CCM wavamia mkutano wa Dk Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wavamia mkutano wa Dk Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ujengelele, Sep 17, 2010.

 1. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wavamia mkutano wa Dk Slaa Friday, 17 September 2010 07:31 0diggsdigg

  [​IMG]
  Katibu mkuu wa CCM Mr Yusuf Makamba

  Tumaini Msowoya, Iringa na Boniface Meena, Bariadi
  WAFUASI wa CCM jana walisababisha tafrani kubwa kwenye kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa baada ya kutinga kwenye mkutano wake na magari yaliyokuwa yakipiga muziki kwa sauti kubwa. Tukio hilo limetoa siku mbili baada ya wafuasi wengine wa CCM kufanya vurugu mkoani Mwanza, Kilimanjaro na Iringa.

  Kwenye tukio lililotokea juzi katika Jimbo la Iringa Mjini, gari lililokuwa na nembo ya chama hicho tawala kukatisha kwenye eneo ambalo Chadema ilikuwa ikiendesha mkutano wake wa kampeni mkoani Iringa na kusababisha dereva wake kupigwa na kujeruhiwa.

  Pia wafuasi wengine wa CCM mkoani Kilimanjaro walisababisha kurushiana makonde kavukavu na wanachama wa TLP baada ya kutaka kuondoa bango la kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Augustine Mrema lililowekwa kihalali kwenye moja ya barabara za kuingia jimboni humo.

  Mjini Mwanza, mwandishi wa gazeti la Mwananchi alishambuliwa na walinzi wa CCM wanaojulikana kwa jina la Green Guard ambao walitaka kumuondoa kwa nguvu pamoja na waandishi wa vyombo vingine kwenye mkutano wa kampeni za mgombea ubunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndasa.

  Kabla ya matukio hayo kutulia, jana kitendo cha gari la CCM kupiga kelele kwenye mkutano wa Dk Slaa kuliamsha mapigano yaliyodumu kwa dakika kadhaa kati ya wafuasi wa CCM na Chadema kabla polisi kuingilia kati.

  Tukio hilo lililotokea kwenye uwanja wa Dutwa kwenye Jimbo la Bariadi Magharibi mkoani Shinyanga.

  Vurugu hizo ziliibuka baada ya magari mawili ya CCM kupita kwa nyakati tofauti kwenye mkutano huo yakiwa yanapiga muziki kwa sauti kubwa wakati Dk Slaa na mgombea mwenza wake, Saidi Mzee Said walipokuwa wakihutubia wananchi wa jimbo hilo.

  Gari la kwanza aina ya Toyota Landcruiser lilipita eneo hilo wakati Mzee akihutubia na hivyo kulazimika kusitisha hotuba yake kwa muda kupisha kilele hizo.

  Mzee aliendelea na hotuba yake baada ya gari hilo kupita na kumpisha Dk Slaa ambaye naye alilazimika kusitisha hotuba yake baada ya gari jingine la CCM aina ya Toyota Canter kupita eneo hilo likiwa linapiga muziki.

  Lakini gari hilo la pili lilisimama kwa muda uwanjani hapo likiendelea na kelelez a muziki, jambo ambalo lilimkera Dk Slaa na kuwaagiza polisi kuwashughulikia wafuasi hao wa CCM.

  Kwa mujibu wa Dk Slaa, ambaye anaonekana kuibukia kuwa mpinzani mkubwa kwenye kinyang'anyiro cha urais, kitendo cha wafuasi hao kufanya fujo kwenye mkutano wa Chadema ni kinyume na taratibu na kanuni za Sheria ya Uchaguzi.

  Lakini kabla polisi hawajafika, tayari wafuasi wa Chadema walishalivamia gari hilo na kuzima muziki huo kisha kumshusha dereva wake na kuanza kumpiga.

  Dereva huyo alikuwa akipigwa na kuhojiwa ili aelezea sababu za kusimamisha gari eneo hilo la mkutano na kufungulia muziki kwa sauti ya juu.

  Hata hivyo, polisi walifika eneo la tukio kumwokoa dereva huyo.

  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasa alilimbia gazeti hili baadaye kuwa polisi mkoani humo inamshikilia dereva huyo na kuendelea na uchunguzi.

  Vurugu ningine zilitokea juzi kwenye Jimbo la Iringa Mjini baada ya dereva wa gari lenye nembo ya CCM kupigwa na kujeruhiwa wakati alipokatisha kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema.

  Mbali na hilo, muungano wa vyama vya Upinzani mkoani Iringa umelalamikia kufanyiwa fujo baada ya wafuasi wake kuvamiwa na vijana wanaodaiwa kuwa wa CCM wakati wakitokea kwenye mkutano wa kampeni. Wafuasi hao walinyang’anywa bendera tatu na kipaza sauti kimoja.

  Wakizungumza na Mwananchi, mashuhuda wa tukio la dereva wa gari la CCM kushambuliwa walisema wafuasi wa Chadema walipandahasira baada ya gari hilo kukatisha mara mbili kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa ukifanyika kwenye kituo kikuu cha mabasi mjini Iringa.

  Baada ya kukatiza mara ya kwanza, wafuasi hao walikosa uvumilivu na kulizingira gari hilo lilipopita kwa mara ya pili na kumkuda dereva wake.

  Mgombea wa udiwani wa Kata ya Kitanzini/Miyomboni kwa tiketi ya Chadema, Gervas Kalolo alisema kuwa vijana hao walifanya hivyo kwa hasira kwa madai kuwa gari hilo halikupaswa kukatisha kwenye eneo la mkutano wao.

  “Ni kinyume cha sheria kwa gari lenye nembo za chama kingine kukatisha kwenye mkutano usio wao... bahati nzuri kulikuwa na askari ambao waliingilia kati na hivyo likasalimika,” alisema Kalolo.

  Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Iringa Mjini, Abeid Kiponza alisema kuwa gari hilo lilikuwa limetokea kwenye msiba wa mmoja wa mwanachama wao aliyekuwa amefariki na kwamba hakukuwa na njia nyingine zaidi ya barabara hiyo.

  “Kuna mwanachama wetu alifariki hivyo gari lilikuwa limetokea kwenye msiba eneo la Makanyagio kuja mjini. Lingepita wapi kama sio stendi ambako kuna njia ya sehemu lilikokuwa likitakiwa kwenda,” alihoji.

  Mwenyekiti huyo alikiri kuwa dereva wa gari hilo alijeruhiwa kifuani baada ya kupigwa na wafuasi wa Chadema, lakini bado hawajafungua mashtaka polisi.

  Katika tukio la pili, Viongozi wa muungano wa vyama vya upinzani wamelalamikia kuvamiwa na vijana wanaodaiwa kuwa wa CCM wakati wakitokea kwenye mkutano wao uliofanyika Kata ya Kitwiru na kunyang’anywa bendera na kipaza sauti.

  Umoja huo unahusisha vyama tofauti vilivyoamua kusimamisha mgombea mmoja wa nafasi tofauti bila ya kushirikisha wagombea kutoka CCM na Chadema.

  Katibu wa NCCR-Mageuzi mkoani Iringa, James Mwamugiga alisema kuwa tukio hilo lilitokea eneo la Isimila ambako vijana waliokuwa kwenye gari la mbele yao, walishuka na kuuvamia msafara wao.

  “Ilikuwa tumeongozana, CCM mbele na sisi nyuma; bahati mbaya wenzetu wakasimama na sisi ikabidi tupunguze mwendo, ndio hapo tukashangaa wameruka kwenye gari lao na kuja kutuvamia bila makosa yoyote,” alisema Mwamugiga.

  Alidai kuwa waliamua kukaa kimya licha ya kuwa walinyang’anywa bendera tatu, mbili zikiwa za NCCR na moja ya TLP.

  Hata hivyo, CCM imekanusha kuhusika kwa njia yoyote katika tukio hilo na kuwa hizo ni tuhuma zinazotolewa kwa lengo la kukipaka matope chama hicho.

  “Nani aliyenyang’anya bendera na kipaza sauti? hili sio la kweli kabisa kwa kuwa mimi mwenyewe nilikuwepo kwenye msafara huu, lakini sikuona tukio kama hilo hata mara moja,” alisema mwenyekiti wa CCM wa Iringa Mjini, Abedi Kiponza.
  Wagombea wanaowania jimbo la Iringa mjini ni Monica Mbega (CCM), Peter Msigwa (Chadema) na Mariam Mwakingwe (NCCR-Mageuzi).
   
 2. Profesy

  Profesy Verified User

  #2
  Sep 17, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wamepata wasiwasi nini?:confused2:
   
 3. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Joto limeanza kupanda na bado majuma sita mbele ngoma ni nzito
   
Loading...