CCM wasaka kura ya mjumbe wodini

CCM wasaka kura ya mjumbe wodini

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
JITIHADA za Kamati za Bunge Maalum la Katiba, kupata uungwaji mkono wa ibara walizozijadili, jana ziliilazimisha kamati namba 12 kumfuata mjumbe wake wodini apige kura.

Mjumbe huyo ni Thomas Mgori, ambaye alilazwa tangu juzi katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kupigwa na wenzake walipokuwa wakibishana juu ya uhalali wa vikao vya Bunge hilo lililosusiwa na wajumbe wa UKAWA.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge ili ibara ipitishwe kwenye kamati husika itahitaji theluthi mbili ya kura za wajumbe wote kutoka Tanzania bara na idadi hiyo hiyo kutoka Zanzibar.

Katika kuhakikisha hilo linatimia kamati namba 12 ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Thuwabay Kissassi, ilikwenda kwa Mgori ambaye alipiga kura ya wazi.

Mgori alizipigia kura ya ndiyo kuanzia sura ya pili hadi ya tano isipokua ibara ya 59 ambapo aliipinga.

Mgori alisema kuwa amepiga kura ya wazi kwa kuwa kanuni za Bunge hilo zimetoa fursa kwa mjumbe kupiga ya wazi au siri kulingana na matakwa yake.

Alibainisha kuwa amepinga ibara ya 59 kwa kuwa inapendekeza mfungwa mlemavu aruhisiwe kuingia jela au mahabusu na magongo yake.

Alisema anapinga pendekezo hilo kwa sababu anaamini kuwa mhusika anaweza kutumia magongo hayo kuwadhuru wenzake.

Mgori alisema mlemavu huyo anaweza asiyatumie magongo hayo kuwadhuru wenzake lakini kuna uwezekano akapokonywa na wababe ambao watawadhuru wengine.

Aliongeza kuwa licha ya ugonjwa alinao ameamua kupiga kura hiyo kwa kuwa ni haki yake ya kimsingi na alishiriki kwenye majadiliano hivyo hakuona sababu ya kukosa kufanya uamuzi wa kile alichokijadili.

“Naamini kuwa kura ni kitu cha thamani sana ndiyo maana sitaki kuikosa fursa hiyo, kura moja inaweza kubadilisha jambo lolote lile,”alisema.

Aliongeza kuwa aliomba afanye hivyo akiwa hospitalini hapo baada ya kujiridhisha yuko sawa kisaikolojia na afya yake inaendelea vizuri.

Katika ujumbe uliokwenda hospitalini hapo alikuwapo Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel na wajumbe wengine walioweka wazi kuwa Mgori ana haki ya kupiga kura.

Joel alibainisha kuwa Mgori, alipelekewa karatasi ya maalum na bango kitita vinavyoendana na upigaji kura.

Katika upigaji kura huo Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba 12, Kissassi alimsomea vifungu vyote Mgori ambaye alivikubali kwa kupiga kura ya ndiyo.

Mgori alipigwa na watu wasiojulikana mapema na kulazwa katika hospitali ya mkoa ya Dodoma juzi.
 
Hayo majadiliano aliyashiriki lini akiwa hospitali?
 
Hayo majadiliano aliyashiriki lini akiwa hospitali?

Ndio ujue jitu kama hilo limepelekwa kwa kazi moja tu. Kuunga mkono wanayoyataka ccm na kuyapinga wasiyoyataka. Hakuna katiba hapo bali ni kitanzi cha kuja kuchinjania hapo baadae.
 
Back
Top Bottom