CCM wanatumia mbinu ya negotiation ya machinga wa Kariakoo

CCM wanatumia mbinu ya negotiation ya machinga wa Kariakoo

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,635
Reaction score
6,529
Mnisamehe kwa title ila ukishansoma vizuri utanielewa.

Naamini baadhi yenu mmeshawahi ku negotiate bei ya kitu fulani kutoka kwa wachuuzi wa Kariakoo au sehemu zingine au hata wale wanaouza bidhaa zao barabarani. Au labda hata wewe umewahi kuitumia wakati unauza kitu fulani. Kuna mbinu hii kitaalamu inaitwa 'positional bargaining'.

Mbinu hii inayotumika sana kwenye mauzo ya namna hii ni kwa muuzaji kuanza na bei ya juu kuliko uhalisia, kwa lugha nyingine ni from an extreme position. Wakati huo huo ukikutana na mnunuaji anayejielewa na yeye atataja bei yake iliyo chini kuliko uhalisia. Mambo yakienda sawasawa na wote wawili wakiwa na nia kabisa ya kufunga dili, hatimaye watafikia makubaliano ya bei ambayo ipo katikati na wote wataondoka wakiwa wameridhika.

Katika masuala ya Katiba na mabadiliko mbalimbali ya kisiasa ikiwemo sheria za Uchaguzi, CCM ni muuzaji. Sisi wananchi kama wanunuzi tumeitamkia bei wakati ule wa rasimu ya Warioba, unaweza kusema chini kuliko uhalisia (kwa mtazamo wao wanaona ni hivyo kwa sababu ilikuwa inatishia hali waliyozoea na kuitegemea).

Baada ya kutafakari CCM wamekuja na bei yao. Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema wame 'double down' ambayo ni juu kuliko uhalisia. Huyu muuzaji, CCM, anasema kwanza hata kuuza kwenyewe hataki, pamoja na kwamba unaona vumbi limemjaa hadi utosini na hajala siku mbili.

Kwa mliowahi kukumbana na muuzaji wa namna hii ulifanya nini hadi akakubaliana na bei uliyomtajia au at least iliyokuwa nafuu kwako ukachukua mzigo?
 
mwenye chake akikuambia hauzi achana naye fuata mambo yako kwani lazima akuuzie?
 
Maelezo mazuri ila naona kama mfano haupo sawa.. Wauzaji ni wananchi maana ndo hasa wenye mali. Hawa wanunuzi sisiemu wanajaribu kutapeli kwa hila nyingi. Wenye mali wasiposhtuka watabaki na manyoya mkononi
 
Maelezo mazuri ila naona kama mfano haupo sawa.. Wauzaji ni wananchi maana ndo hasa wenye mali. Hawa wanunuzi sisiemu wanajaribu kutapeli kwa hila nyingi. Wenye mali wasiposhtuka watabaki na manyoya mkononi

Unaweza kuliangalia kwa mtazamo huo. Na mimi wakati naandika nililiangalia pia hivyo na bado ujumbe ukawa ule ule.

Cha msingi ni kuwa CCM wanatumia hii negotiation tactic na ni muhimu kwa wale wanaodai mabadiliko fulani walielewe hilo, litawasaidia kujua ni mbinu gani za kutumia kupata kile wanachotaka. Bila kuwa na uelewa huo, huyu muuzaji (au mnunuzi kulingana na unavyoliangalia hili) ataendelea kuringa na kudengua na muda unakwenda.

Cha msingi ni kujua kuwa negotiation za namna hii lazima kuwe na compromise, bahati mbaya hauwezi kupata 100%.
 
Unaonyesha kuna options zingine kisha Unaonyesha kua unataka kuondoka.
 
Unaonyesha kuna options zingine kisha Unaonyesha kua unataka kuondoka.

Hiyo ni njia moja wapo na ni kweli inafanikiwaga. Sasa iapply kwenye situation hii ya mabadiliko ya kisiasa inaweza kutoa mbinu mbadala. Siyo lazima utuambie hapa usije ukaunganishwa na kesi ya Zitto!!

Wengine tuendelee kufundishana. Mbinu gani mnazitumiaga kuwalalia wamachinga?
 
Pitieni huu uzi unaweza kuwasaidia
 
Back
Top Bottom