CCM wanajichimbia kaburi Zanzibar

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
2,149
1,717
Mpaka sasa wazanzibar wote wameshakuwa na hasira ya 1) Kutokuthaminiwa uhuru wao wa maoni 2) Kudharaulika ndani ya muungano kwani mpaka sasa serikali mpaka kwenye bunge wameshafanya karibu mambo yote bila kujali kama Zanzibar ina serikali ama la. 3) Kukandamizwa na vyombo vya dola.

Sasa kutokana na hayo inaonesha kabisa wazanzibar wanaenda kupiga kura za hasira ili kuiondoa CCM madarakani kwa nguvu zote na ihakikishe kwamba inarejesha uhuru wake na thamani ya raia wa Zanzibar. Na kwa hasira za wazanzibar kwa sasa sina hakika kama amani itaendelea kuwepo kama CCM itajaribu kuhodhi machaguo ya wananchi.

Kwa ufupi CCM imefanya kosa kubwa la kihistoria bila kufikiri na pasipo kujua. Imewapa wazanzibar sababu ya kuungana kwa pamoja kupigania uzanzibar wao and believe me wazanzibar sasa ni wamoja kuliko mda wowote ule. Na ni suala la mda tu. Baada ya miezi 4 au 5 kutoka sasa CCM zanzibar itakuwa ndani ya lile jumba la makumbusho pale forodhani.
 
Chama cha kikomunisti ccm
Knadhani mbilingembilinge ndio mbinu ya kisiasa
Itafika mahali ccm mtakwama
Cut kupata maji.mbo 9 unguja mjiandae kuyaona yakiongezeka
Wazanzibar sio nyumbu mnaowatesa bara
 
Wangeacha kufanya tu huo uchaguzi... Mbona maisha yanaenda tu bila wawakilishi, mawazir?
 
Unatarajia mshinde kwa Tume hiyo hiyo ya Jecha?

Jiulize ni kwa nini uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015 na waangalizi wote wa ndani na nje ya nchi wakatoa taarifa zao kuwa uchaguzi ule ulikuwa huru na haki na bado huyo Jecha akaufuta kwa madai ya kuwa ulikuwa na kasoro chungu nzima?

Fahamu kuwa hata wakazi wote wa Zanzibar hiyo tarehe mpya ya uchaguzi 20/03/2016 aliyoitangaza huyo Jecha, kama wataamua kumpigia kura mgombea wa upinzani, bado mgombea huyo wa upinzani hataweza kutangazwa mshindi, kwa kuwa tuliyaona mabango yao CCM kwenye sikukuu ya Mapinduzi yakisomeka Chotara Hizbu Zanzibar ni ya Waafrika pekee!

Hiyo kwa tafsiri nyingine ni kuwa Sisiem walikuwa wanatekeleza 'slogan' yao inayosema Zanzibar haiwezi kutolewa kwa vijikaratasi vya kupigia kura.
 
Na huo ndo utakuwa mwanzo wa machafuko ambayo hayajapata kutokea Zanzibar. We unataka kuaminisha kwamba ccm Zanzibar wana nguvu? CCM haijawahi kuwa na nguvu Zanzibar hata mara moja. Miaka yote wameshinda kwa wizi na inajulikana wazi. Ila sasa wamefika ukingoni. Naomba uhifadhi unabii wangu baada ya miezi 4 turudi kujadili hali ya CCM Zanzibar
 
tena prpaganda za Kisonge. Hakuna kurejewa kwa uchaguzi.Wamesema hakuna kampeni lakini Alhaj Bulebo na CCM Tanganyika inapiga kambi Zanzibar, ya nini?
 
Ndio maana mwaka huu mvua inaleta shida, njaa baadhi ya mikoa, hii ni laana kwa kuongozwa Na CCM
 
Mpaka sasa wazanzibar wote wameshakuwa na hasira ya 1) Kutokuthaminiwa uhuru wao wa maoni 2) Kudharaulika ndani ya muungano kwani mpaka sasa serikali mpaka kwenye bunge wameshafanya karibu mambo yote bila kujali kama Zanzibar ina serikali ama la. 3) Kukandamizwa na vyombo vya dola.

Sasa kutokana na hayo inaonesha kabisa wazanzibar wanaenda kupiga kura za hasira ili kuiondoa CCM madarakani kwa nguvu zote na ihakikishe kwamba inarejesha uhuru wake na thamani ya raia wa Zanzibar. Na kwa hasira za wazanzibar kwa sasa sina hakika kama amani itaendelea kuwepo kama CCM itajaribu kuhodhi machaguo ya wananchi.

Kwa ufupi CCM imefanya kosa kubwa la kihistoria bila kufikiri na pasipo kujua. Imewapa wazanzibar sababu ya kuungana kwa pamoja kupigania uzanzibar wao and believe me wazanzibar sasa ni wamoja kuliko mda wowote ule. Na ni suala la mda tu. Baada ya miezi 4 au 5 kutoka sasa CCM zanzibar itakuwa ndani ya lile jumba la makumbusho pale forodhani.
Nadhani hilo la kuing'oa ccm lingewezekana kama vyama vya upinzani
vingekubali kurudia uchaguzi na kuwahamasisha
wananchi kuonyesha hasira zao kupitia sanduku
lakini kwa mtaji huu wa kususia uchaguzi japo ni wa kulazimisha sisiemu watapata
vya kunyonga kama kawaida yao.
 
CCM wanajua kwamba watacheza faulo ili washinde na ndio ilikuwa njama yao ya tangu mwanzo, ila kwa sasa upinzani washiriki ama wasusie bado CCm ana hali ngumu sana. Kuna harufu ya machafuko makubwa Zanzibar
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom