Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
Wanachama na makada mbalimbali wa chama cha mapinduzi CCM wameuijia juu uongozi wa chama hicho Kwa kuhoji kwamba chama hicho kimekosa hoja, au viongozi wake ni mizigo? Kwanini hakuna kiongozi yoyote aliyeweza kukanusha au kujibu tuhuma zilizotolewa na Kiongozi wa upinzani nchini Zanzibar Mhe. Maalim Seif? Wengi wamedai kuwa yawezekana hoja za Maalim Seif ni za msingi na zina ukweli.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa, na wasomi mb...alimbali wamezungumzia sakata hilo na kudai kwamba Siasa ili ziwe siasa ni lazima kuhusisha pande mbili za siasa au zaidi, Kwa maana kwamba upande mmoja ukisema hivi, upande mwingine unasema vile, hivyo; kama upande mmoja unaushutumu upande mwingine na upande unaoshutumiwa hauna majibu, ni dhahiri kwamba hoja za upande mmoja ni za kweli.
Wakizungumza wanachama hao wakongwe na viongozi wa chama hicho, ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao wala vyeo vyao, walidai kwamba, chama cha mapinduzi CCM kimeendelea kupoteza mvuto na kumegeka siku hadi siku kutokana na uelewa wa wananchi kukua, wananchi wanayapima yaliyozungumzwa wakati wa kampeni na wanalinganisha na hali halisi ya sasa, ni tofauti kabisa, ni kama chama hicho kiliwadanganya wananchi, na hakisimamii kiliyoyasema.
Wakizungumzia hoja za Maalim Seif Kwa nyakati tofauti, wamedai kwamba kama chama hicho kimeshindwa kwenda Kwa wananchi kueneza Sera zake na itikadi yake na badala yake kimeamua kuwatumia watu mamluki kama Profesa Lipumba kuuvuruga upinzani, ni wazi chama hicho kimehama kutoka kwenye misingi yake na kimeanza kutkeleza majukumu mengine yasiyo ya kisiasa.
CCM haizungumzii ushindi wa Zanzibar wala mkwamo wa kisiasa nchini humo, hii inaonesha kwamba chama hicho kinaogopa kuikuza mijadala hiyo kwasababu hakina hoja za kujibu na badala yake kimetumia mgongo wa vyombo vya dola kutawala.
Akijibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari, Maalim Seif alisema kwamba, CCM haikushinda Uchaguzi mkuu nchini Zanzibar, na ubabe uliotumika kufuta matokeo ni ukweli kwamba CCM haina tena uhalali wa kuongoza. Pia Maalim Seif aliongeza akisema kwamba, amani nchini Zanzibar ipo mikononi mwake na wala sio vyombo vya dola, na vijana wapo tayari wanamsubiri akisema 'Suu', waidai haki yao.
Wanachama wa CCM hususan mijini wamekuwa wakitamka wazi kwamba, hawana maslahi yoyote na utawala wa CCM wala kwenye chama hicho, na wanatambua kwamba nchi hii ni moja na ni ya wote, na kila mtanzania anayo haki ya kuchaguliwa kuwa kiongozi na haki ya kujichagulia kiongozi anayempenda, hivyo hawaoni haja ya kuendelea kuamini kwamba kiongozi wa nchi lazima aendelee kutoka CCM, wamedai wapo tayari kuikabidhi nchi Kwa viongozi nje ya CCM.
Mmoja wa viongozi wa CCM niliyepata kumuuliza machache kuhusiana na mipasuko hiyo ya ndani ya chama hicho, alisema Kwa sasa hana LA kuzungumza, lakini huenda yanayosemwa ni kweli, lakini naye aliomba asitajwe jina lake.