CCM wanazalisha mdudu mbaya sana atakaewamiwa wenyewe baadaye

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Wameikataa katiba mpya, wanafurahia makada wao kuteuliwa nafasi za ukuu wa mikoa, ukuu wa wilaya,Ukatibu tawala, ukurugenzi na nafasi zingine ambazo kiuhalisia ni mzigo mzito kwa taifa maskini kama letu.

Kwa hali hii wasitehemee kuliongoza taifa hili milele, iko siku wengine watashika usukani na nafasi zote pamoja na vyeo vyake vitakuwepo.Itakapofikia wakati wa wao CCM kuwekwa kando na wengine kuteuliwa hali inaweza kua mbaya sana kwa waluozoea vyeo.Sijui kama CCM watafirahia wapinzani wao kuteua makada wao kushika nafasi mbali mbali ikiwa ni pamoja na wakurugenzi wa halmashauri ambao kwa kiasi kikubwa hulaimiwa kukibeba chama wakati wa uchaguzi.


Kwakua wananadhani katiba mpya ni kwa maslahi ya wapinzani wasubiri siku watakapowekwa kando na katiba hii iendelee kutumika ili nao wauone uchungu wake, ndipo watakapojua kua kupigania maslahi ya taifa ni bora kuliko maslahi binafsi.Watajutia matendo yao ya sasa yatakayokua na maumivu makali kwa vizazi vyao.


Ikumbukwe kua vyama vingi vya ukombozi mahali popote dunidniuumaisha yake sio marefu sana, watu wamevichoka vyama vikongwe wanatamani kuona vionjo vipya! Tatizo lililopo kwenye vyama vya upinzani ni kuzidiwa mbinu kidogo na chama tawala ikiwa ni pamoja na kiobaadhi ya vyombo vya dolail kukibeba, kilichobaki hivi sasa chama jina halijiuzi,halitamkiki mdomoni, kimebaki kubebwa na jina la mtu moja moja badala ya jina la chama chenyewe.Kama ni muda wa kuondoka kwa chama tawala uhai wake kwa sasa hata miaka 20 hauwezi kufika na itafikia mahali hata vyombo vya dola vitasimamia haki.


Kuna mtu moja mzee kabisa wa makamo aliwahi kuniambia kua "Unavyowaona vijana wote ndani ya chama tawala hawana misimamo wana ndimi mbili, wao hutazama upepo wa maslahi na wanakimbilia chama tawala kujijengea uzoefu kiasi kwamba mambo yakiharibika wanatimkia upinzani ambapo kwa uzoefu watakaojijengea watapokelewa na kupewa vyeo vile vile, na pia wale wenye chama tawala nyoyoni mwao ni wachache sana"


Kwahiyo kuendelea kukumbatia mifumo kandamizi isiyoendana wakati kwa kutumika katiba ya zamani kunaweza kuzua vurugu hapo baadae pale ambapo anayemkandamiza mwenzake kwa sasa atakapotolewa madarakani atadhani kua naye anakandamizwa.Tungeweza kuliokoa taifa letu kwa kujenga au kutengeza katiba imara ambayo haitoathiriwa na mabadiliko yeyote ya kisiasa.Katiba iliyojaa misingi imara ya uzalendo na isiyo na chembe hata moja ya hisiaza uonevu kuliko ulivyo hivi sasa.
 
Katiba mpya Kwa TZ kwa sasa sio ya lazima, cha msingi ni good practices n Good Governance. Hatahivyo, kuinua uchumi Wa Watz ni suala la muhimu zaidi. Watu wawe na economic power, waweze kununua, kufanya choices mbalimbali Za mahitaji yao, huduma mbalimbali mzuri wazipate pale wanapohitaji. Kule Libya Gadafi walimuua bure tu
 
We need Economic Development not only Growrh
pole..hata nchi zilizofanikiwa kiuchumi ziliongozwa na katiba ambayo ilikuwa ina miongozo na dira nzuri ya kutekeleza huo uchumi endelevu..sio jukumu la mtu mmoja kuamua mustakabali wa maendeleo...ni mchakato shirikishi ambao unahusisha "wadau wote" wa maendeleo...Tatizo wengi hatujui katiba ni nini...hatujui inagusaje maisga binafsi 6a mtu mmoja mmoja!
 
Uchaguzi mkuu uliopita mimi nilitofautiana kidogo na Chadema, pale waliposema kuwa wangeliweza kushinda uchaguzi kwa sheria hizihizi za Uchaguzi na Katiba hiihii ya kale. Inaonekana kuwa wanaamini hivyo bado kwa kuwa sijaonana wakiweka mkakati wa kudai Katiba mpya. Suala la Katiba mpya ni kete kubwa sana ya CCM na msidhani kuwa wataibadilisha. Kubadilisha sheria ya uchaguzi na kuunda tume huru ya uchaguzi ni sawa na kunywa sumu na mwenye akili hawezi kufanya hivyo. Bila mabadiliko hayo, Upinzani msahau kabisa kushinda na kuingia ikulu. Mtaendelea kuota ndoto tu!!!
 
Vyama vya upinzani na chama tawala wanatuchezea sana watanzania hawa ni wanafki sana hawafanyi siasa za kueleweka
 
Back
Top Bottom