CCM wanatengeneza vitambulisho feki

CCM wanatengeneza vitambulisho feki

chikuyu

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2013
Posts
277
Reaction score
179
CCM WANATENGENEZA VITAMBULISHO FEKI.

Na Musa Makongoro.
Baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wanashirikiana na wagombea wa CCM, kutengeneza vitambulisho feki vya kupigia kura.

Pia Wanafunzi wa shule za sekondari hasa katika mikoa ambayo UKAWA ina nguvu, wanaandikishwa namba za vitambulisho vyao na wengine wanapewa shilingi 5,000 mpaka 10,000 ili kutoa vitambulisho vyao.
Mfano jijini Dar Es Salaam, Saa moja usiku ya tarehe 20.10.2015, kijana aliyefahamika kwa majina Hamidu Hussein(27),kutoka kitengo cha uhamasishaji, UVCCM, jimbo la Ilala, amekutwa anachukua majina ya wanafunzi wanaosoma shule ya sekondari ya Tambaza,iliyopo wilaya ya Ilala, jijini Dar Es Salaam.
Mmoja wa wanafunzi(jina linahifadhiwa) aliyekataa kutoa kitambulisho chake, amesema kwamba kazi hiyo hufanywa usiku shuleni hapo, na kwenye nyumba za walimu wasiowaaminifu.
"Walikuja hapa(Tambaza) hata jana wakachukua majina na namba za baadhi yetu, na kutoa shilingi 5000 na wengine wabishi walipewa shilingi 10,000". Alisema mwanafunzi huyo aliyeomba kujitambulisha kwa jina moja la Amos.
''Shule mbalimbali zikiwemo baadhi ya shule za jimbo la Ukonga, pia hawa wameenda huko''. Aliongeza.
Mwalimu mkuu wa shule ya Tambaza, ambaye hakutaka kuandikwa hadharani, amekili kutokea kwa suala hilo na kusema kwamba wanalishughulikia.
Nae mmoja wa wanafamilia wa mwalimu Kelani Hujulwa,shule ya Sekondari Ukonga, amekili kuona wanafunzi wakiandikishwa nyumbani kwa kaka yake,muda wa usiku.
''Kuna wanafunzi huandikwa hapa usiku majina na vitambulisho vyao na wakati mwingine naona pia polisi wapo hapa wanazunguka, na huwa wanatumia gari nyeusi kuingia hapa''.
Mwandishi wa habari hizi aliweka kambi katika maeneo ya nyumba hiyo iliyopo eneo la Banana, yenye geti la rangi myeusi na kushuhudia mchezo huo,ambao unahusisha polisi waliovalia sare ya jeshi la polisi na wanafunzi ambao wanaingia nyumbani hapo wakiwa katika gari nyeusi aina ya prado,yenye namba T 456 AZP. Katika kuweka kambi hapo mwandishi ameweza kubaini kwamba gari hiyo, huingiza wanafunzi angalau mara mbili, na zoezi hilo hufanywa haraka haraka.
Uchunguzi unaonyesha kwamba viongozi wa CCM, wanashirikina na baadhi ya walimu wakuu, kupata wapiga kura feki, baada ya kugundua mchezo wa kupitisha kura zilizopigwa utakuwa mgumu zaidi kila kona ya nchi.
Mkakati wa kuwatumia wanafunzi umelengwa angalau kupata wanafunzi ambao ni wapiga kura feki 150 kutoka kila shule.
Kura hizi ni kwa ajili ya nafasi ya urais katika eneo husika.
Mmoja wa walimu kutoka shule ya sekondari Jitegemee,jijini Dar Es Salaam, anabainisha kwamba, mchezo huo unaratibiwa na baadhi ya walimu wakuu wa shule na wagombea wa CCM.
"Kuna posho wakubwa wetu wamepewa na pia wameambiwa wakiokoe chama kwa kutoa angalau wanafunzi 150 wasaidie kuongeza kura".
Wanafunzi hao ni ambao watatengenezewa vitambulisho feki,na kwamba, siku ya kupiga kura wanaweza kupiga kura katika maeneo mawili tofauti kwenye vituo vya kupigia kura.
 
Hata Dodoma haki iko hivyohivyo,mgombea ubunge anahaha kujinasua kwenye kibano cha kigaira ,kuna vijana wamekamatwa kata ya Ihumwa wakinakili namba za vitambulisho ili wafoji vitambulisho,hatahivyo vijana hao wamekamatwa na polisi
 
Kamata,piga kibomatch + petrol +general tyre
 
CCM na serikali watasababisha machafuko mwaka huu.
 
hawatashindana n nguvu ya MUNGU,,,machozi,,,,damu na vilio vya askini havitawaacha salama
 
CCM WANATENGENEZA VITAMBULISHO FEKI.

Na Musa Makongoro.
Baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wanashirikiana na wagombea wa CCM, kutengeneza vitambulisho feki vya kupigia kura.

Nae mmoja wa wanafamilia wa mwalimu Kelani Hujulwa,shule ya Sekondari Ukonga, amekili kuona wanafunzi wakiandikishwa nyumbani kwa kaka yake,muda wa usiku.
''Kuna wanafunzi huandikwa hapa usiku majina na vitambulisho vyao na wakati mwingine naona pia polisi wapo hapa wanazunguka, na huwa wanatumia gari nyeusi kuingia hapa''.
Mwandishi wa habari hizi aliweka kambi katika maeneo ya nyumba hiyo iliyopo eneo la Banana, yenye geti la rangi myeusi na kushuhudia mchezo huo,ambao unahusisha polisi waliovalia sare ya jeshi la polisi na wanafunzi ambao wanaingia nyumbani hapo wakiwa katika gari nyeusi aina ya prado,yenye namba T 456 AZP. Katika kuweka kambi hapo mwandishi ameweza kubaini kwamba gari hiyo, huingiza wanafunzi angalau mara mbili, na zoezi hilo hufanywa haraka haraka.
Uchunguzi unaonyesha kwamba viongozi wa CCM, wanashirikina na baadhi ya walimu wakuu, kupata wapiga kura feki, baada ya kugundua mchezo wa kupitisha kura zilizopigwa utakuwa mgumu zaidi kila kona ya nchi.
Mkakati wa kuwatumia wanafunzi umelengwa angalau kupata wanafunzi ambao ni wapiga kura feki 150 kutoka kila shule.
Kura hizi ni kwa ajili ya nafasi ya urais katika eneo husika.
Mmoja wa walimu kutoka shule ya sekondari Jitegemee,jijini Dar Es Salaam, anabainisha kwamba, mchezo huo unaratibiwa na baadhi ya walimu wakuu wa shule na wagombea wa CCM.
"Kuna posho wakubwa wetu wamepewa na pia wameambiwa wakiokoe chama kwa kutoa angalau wanafunzi 150 wasaidie kuongeza kura".
Wanafunzi hao ni ambao watatengenezewa vitambulisho feki,na kwamba, siku ya kupiga kura wanaweza kupiga kura katika maeneo mawili tofauti kwenye vituo vya kupigia kura.

CC Mzee Mwanakijiji hii ndiyo chama ambacho umekwenda mpaka nyumbani kwa Mzee Mwinyi Raisi mstaafu kumuomba ampigie chapuo Magufuli na chama kinachokwenda kwenye historia hapo 25.10.2015 kuwa ilikuwa madarakani na kuleta uhuru na sasa ni chama cha upinzani Tanzania?
Kweli Mungu akitaka kumvua biandamu nguo huwa hachagui siku-akifurahi tu hutoa zawadi.

Habari ndiyo hii-Lumumba wako hoi!

Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom