CCM wanajitapa kwa lipi?

CCM wanajitapa kwa lipi?

kubenafrank

Member
Joined
Aug 14, 2011
Posts
82
Reaction score
22
Katika taarifa ya habari ya jana saa mbili usiku katika Star Tv, mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi alijitapa kuwa ifikapo mwakani wataajiri walimu 25000 nchi nzima wa shule za msingi na sekondari.Aliendelea kujitapa kuwa walimu hao watalipwa na serikali ya ccm.Ni lini watumishi wa umma walishawahi kulipwa mishahara na ccm?na ni lini ccm walisha ajiri wafanyakazi na kuwafanya kuwa watumishi wa umma? Nijuavyo, watumishi wote wa umma wanalipwa na kodi ya wananchi na si fedha za ccm kama alivyokuwa akijitapa huyo mwenyekiti wa wazazi ccm.Wahenga walisema "Siku ya kifo cha Nyani miti yote huteleza."Huu ni uwongo ambao haufai katika majukwaa ya siasa.
 
Back
Top Bottom