikubali hali na majuto mengi ya kuwapuuza wakenya na kuwabeza, CCM nayo kama KANU sikio la kufa halickii dawa.

Hata Rupia Banda hakuwai kuwaza kabsa kama angeshindwa na Satta.. ni mnafiki pekee anayeweza kupuuza mageuzi yaliyopo na yanayoendelea kila kukicha Tanzania..

Wenye akili CCM wameshaanza ku smell changes na unaweza hata kuona wameacha zile kauli za kipuuzi na kebei ila wendawazimu ambao wanaona chini ya pua zao na vipofu wa kesho ndo hawa wanakuja na thread za namna hii.
Hali ni mbaya watu wamechoka kupuuzwa kila mwenye akili na macho anaona ila mwenye macho akila hakuna ataona ila kung'amua na kuelewa anachoona kamwe hawezi!
 
ccm mnajifariji tu... jipe moyo huo c mbaya bt kumbuka kata za uchaguzi zjazo pamoja na kalenga ya mgimwa zinachukuliwa na cdm
 
Back
Top Bottom