MAFILILI
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 2,377
- 1,200
Siku zinavyozidi kusonga mbele kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2014, ikiwa ni JARAMBA la Uchaguzi Mkuu 2015; chama kisicho na demokrasia kimezidi kupungukiwa wapenzi huku wakiambulia kapa mahakama ya rufaa kuhusiana na majimbo ya ubunge ya Igunga na Sumbawanga Mjini. Hali katika mikoa ya DSM, Pwani, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Kusini Unguja, Mtwara, Mbeya, Iringa, Lindi, Tanga, Ruvuma, Morogoro, Singida, Rukwa, Tabora, Shinyanga, Simiyu,Geita, Kagera, Mara, Njombe na makao makuu ya nchi - Dodoma ni KUSHAMIRI kwa rangi ya kijani iliyo maarufu kwa CCM. Hali imekuwa ngumu katika mikoa hiyo kwa CHADEMA huku wakishuhudiwa uwingi wa wafuasi wao kauchana na chama hichona kurejea CCM kutokana na kuchoshwa na siasa za CHADEMA zilizoegemea kwenye mgawanyiko na upendeleo kutegemea na UDINI, UKANDA, UKABILA na UKOO. Yote kwa yote ofisi za CHADEMA zililzokuwapo katika maeneo hayo zimegeuzwa kuwa maskani ya vijana wa CCM walioachana na CDM.
Dalili zipo wazi kuwa CDM haitaweza kushiriki katika uchaguzi wa mwakani katika maeneo makubwa ya mikoa hiyo kwa vile hawajawa na misingi ya kuendeshea siasa katika mikoa husika. Hiyo ni kuashiria CCM itajihakikishia kupata ushindi wa asilimia 85% ya uchaguzi wa serikali za mitaa huku vyama vya upinzani vikigawana asilimia zilizobaki.
Watanzania wapenda amani mlioko nje ya nchi mkae kwa amani, mkijua CCM itazidi kutesa katika anga za siasa za TZ .Vijana wa CDM ni mahodari kwa kupiga proganda katika mitandao huku wakisahau kuwatembelea wapiga kura mikoani. Kutokana nakukata tamaa, CDM imeamua kuleta vurugu katika mikutano yao ya siasa, bungeni na mabaraza ya halmashauri.
CCM Oyee!