Ccm wamsukia zengwe millya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm wamsukia zengwe millya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jodoki Kalimilo, Apr 22, 2012.

 1. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,621
  Likes Received: 2,042
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]KWENYE SIASA WATU WAZIMA WANAKUWA KAMA WATOTO SOMETIMES MAANA HAPO CHINI INANIKUMBUSHA ENZI ZILE ZA MTOTO MWENZAKO UKIGOMBANA NAE MABAYA YOTE ANAYAWEKA WAZI ENZI ZILE MULIPOKUWA NA AMANI, SASA HAPA MIAKA IMEPIATA MINNE NA WAMESUBIRI JAMAA AMETIMKA NDIO WANASEMA, KWA WATU MAKINI UVCCM ARUSHA WAMECHEMSHA WAMEONYESHA NI WANAFIKI NA HAWANA UWEZO WA KUKEMEA MAOVU MAANA KAMA MWENYEKITI WAO HAKUITISHA VIKAO KUNA TARATIBU ZA KUMWAJIBISHA NA SI KUMSUBIRI MPAKA AONDOKE NDIO MSEME "HIZI NI SIZITAKI MBICHI HIZI"
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 20 April 2012 22:35 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya

  Waandishi Wetu
  SIKU chache baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya kujiondoa kwenye chama hicho akifuatiwa na wimbi kubwa la makada na viongozi mkoani humo, CCM kimeanza kumsukia zengwe.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa CCM Mkoa wa Arusha kina mpango wa kumfikisha mahakamani Ole Millya kwa ubadhirifu ndani ya chama ikiwamo madai ya kuondoka na Sh2 milioni za UVCCM zilizoelezwa kuwa zililenga kuanzisha Saccos ya vijana.

  Fedha hizo zinadaiwa kutolewa na waliokuwa wabunge katika majimbo mawili tofauti; Arusha Mjini, Felix Mrema na Arumeru Magharibi, Elisa Mollel mwaka 2008.

  CCM pia kinadai kuwa Millya hajakabidhi taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita inayokadiriwa kufikia Sh600milioni.

  Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa anayewakilisha Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na Mjumbe wa Baraza la Vijana Mkoa wa Arusha, Kennedy Mpumilwa, walimpiga vijembe Ole Millya.

  Gambo alimwelekezea Ole Millya kama msumari uliokuwa unatoboa tairi, akimaanisha CCM.

  “Kwa ujumla vijana Arusha tumefurahishwa na kitendo cha Ole Millya kuhama kwani alikuwa akikidhoofisha chama badala ya kukijenga. Alianzisha vurugu zilizosababisha mpasuko mkubwa mkoani Arusha. Alikuwa msumari uliokuwa unatoboa tairi la gari letu na kusababisha lipate pancha," alisema Gambo
  Alisema Ole Millya na wengine waliotangaza kujivua uanachama wa CCM na kujiunga Chadema ni magamba dagaa ambao wanapalilia njia kwa
  magamba wakubwa kufuata.

  “Tutamdai yeye akiwa hai au mfu na asipolipa tutaendelea kudai watoto wake hadi wajukuu,” alisema Gambo.

  Akijibu swali kwa nini wanajitokeza kudai fedha hizo karibu miaka sita sasa tangu zitolewe, hasa kipindi hiki ambacho Ole Millya amejitoa CCM na kuhamia Chadema, Gambo alidai mara nyingi vikao vya kuzungumzia suala hilo vimekuwa vikivunjika bila muafaka kupatikana kutokana na vurugu zilizokuwa zikianzishwa na wapambe wake.

  Kwa upande wake, Mpumilwa alidai kuwa Ole Millya ameondoka bila kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya zaidi ya Sh600 milioni zilizotokana na kodi ya pango la vyumba 96 vya biashara vinavyomilikiwa na UVCCM.

  Akizungumzia tuhuma hizo, Ole Millya alisema ni dalili za kuanza kuchanganyikiwa kwani kwa uwezo wake kiuchumi, hawezi kuchukua hata senti moja ya chama akisema kinyume chake, alikuwa akitumia fedha zake binafsi kutekeleza baadhi ya majukumu ya kukijenga CCM.

  “Lakini jambo kubwa la kujiuliza ni je, fedha za jumuiya zinapokewa na kuhifadhiwa na Mwenyekiti? Je, Mwenyekiti ni 'returning officer' wa UVCCM hadi mimi nihojiwe kuhusu fedha za mapato na matumizi ya Jumuiya?” alihoji Ole Millya.

  Wakati viongozi na wana CCM hao mkoani Arusha na wengine wa ngazi ya kitaifa wakimponda Ole Millya kwa madai kwamba alikuwa mzigo au gamba, tayari watu kadhaa wametangaza kujitoa katika chama hicho tawala na kujiunga na Chadema
  kumuunga mkono mwenyekiti huyo wa zamani wa UVCCM.

  Siku moja baada ya kuondoka, alifuatiwa na Katibu wa Uhamasishji wa UVCCM Wilaya ya Longido na juzi, wenyeviti watano wa vitongoji na wanachama 2,402 wa CCM wilayani Ngorongoro walikihama chama hicho tawala.

  Makada wengine waliotangaza kukihama chama hicho juzi ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Monduli, Julius Kalanga na Diwani wa Kata ya Nyampulukano, Sengerema, mkoani Mwanza, Hamis Mwagoa.

  Mbali ya hao wapya kujiondoa CCM wametokea jimboni kwa Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja ambako wanaCCM 83 wa Tawi la Igalagalilo, Kata ya Kasungamile wametangaza kuhamia Chadema.

  Katibu wa Chadema jimbo la Sengerema ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana Taifa, Rafiki Rufunga alisema kuhama huko kunatokana na Serikali ya CCM kushindwa kutatua kero zinazowakabili wananchi.


  Habari hii imeandikwa na Salum Maige, Sengerema na Peter Saramba, Arusha[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. e

  ezelina Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona hayo magamba yanadaiwa pesa nyingi sana na watanzania, na walikua wapi kumdai siku Ole Millya sik zote mpaka wamesubiri ahamie CDM. KWELI MFA MAJI.............
   
 3. Sorrow to Joy

  Sorrow to Joy JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 293
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mapato na matumizi yanashughulikiwa na Katibu na si mwenyekiti hao watakuwa mazuzu. Katibu ndiye mtendaji mkuu hawa vipi?
   
Loading...