spiritual hero
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 354
- 64
Kila mara ccm wanapokomalia jambo huwa lina maslahi kwao hii tunatambua na tumeshawazoea. Safari hii kama kweli wameamua kulihodhi bunge la katiba kwa hila kama kawaida yao basi tuwe na uhakika kuwa watapitisha katiba yao huku wakijipanga kutudhibiti pale tutakapoamua kudai haki yetu. Hii ni kama kutuchimbia kaburi sisi wananchi maana watatuua kifikra, na kimwili pia. Hila walizofanya kwenye mdahalo wa juzi walipoandaa makada-njaa wao ili waje kuzomea watetezi wa katiba ya wananchi, wenye akili timamu wamebaini. Na mpaka sasa bado tunaunga mkono UKAWA wasirudi bungeni. Kwani kuna ugumu gani kukubali tu kujadili maoni ya wananchi? Ina maana safari hii mawazo ya ziada ndio yana umuhimu zaidi ya mawazo makuu. Hawa watu hata jina la interahamwe halijafikia kiwango cha uovu wao. Hawa ni mazombi kabisa. Wanitafute na mimi waniue waninywe damu ili watanzania wenzangu wapone.