CCM wapinga serikali tatu

kbm

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
5,144
Likes
268
Points
180
kbm

kbm

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
5,144 268 180
Dodoma. Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepinga muundo wa Muungano wa Serikali tatu unaopendekezwa katika rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Chama hicho tawala kimesema bado kinaamini katika muundo wa Serikali mbili.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kwamba mapendekezo yaliyowasilishwa mbele ya Tume hiyo yanabaki kama yalivyo, hivyo msimamo wao ni kuwapo kwa muungano wenye muundo wa Serikali mbili.
“Mapendekezo ambayo ndiyo msimamo wa chama tulishayawasilisha kwenye Tume kuwa sisi tunapendekeza mfumo wa Serikali mbili na siyo tatu wala moja,” alisema Nape alipokuwa akitoa taarifa ya uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyokutana usiku wa kuamkia jana kujadili suala hilo.
Kauli ya Nape inafanana na matamshi ambayo yamewahi kutolewa na baadhi ya wanasiasa wakongwe ambao ni makada wa CCM wakiwamo, mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na John Malecela, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na baadhi ya wabunge ambao mara kadhaa wamekaririwa wakipinga pendekezo la Serikali tatu.
Hata hivyo, Nape alisema matamshi ya viongozi hao yalikuwa ni maoni yao binafsi na kauli yake ndiyo rasmi ya chama hicho... “Mimi ndiye msemaji wa chama hiki. Ndiye ninayeeleza msimamo wa chama chetu, yanayozungumzwa na watu wengine hata kama ni viongozi siyo msimamo wa chama ni maoni yao binafsi.”
Habari ambazo gazeti hili ilizipata zinasema katika kikao hicho cha CC kulijitokeza hofu ya suala la wananchi kuwa na mamlaka ya kuwang’oa wabunge ikiwa hawatatekeleza masilahi yao na kwamba pendekezo hilo lina upungufu kwani halitafsiri masilahi hayo ni yapi.
Waunda kamati
Nape alisema rasimu iliyotolewa na Tume siyo waraka wa mwisho kwani bado unatoa fursa kwa Watanzania kuijadili na kutoa maoni yao na kwamba CCM kitatumia nafasi hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu jambo hilo.
Alisema chama hicho kitawasiliana na wanachama wake zaidi ya 6,000 nchini ili waendelee kutoa maoni yao kuhusu suala hilo.
“Wengi wanadhani rasimu hii ndiyo ya mwisho… hii ni ya mwanzo tu, itajadiliwa italetwa ya pili na ya tatu, kwa hiyo hatuwezi kusema kilichoelezwa kwenye tume ndiyo msimamo. Ndiyo maana tumeamua kurejesha suala hili kwa wanachama wetu liendelee kujadiliwa,” alisema na kuongeza:
“Kama wanachama wetu wakiamua kuwepo kwa Serikali tatu, hatutachakachua, tutayachukua na kuyapeleka kama msimamo wetu, lakini tutakubaliana ikiwa uamuzi utakuwa umewahusisha wanachama wetu katika ngazi zote.”
“Hatuangalii kipengele kimoja tu. Tutapitia vipengele vyote hadi kuzimaliza kurasa zote zaidi ya 70 zinazoainisha mapendekezo ya Tume ya Jaji (Joseph) Warioba.”
Alisema wanachama wake wanapaswa kuipitia na kuijadili rasimu hiyo kwa kuzingatia mapendekezo kilichoyatoa awali wakati wa mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba Mpya.
“Tulitoa maoni yetu na sasa tunaijadili Rasimu ya Katiba Mpya kwa kuzingatia maoni yetu yale, CCM tunakwenda kwa mujibu wa sheria,” alisema. Habari kutoka ndani ya CC ya CCM zinasema chama hicho kimeipa kazi kamati ambayo ilitumika kuandaa mapendekezo yake awali, kupitia rasimu hiyo na kufanya ulinganisho wa yale ambayo chama hicho kilipendekeza dhidi ya yale yaliyozingatiwa katika Rasimu ya Katiba hiyo.
“Kamati itafanya ulinganisho na baada ya hapo tutakwenda kwa wanachama kuwaeleza ni yapi tulipendekeza kama chama na ni yapi ambayo Tume imeyazingatia na hapo tutapata mawazo yao ambayo tutayatumia katika ngazi ya mabaraza ya Katiba,” kilisema chanzo chetu.

CHANZO: Mwananchi

===
Warioba: Bila Serikali tatu Muungano utavunjika

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, JajiJoseph Warioba, ametahadharisha kuwa kung'ang'ania kuendesha nchi kwa kufuata mfumo wa sasa wa utawala wa Serikali mbili ili kuepuka gharama za uendeshaji wa serikali tatu kunaweza kusababisha kuvunjika kwa Muungano siku za usoni.
Alisema Watanzania wanapaswa kuamua kujitoa kwa gharama ndogo kwa ajili ya serikali tatu kwa kukubalia mapendekezo ya rasimu ya Katiba mpyavinginevyo wataukosa kabisa Muungano wenyewe ambao umedumu kwa takribani miaka 49 sasa.
Jaji Warioba aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni ya ITV wakati wa mahojiano na kutoa mambo muhimu juu ya rasimu ya katiba iliyozinduliwa Juni 3, mwaka huu.
"Wenzetu wa Zanzibar walikuwa na mambo mengi ya kutoridhishwa juu ya Muungano kuliko Tanzania Bara. Ni vema tukatafuta njia ya kupunguza gharama badala ya kuiepuka kama tunataka kuuokoa Muungano. Maamuzi haya tumeyatoa baada ya kutafakari maoni ya waliowengi na siyo hivi hivi tu. Tumezingatia mapendekezo ya Watanzania wengi,” alionya Jaji Warioba.
Jaji Warioba pia alijibua changamoto zinazotolewa na watu juu ya dira ya taifa, alisema Tume imeweka wazi katika utangulizi wa rasimu yake kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaongozwakwa misingi ya demokrasia na utawala bora na kusisitiza juu msingi ya kujitegemea.
"Serikali inatakiwa kutoataarifa zake kila mwaka kwa wananchi katika Bunge la Agosti ni jinsi gani imefanya kazi bila kujali itikadi za kisiasa," alisema.
Jaji Warioba alizitaja maeneo ambayo yalijadiliwa zaidi katika ukusanyaji wa maoni ya katiba mpya kuwa ni ardhi, elimu na afya.
“Kwenye ardhi kulikuwa na matatizo mengi hasa juu ya umiliki wake na matumizi yake kuna ubishani mwingi juu nani mwenye haki ya milki ya ardhi. Pia kuna suala matumizi ya ardhi kati wawekezaji na wananchi, Hata hivyo, ardhi siyo suala la Muungano,” alisema Jaji Warioba.
Kauli ya Jaji Warioba inatolewa siku chache tu baada wanataaluma na wansisiasa kuelezea wasiwasi wao juu ya mfumo wa serikali tatu wakisema utakuwa wa gharama kubwa na ni kuzidi kuwabebesha mzigo walipa kodi.
Wakati huo huo; Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) kimeyataka mabaraza ya katiba kupambana kwa ajili ya kuondoa mapungufu juu ya haki za wanawake na watoto ili kuleta haki, usawa na maendeleo ya nchi.
“Tamwa inaamini katika kuleta mabadiliko ambayo ushawishi wa maendeleo katika Tanzania ni muda muafaka kwa mabaraza kuangalia rasimu na kuhakikisha mapungufu yanatolewa kabisa kuwapo kwa usawa kwa wanawake na wanaume Tanzania,” alisema Mwenyekiti wa Tamwa Valerie Msoka.
Msoka alisema kunahitajika nguvu za wanaume na wanawake katika kukabiliana na tatizo la unyanyasaji wa kijinsia na sheria kandamizi kwa wanawake na watoto wakike.
Aliipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kutoa rasimu hiyo kwani itakuwa ni fursa kwa wananchi, wanawake na wanaume kushiriki katika demokrasia ya nchi yao, hasa kwa kulinda mwanamke na mtoto wa kike dhidi ya vita ubakaji, ndoa za mapema na ukeketaji.
Juni 3, mwaka Tume hiyoilizindua rasimu ya kwanza ya katiba ambapo miongoni mwa masuala ambayo ilikuwa ni pamoja na kuundwa kwa serikali tatu idadi yamambo ya Muungano kuwa saba kutoka 22; nafasi ya Spika wa Bungena Naibu wake kutotokana na chama chochote cha siasa.
Mengine ni mawaziri kutokuwa wabunge; nafasi za uteuzi wa Rais kuidhinishwa na Bunge; kuongeza umri wa kuwa mbunge kutoka miaka 21hadi 25; kuingizwa kwa ibara za haki ya kupata habari katika katiba.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi hasa Zanzibar wameeleza kutokufurahishwa na mapendekeo hayo wakitaka mamlaka kamili ya Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE
===
Serikali tatu: Kamati Kuu CCM yagwaya

Kamati Kuu ya Chama ChaMapinduzi (CCM) imekwepa kutoa maimamo wake juu ya rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Kurekebisha Katiba Juni 3, mwaka huu na badala yake wametupa mpira huo kwa wanachama wake.
Kamati hiyo iliyokutana mjini Dodoma juzi, ilijiweka kando na pandekezo la kuanzishwa kwa mfumo wa serikali tatu kama inavyosema rasimu ya sasa na badala yake imetaka wanachama waijadili kwanza rasimu na kutoa maoni yao.
Ingawa Kamati Kuu imesisitiza kwamba sera ya CCM ni mfumo wa Muungano wa serikali mbili, kitabadili sera yao na msimamo huo ili uwe wa serikali tatu, ikiwa tu wanachama wake wataamua hivyo.
CCM iliyoanzishwa Februari 5, 1977 kutokana na Chama cha Afro Shiraz (ASP) cha Zanzibar na Chama cha Tanganyika African Nation Union (Tanu) cha Tanganyika, inasimamia na kutetea mfumo wa serikali mbili; za Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Msimamo huo wa CCM umedumu kwa takriban miaka 49 sasa, tangu Tanganyika kuungana naZanzibar Aprili 26, 1964, siku iliyozaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo, rasimu iliyochapishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba, pamoja na mambo mengine, inapendekeza kuwapo mfumo wa serikali tatu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema chama hicho kimetoa uhuru kwa wanachama wake kujadili Rasimu ya Katiba mpya, kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa.
Nape alikuwa akiwasilisha taarifa ya kikao cha Kamati Kuu (CC)ya CCM, kilichofanyika juzi mjini hapa na kuongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.
Alisema katika mjadala huo, CCM inasimamia uwapo wa serikali mbili, isipokuwa kama wanachama wataamua vinginevyo.
“Kama wanachama wetu wakiamua kuwapo kwa serikali tatu, hatutachakachua … wanachama wakiamua hatutakataa, lakini lazima hiyo iwe ime-involve (husisha) wanachama,” alisema Nape.
Tangu kuzinduliwa kwa rasimu ya kwanza ya Katiba mpya, mjadala mkubwa umehusisha zaidi pendekezo la kuwapo serikali tatu.
Miongoni mwa wanaolijadili pendekezo hilo, ni wabunge na mawaziri wanaotokana na CCM, wakipingana kutokana na baadhi yao kuunga mkono, huku wengine wakipinga.
Wanaounga mkono, wanaelezea kuwa pamoja na mambo mengine, Wazanzibari wamekuwa na kasumba ya kuulalamikia Muungano, hivyo ni fursapekee ya kuwaacha wajisimamie.
Lakini wanaolipinga pendekezo hilo, wanatoahoja tofauti, ikiwamo ukubwa wa gharama za uendeshaji wa serikali tatu na hofu ya Zanzibar kushindwa kujiendesha kiuchumi na kiusalama.
Hata hivyo, Nape alisema jana kuwa CCM haijatoa msimamo wa moja kwa moja, isipokuwa kupitia maoni binafsi ya wanachama wake, wakiwamo wabunge na mawaziri wa serikali ya chama hicho.
Alisema, tamko rasmi la CCM ni kuhusu ushiriki wa wanachama katika mabaraza yanayopendekezwa kuundwa ndani ya chama hicho na jumuiya zake.
Alisema kwa mujibu wa maombi ya ushiriki wa kitaasisi, CCM inakusudia kuhusisha pia jumuiya zake katika kuijadili rasimu ya katiba, kuanziakwenye matawi, wilaya, mkoa hadi taifa.
Kwa mujibu wa Nape, ushiriki wa jumuiya hizo hautokani na maelekezo ya CCM, bali utashi na utayari wa ‘vyombo’ hivyo katika ustawi wa chama hicho.
Alisema Kamati Kuu ya chama hicho imeagiza wanachama wake kujipanga na kushiriki kwa uhuru kuijadili rasimu hiyo.
“Sisi hatuangalii kipengele kimoja tu. Tutapitia kipengele kwa kipengele hadi kuzimaliza kurasa zote zinazoainisha mapendekezo ya Tume ya Jaji Warioba,” alisema Nape.
Alisema wana-CCM wanapaswa kuipitia na kuijadili rasimu hiyo kwakuzingatia mapendekezoyao (CCM) yaliyotolewa wakati wa mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba mpya.
“Tulitoa maoni yetu na sasa tunaijadili rasimu yaKatiba mpya kwa kuzingatia maoni yetu yale,” alisema Nape.
WITO KWA TUME
Nape alisema Kamati Kuuya CCM inapendekeza kwa Tume ya Jaji Warioba kuongeza wigo wa kuielimisha jamii kuhusu mchakato wa Katiba mpya, ikigusia zaidi hatua ya rasimu zitakazopitiwa.
Alisema hivi sasa kuna hali ya ‘sitofahamu’ kwa umma baada ya kutangazwa kwa rasimu ya kwanza ya Katiba mpya.
Hata hivyo, alisema Kamati Kuu inahimiza raia kushiriki mjadala warasimu hiyo kwa amani, utulivu na kuvumiliana.
Mchakato wa kuunda Katiba mpya umefikia hatua ya kutolewa rasimu ya kwanza itakayojadiliwa katika mabaraza ya katiba ya wilaya na asasi za kijamiikisha kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum laKatiba kwa hatua zaidi.
Mjadala wa rasimu hiyo katika ngazi za wilaya namabaraza, unatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti31, mwaka huu.
Hii ni mara ya pili CCM inarejesha kwa wanachama wake hoja ya kuwako kwa mfumo wa serikali tatu ndani Muungano. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwanzoni mwa miaka ya90 baada ya kundi la wabunge wa G55 kuwasilisha bungeni hoja ya kuuwako kwa serikali ya Tanganyika katika muundo wa Muungano.
Azimio la kuundwa kwa serikali hiyo liliwasilishwa serikalini, lakini kabla ya kuanza kutekelezwa, Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliibuka na kuwapinga wabunge hao kwenye kikako cha Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyoitishwa kujadili sualahilo.
Katika hoja zake, Mwalimu Nyerere alisema mfumo wa serikali tatu haukuwa sera ya CCM na kutaka suala hilo lirejeshwe kwawanachama kupata maoni yao. Wengi wanadaiwa kuukataa mfumo wa serikali tatu hivyo hoja ya Tanganyikaikafa.
Hata hivyo, hoja ya Tanganyika haikufa hivi hivi tu kwani iliondoka na baadhi ya viongozi, akiwamo Waziri Mkuu naMakamu wa Kwanza Rais,John Malecela pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Marehemu Horace Kolimba, wakituhumiwa kutokumshauri Rais Ali Hassan Mwinyi wakati huo.
Mfumo wa serikali tatu pia ulikwisha kuwaweka pabaya baadhi ya viongozi wa Zanzibar, akiwamo aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais, Mzee Abdul Jumbe Mwinyi na hata Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) sasa, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati huo akiwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

CHANZO: NIPASHE
 
Headless Person

Headless Person

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2012
Messages
307
Likes
0
Points
0
Headless Person

Headless Person

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2012
307 0 0
CCM ni kama tundu la choo, kila uchafu unaingia na kutoka humo!
 
M

mujore

Member
Joined
Jan 9, 2013
Messages
89
Likes
0
Points
0
Age
29
M

mujore

Member
Joined Jan 9, 2013
89 0 0
Dodoma. Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepinga muundo wa Muungano wa Serikali tatu unaopendekezwa katika rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Chama hicho tawala kimesema bado kinaamini katika muundo wa Serikali mbili.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kwamba mapendekezo yaliyowasilishwa mbele ya Tume hiyo yanabaki kama yalivyo, hivyo msimamo wao ni kuwapo kwa muungano wenye muundo wa Serikali mbili.
"Mapendekezo ambayo ndiyo msimamo wa chama tulishayawasilisha kwenye Tume kuwa sisi tunapendekeza mfumo wa Serikali mbili na siyo tatu wala moja," alisema Nape alipokuwa akitoa taarifa ya uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyokutana usiku wa kuamkia jana kujadili suala hilo.
Kauli ya Nape inafanana na matamshi ambayo yamewahi kutolewa na baadhi ya wanasiasa wakongwe ambao ni makada wa CCM wakiwamo, mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na John Malecela, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na baadhi ya wabunge ambao mara kadhaa wamekaririwa wakipinga pendekezo la Serikali tatu.
Hata hivyo, Nape alisema matamshi ya viongozi hao yalikuwa ni maoni yao binafsi na kauli yake ndiyo rasmi ya chama hicho... "Mimi ndiye msemaji wa chama hiki. Ndiye ninayeeleza msimamo wa chama chetu, yanayozungumzwa na watu wengine hata kama ni viongozi siyo msimamo wa chama ni maoni yao binafsi."
Habari ambazo gazeti hili ilizipata zinasema katika kikao hicho cha CC kulijitokeza hofu ya suala la wananchi kuwa na mamlaka ya kuwang'oa wabunge ikiwa hawatatekeleza masilahi yao na kwamba pendekezo hilo lina upungufu kwani halitafsiri masilahi hayo ni yapi.
Waunda kamati
Nape alisema rasimu iliyotolewa na Tume siyo waraka wa mwisho kwani bado unatoa fursa kwa Watanzania kuijadili na kutoa maoni yao na kwamba CCM kitatumia nafasi hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu jambo hilo.
Alisema chama hicho kitawasiliana na wanachama wake zaidi ya 6,000 nchini ili waendelee kutoa maoni yao kuhusu suala hilo.
"Wengi wanadhani rasimu hii ndiyo ya mwisho… hii ni ya mwanzo tu, itajadiliwa italetwa ya pili na ya tatu, kwa hiyo hatuwezi kusema kilichoelezwa kwenye tume ndiyo msimamo. Ndiyo maana tumeamua kurejesha suala hili kwa wanachama wetu liendelee kujadiliwa," alisema na kuongeza:
"Kama wanachama wetu wakiamua kuwepo kwa Serikali tatu, hatutachakachua, tutayachukua na kuyapeleka kama msimamo wetu, lakini tutakubaliana ikiwa uamuzi utakuwa umewahusisha wanachama wetu katika ngazi zote."
"Hatuangalii kipengele kimoja tu. Tutapitia vipengele vyote hadi kuzimaliza kurasa zote zaidi ya 70 zinazoainisha mapendekezo ya Tume ya Jaji (Joseph) Warioba."
Alisema wanachama wake wanapaswa kuipitia na kuijadili rasimu hiyo kwa kuzingatia mapendekezo kilichoyatoa awali wakati wa mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba Mpya.
"Tulitoa maoni yetu na sasa tunaijadili Rasimu ya Katiba Mpya kwa kuzingatia maoni yetu yale, CCM tunakwenda kwa mujibu wa sheria," alisema. Habari kutoka ndani ya CC ya CCM zinasema chama hicho kimeipa kazi kamati ambayo ilitumika kuandaa mapendekezo yake awali, kupitia rasimu hiyo na kufanya ulinganisho wa yale ambayo chama hicho kilipendekeza dhidi ya yale yaliyozingatiwa katika Rasimu ya Katiba hiyo.
"Kamati itafanya ulinganisho na baada ya hapo tutakwenda kwa wanachama kuwaeleza ni yapi tulipendekeza kama chama na ni yapi ambayo Tume imeyazingatia na hapo tutapata mawazo yao ambayo tutayatumia katika ngazi ya mabaraza ya Katiba," kilisema chanzo

si zinakaribia za wazanzibari kujipatia mamambo tunayoyataka.. long kipindi nilisema tunawabura sisi watanganyika ona sasa.. yale yale wanayosema zazenj ndo hayo yanakua.. zanzibar first... tunabura tanganyika and all... hakuna muungano dhalim huu ulokuwepo for long time.. sasa ni our way or hamna njia nyengine.. zanzibar kimpango wao na tanganyika kimpango wao first.. halafu kwanza nyinyi nyikazz anzeni kutafuta nyumba sio.. hamna makaazi nyinyi mlilala wakati sisi tunatengezeza makaazi,, nyinyi hamnabunge ikulu wala katiba tanganyika... zenj kila kitu kipo sio.... dua ninawaombea ex ndugu tanganyika.

G

Gitifii

Senior Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
190
Likes
4
Points
35
G

Gitifii

Senior Member
Joined Dec 27, 2012
190 4 35
Afadhali jamani wanafagia njia ya zanzibar kwenda kufia mbele kelele ziishe.
 
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
4,882
Likes
68
Points
135
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
4,882 68 135
Dodoma. Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepinga muundo wa Muungano wa Serikali tatu unaopendekezwa katika rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Chama hicho tawala kimesema bado kinaamini katika muundo wa Serikali mbili.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kwamba mapendekezo yaliyowasilishwa mbele ya Tume hiyo yanabaki kama yalivyo, hivyo msimamo wao ni kuwapo kwa muungano wenye muundo wa Serikali mbili.
“Mapendekezo ambayo ndiyo msimamo wa chama tulishayawasilisha kwenye Tume kuwa sisi tunapendekeza mfumo wa Serikali mbili na siyo tatu wala moja,” alisema Nape alipokuwa akitoa taarifa ya uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyokutana usiku wa kuamkia jana kujadili suala hilo.
Kauli ya Nape inafanana na matamshi ambayo yamewahi kutolewa na baadhi ya wanasiasa wakongwe ambao ni makada wa CCM wakiwamo, mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na John Malecela, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na baadhi ya wabunge ambao mara kadhaa wamekaririwa wakipinga pendekezo la Serikali tatu.
Hata hivyo, Nape alisema matamshi ya viongozi hao yalikuwa ni maoni yao binafsi na kauli yake ndiyo rasmi ya chama hicho... “Mimi ndiye msemaji wa chama hiki. Ndiye ninayeeleza msimamo wa chama chetu, yanayozungumzwa na watu wengine hata kama ni viongozi siyo msimamo wa chama ni maoni yao binafsi.”
Habari ambazo gazeti hili ilizipata zinasema katika kikao hicho cha CC kulijitokeza hofu ya suala la wananchi kuwa na mamlaka ya kuwang’oa wabunge ikiwa hawatatekeleza masilahi yao na kwamba pendekezo hilo lina upungufu kwani halitafsiri masilahi hayo ni yapi.
Waunda kamati
Nape alisema rasimu iliyotolewa na Tume siyo waraka wa mwisho kwani bado unatoa fursa kwa Watanzania kuijadili na kutoa maoni yao na kwamba CCM kitatumia nafasi hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu jambo hilo.
Alisema chama hicho kitawasiliana na wanachama wake zaidi ya 6,000 nchini ili waendelee kutoa maoni yao kuhusu suala hilo.
“Wengi wanadhani rasimu hii ndiyo ya mwisho… hii ni ya mwanzo tu, itajadiliwa italetwa ya pili na ya tatu, kwa hiyo hatuwezi kusema kilichoelezwa kwenye tume ndiyo msimamo. Ndiyo maana tumeamua kurejesha suala hili kwa wanachama wetu liendelee kujadiliwa,” alisema na kuongeza:
“Kama wanachama wetu wakiamua kuwepo kwa Serikali tatu, hatutachakachua, tutayachukua na kuyapeleka kama msimamo wetu, lakini tutakubaliana ikiwa uamuzi utakuwa umewahusisha wanachama wetu katika ngazi zote.”
“Hatuangalii kipengele kimoja tu. Tutapitia vipengele vyote hadi kuzimaliza kurasa zote zaidi ya 70 zinazoainisha mapendekezo ya Tume ya Jaji (Joseph) Warioba.”
Alisema wanachama wake wanapaswa kuipitia na kuijadili rasimu hiyo kwa kuzingatia mapendekezo kilichoyatoa awali wakati wa mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba Mpya.
“Tulitoa maoni yetu na sasa tunaijadili Rasimu ya Katiba Mpya kwa kuzingatia maoni yetu yale, CCM tunakwenda kwa mujibu wa sheria,” alisema. Habari kutoka ndani ya CC ya CCM zinasema chama hicho kimeipa kazi kamati ambayo ilitumika kuandaa mapendekezo yake awali, kupitia rasimu hiyo na kufanya ulinganisho wa yale ambayo chama hicho kilipendekeza dhidi ya yale yaliyozingatiwa katika Rasimu ya Katiba hiyo.
“Kamati itafanya ulinganisho na baada ya hapo tutakwenda kwa wanachama kuwaeleza ni yapi tulipendekeza kama chama na ni yapi ambayo Tume imeyazingatia na hapo tutapata mawazo yao ambayo tutayatumia katika ngazi ya mabaraza ya Katiba,” kilisema chanzo chetu.

CHANZO: Mwananchi
Wakuu CCM kama CUF, TLP na Tadea wana haki ya kuwa na maoni yao kuhusu katiba, lakini ni lazima pia CCM itambue kuwa haina haki ya kulazimisha maoni yake yawe maoni ya watanzania, na isitake kutafuta nafasi ya kuwa mwamuzi wa mwelekeo wa katiba mpya. Tunatakiwa kuzingatia mao mengi kuhusu katiba, ikiwa nia pamoja na hali ya katiba wakati CCM si chama tawala, na CUF si mtawala mwenza.

Hata hivyo ingekuwa ni vizuri sana kama katiba mpya ingeeleza kuhusu insitution za serikali ya Tanzania bara, kama vile Bunge, mahakama zake na namna ya kuipata serikali yake. Iwekewe wazi serikali ya Tanzania bara itaongozwa na nani, Rais, waziri Mkuu??atakaa magogoni? na ieleze wazi huyo atakayekuwa rais wa jamhuri ya Muungano atakaa wapi. Ofisi zake zitakuwa wapi. Ni kama kazi ya katiba ni ya kulipua kidogo.

Sheria ya usalama wa taifa ni muhimu sana, inatakiwa kuwekwa wazi zaidi na majukumu yake yajulikane zaidi. Isiwe kama ya sasa inayosema maslahi ya CCM ndio mslahi ya taifa, hata kama Chama kimeharibika kama kilivyo sasa.
 
Forum statistics

Threads 1,272,635
Members 490,036
Posts 30,455,626