CCM wampiga STOP Lowassa Arumeru, Yeye asisitiza anakwenda kukampeni... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wampiga STOP Lowassa Arumeru, Yeye asisitiza anakwenda kukampeni...

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by bibikuku, Mar 25, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Lowassa aigawa CCM Arusha

  ADAIWA KUPIGWA 'STOP' ASISHIRIKI,ASEMA NI UZUSHI WA KIPUUZI, CHADEMA WALIA
  Waandishi Wetu, Arumeru na Dar

  USHIRIKI wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge Arumeru Mashariki unadaiwa kuigawa timu ya kampeni ya CCM inayomnadi mgombea wa chama hicho, Sioi Sumari.Lowassa ambaye yuko mkoani Arusha tangu Machi 20, mwaka huu, amekuwa akitajwa kwamba atamnadi Sioi lakini tofauti na makada wengine, hadi sasa hakuna ratiba yoyote ndani ya CCM inayoonyesha ni lini mbunge huyo wa Monduli atapanda jukwaani.

  Habari zilizopatikana jana kutoka Arumeru na Dar es Salaam zinasema baadhi ya viongozi wa CCM na timu inayoongoza kampeni za uchaguzi huo wamegawanyika kuhusu Lowassa kupanda jukwaani, huku wengine wakipinga.

  Kumekuwepo na kundi ambalo linaona kwamba Lowassa akiingia kwenye kampeni hizo anaweza kuzua mazingira ambayo yataipa ugumu CCM kushinda kutokana na kumbukumbu kuwa alijiuzulu kutokana na kashfa ya utoaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni tata ya Richmond Development LCC.

  Chadema tayari kimetangaza kuwa endapo Lowassa atajitokeza kwenye kampeni hizo kumnadi mgombea wa CCM, watamuumbua kwa kile wanachodai wataweka hadharani tuhuma kinazodai zinamhusu.

  Jana, mmoja wa viongozi wa chama hicho alisema: “Hatapanda jukwaani (Lowassa), wala hatothubutu kufanya hivyo kwani tayari ameambiwa aache na huyo aliyemwambia nadhani anamsikiliza, hawezi kukiuka.”

  Kauli ya kiongozi huyo inafanana na ile iliyotolewa na mmoja wa makada wakongwe wa CCM anayeshiriki kampeni za Arumeru Mashariki ambaye Machi 20 mwaka huu akiwa Usa River alsikika akisema: "Lowassa hana umuhimu wowote” kwenye kampeni hizo.

  Kiongozi huyo alikuwa akichangia mjadala usio rasmi uliokuwa ukiwahusisha makada kadhaa wakongwe wa CCM, walipokuwa wakisubiri kuanza kwa msafara wa kwenda kwenye moja ya mikutano ya kampeni.

  Lowassa ajibu
  Akizungumza kwa simu kuhusu madai hayo jana, Lowassa aliziita taarifa za kukatazwa kwake kupanda jukwaani kumnadi Sioi kuwa ni “uzushi usiokuwa na msingi.”

  Hata hivyo, hakuwa tayari kuweka bayana aina ya ushiriki wake kwenye kampeni hizo zinazoelekea ukingoni, huku CCM kikikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mahasimu wao Chadema ambacho kimemsimamisha, Joshua Nassari.

  “Kwani kuna nini, hakuna haja ya kuwa na haraka, kwani vyovyote itakavyokuwa mtajua tu,” alisema Lowassa.

  Mapema jana asubuhi alipotafutwa kwa simu, Lowassa alisema asingeweza kuzungumza kwani alikuwa kwenye kikao. “Nipigie majira ya mchana kama saa tisa hivi, maana sasa niko kwenye kikao,” alisema.

  Hata hivyo, watu walio karibu na kiongozi huyo walisema Lowassa atapanda jukwaani kesho na kwamba tayari ameanza kampeni za kumnadi Sioi kwa kufanya vikao vya ndani na kwamba kikao cha jana ni moja ya vikao hivyo.

  “Hizo taarifa kwamba amezuiwa siyo za kweli, mimi nimehakikishiwa kwamba atapanda jukwaani kuanzia Jumapili (kesho) na ninavyofahamu tayari ameanza vikao vya ndani,” alisema mmoja wa watu wa karibu na Lowassa.

  Mwana CCM mwingine aliye karibu na kiongozi huyo alisema: “Ni kweli walikuwa wakihaha kumzuia, eti wandai kwamba ushindi ukipatikana itaonekana kwamba ni mafanikio yake, lakini wameshindwa maana hadi sasa tuna uhakika Mzee (Lowassa) atapanda jukwaani."

  Habari zaidi zinasema kuwa Mratibu wa Kampenzi za CCM katika uchaguzi huo, Mwigulu Nchemba juzi jioni alikutana na Lowassa kuweka mambo sawa kabla ya kiongozi huyo kupanda jukwaani kesho.


  MY TAKE: Hapo nataka kujua nani ataibuka tena mbabe katika vita hii mpya. Ni CCM Lowassa au CCM JK?? Alishinda katika kinyang'anyiro cha kumuweka SIOI, na hapa lazima ashinde tu.
   
 2. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kuchafuka walishazoe,sabuni ya omo,au komoa ipo tutafua nguo,tutapiga pasi kiwalo kitavaliwa kwani shida nini ati?Kwa kuwa toka lini kelele za chura zikamzuia ng'ombe kunywa maji.Hakika CCM kama hawana cha kupoteza chonde chonde wasimpandishe EL,vinginevyo EL ni yule yule alietoka Ifakara kuwaambia Serikali ya CCM imeshindwa kupambana na janga ya ajila ya vijana leo anakwenda kumpigia kampeni kijana wa CCM,ambae kama akishinda ana nafasi kubwa uenda siku zisizo na jina akapata uteuzi wa kuwa naibu waziri wa maendelo ya viiana na kazi.

  Au ni EL mwingine jamani,consider everything is constant based on the UFISADI ISSUES.
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  kwa ukombozi wa Arumeru, nitapenda EL apande jukwaani ili aiukane vizuri serikali na wapiga kura wajue kuwa kumbe CCM haitawasaidia
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ila imekaa very technical vibaya sana kwa kuwa kushindwa kupanda that means URAIS HAUPO,kwa kuwa KAMA UMESHINDWA KUSIMAMIA MASHAMBULIZI YA KUMNYANYUA MKWE WAKO MWENYEWE, SEMBUSE URAIS WA NCHI KUZUNGUKA TANZANIA NZIMA na MICHAKATO YA AWALI NDANI YA CCM MPAKA KUJA KAMPEINI, MTU ATAKUWA NA VIFUNGO VYA SHATI AU NDIO TUMBO WAZI NA TAULO KIUNONI NA WAKWE WAMESIMAMA WAKIOMBA MUNGU UPEPO USITOKEE MANAKE YATAKUWA MENGINE.

  CDM wanasema akipanda Jukwaani kumnadi SIOI, wanampigia muziki hasa ule wimbo wa Msondo unaitwa nini vileeee !!!!!!! ehhhh eti nimekumbuka unaitwa MAMBO HADHARANI, RIP TX-Moshi, na wenzie wana msondo waliotangulia mbele ya haki.
   
 5. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  kweli EL ana mtihani mkubwa, mbele kiza, nyuma kuna shimo
   
 6. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Na sasa alishawatukana akawaambia HAWAFANYI MAAMUZI MAGUMU,sasa MAAMUZI MAGUMU NI "USIPANDE JUKWAANI KWA KUWA HALI YAKO YA KISIASA NI TATA,KWA FAIDA YA MTU ALIYEKUOLEA MTOTO WAKO AKA MKWE WAKO AU UPANDE WEWE KUMTETEA AKOSE YEYE HUYO MKWEWE WAKO [SIOI], NA UKIPANDA AKAKOSA NAWE PIA UCHAFUKE NA UTUCHAFUE CHAMA MPAKA UWEZO WA JIKI KUKUKOSHA NA KUTUKOSHA UWE HAUPO UNASEMAJE SIGN HAPA.Mhhhhhhhh sipati picha!.

  Msanii wa kizazi kipya Fid Q aka Ngosha the Don anasema chagua moja kusuka ua kunyoa!!!!!!!!!!!!!!.Anasikia utaaaaaaam.
   
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Lowassa hana umuhimu wowote ndio maana hata kwenye ratiba hayumo,sema yeye anaguswa na uchaguzi huo kwa kuwa ana uhusiano na mgombea wa ccm ambae mkwewe hivyo anaona itakuwa si vema kukaa pembeni ndio maana kaomba apewe nafasi,lakini chama kama chama kilishajipanga siku nyingi kwa kuwateua makada wake ambao kimeona wanafaa kwa project ya arumeru,Chama kisingeweza ku risk kumpanga Lowassa kuwa ni mmoja wa makada watakaoendesha official kampeni za kichama kwa kuwa kina kumbukumbu mbaya dhidi ya ushiriki wake kwenye jimbo la arusha mjini kwenye uchaguzi mkuu uliopita ambapo yeye ndio alisababisha ccm kushindwa arusha mjini na chadema kutokana na yeye kuachiwa asimamie kampeni za mgombea wa ccm kama alivyong'ang'ania..
   
 8. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Kwa jinsi ninavyowafahamu CCM pamoja na Lowasa wao hakuna mtu anayeweza kumzuia, na siku zote Lowasa amekuwa akifanya mambo yake kwa kutumia akili saana, physically inaweza ikaonekana Lowasa hayupo Arumeru lakini, hiyo haimaanishi kuwa he is not participating katika mchakato wa kampeni. Najua mpaka sasa kuna vijana wake kama kina Millya, Kadogo diwani wa Monduli, Sanare na wengine wengi, lakini pia kutokana na mtandao wake tayali anajua upepo unavumaje na kwa hiyo atakuwa ameshaanza kujipanga kivingine kwa kuhakikisha kuwa kwa namna iwayo yoyote ile tume ya uchaguzi imbayo inakuwa chini ya mkurugenzi itamtangaza Sioi. Cha msingi CHADEMA wahakikishe wanajipanga kwa namna ambayo hakutakuwa na upenyo wa kuruhusu ghiliba na uzandiki kufanyika kwa sababu mpaka sasa CCM tayali ishawezwa katika kampeni, muhimu huwa ni namna ya kumalizia mbio na sio ulianzaje.
   
 9. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Kwa jinsi ninavyowafahamu CCM pamoja na Lowasa wao hakuna mtu anayeweza kumzuia, na siku zote Lowasa amekuwa akifanya mambo yake kwa kutumia akili saana, physically inaweza ikaonekana Lowasa hayupo Arumeru lakini, hiyo haimaanishi kuwa he is not participating katika mchakato wa kampeni. Najua mpaka sasa kuna vijana wake kama kina Millya, Kadogo diwani wa Monduli, Sanare na wengine wengi, lakini pia kutokana na mtandao wake tayali anajua upepo unavumaje na kwa hiyo atakuwa ameshaanza kujipanga kivingine kwa kuhakikisha kuwa kwa namna iwayo yoyote ile tume ya uchaguzi imbayo inakuwa chini ya mkurugenzi itamtangaza Sioi. Cha msingi CHADEMA wahakikishe wanajipanga kwa namna ambayo hakutakuwa na upenyo wa kuruhusu ghiliba na uzandiki kufanyika kwa sababu mpaka sasa CCM tayali ishawezwa katika kampeni, muhimu huwa ni namna ya kumalizia mbio na sio ulianzaje.
   
 10. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Jambo kama lipi alilofanya kwa kutumia akili?kuandika vimemo kwa waziri wa nishati na madini wakati ule ili aziache kampuni zenye uwezo wa kufua umeme kiukweli na kuichukua RICHMOND au kutaka kwenda kutununulia mvua ya kichina Thailand?

  Kweli mtu akipenda chongo huita kengeza nimeamini.
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Natamani sana kumsikia mamvi akihutubia
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  bora tu aache mana siku zake za kuishi zitazidi kupunguzwa na makombora atakayorushiwa
   
 13. M

  Matunyengule JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 708
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hivi kwa nini mnamwogopa sana ENL. Mnampandisha chati sana, ni vyema kumruhusu apande ili kusikiliza kama ana jipya lolote.
   
 14. K

  KIMALE New Member

  #14
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanini wapige Lowasa stop?hebu tujiulizeni kuna nini?
   
 15. R

  Ramanengo Member

  #15
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chama cha magamba hakuna wa kumzuia kapteni lowasa kushiriki kampeni za mkwe wake(sioi ) izo ni porojo za nape na wenzake
   
 16. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  wanamuogopa wapambe wake anaowaweka mjini kina peter sio mtu kama mimi.
   
 17. L

  LULENGO Member

  #17
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda aende pale Meru huyo MAMUVI tuone,na ASILOGWE akajiingiza kichwakichwa next presdencial race hakika hatasahau siasa ni nini,yeye akae tu aendelee kula matunda yake ya Richmonduli,na aendelee kuwatawala mayeru wenzake huko monduli basi.
   
 18. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Lowasa gari kubwa hawamuwezi
   
 19. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hahahahah! ngoja niendelee kufuatilia hii zengwe la EL & JK, watu ambao hajakutana barabarani!! Naimani kuna ramani zinachorwa kwa mwendokasi wa mwanga wa jua. Subirini mtakuja shangaa.
   
Loading...