CCM wamejiandaa kukubali matokeo?

CCM wamejiandaa kukubali matokeo?

Muulizeni muone kama atakwepa swali

Tutampata wapi wakati Haonekani kwenye media? Mwenzie ameshafanya interview na TV stations zaidi ya tano ila yeye hajafanya hata moja, ana kazi ya kusema tumwamini hatatuangusha.

Hivi ulisoma makala ya Jenerali Ulimwengu? Kuwa Magufuli alikataa mahojiano na akataka apelekewe Maswali lakini bado hakuyajibu?
 
Swali hapo linatakiwa liwe UKAWA wako tayari kukubali matokeo?
Umeshaambiwa kuwa tayari Lowassa ameeleza bayana alipohojiwa na Zuhura Yunus wa BBC kuwa iwapo atashindwa kwenye uchaguzi wa keshokutwa atarejea Monduli na kufuga ng'ombe wake.

Tunamtaka na Magufuli naye ajitokeze hadharani na kutamka bayana kuwa iwapo kura kwa upande wake hazitatosha hapo keshokutwa atakuwa naye tayari kurejea Chato na kujishughulisha na shughuli za uvuvi.

Iwapo Magufuli atashindwa kujitokeza hadharani na kulitamka hilo basi wananchi tutaamini kuwa CCM ina mpango wa kufunga goli la mkono kwenye uchaguzi wa keshokutwa.
 
Washindanapo fahari wawili ni lazima mmoja atashindwa.

Tayari Lowassa ameonyesha njia, alipohojiwa na BBC alieleza bayana kuwa iwapo atashindwa kwenye uchaguzi wa keshokutwa atarudi Monduli kwenda kufuga ng'ombe wake.

Tunamtaka Magufuli na CCM yake wajitokeze hadharani na wautangazie Umma wa watanzania kuwa iwapo wao nao watashindwa, watayapokea matokeo hayo na kuwa tayari kukabidhi madaraka kwa amani kwa Ukawa.

Iwapo Magufuli 'atagoma' kutamka hadharani kuwa iwapo na yeye atashindwa kwenye sanduku la kura basi atakuwa tayari kuyapokea matokeo, tutaamini kuwa lipo jambo nyuma ya pazia la goli la mkono ambalo maccm wamelipanga.

Itabidi CCM wasikilize ushauri wa busara sana alioutoa Goodluck Jonathan, aliyekuwa Rais wa Nigeria ambaye aliksbidhi madaraka kwa amani kwa mpinzani wake Mohamed Buhari aliyeshinda uchaguzi huo.

Kitendo chochote cha CCM kulazimisha goli la mkono kitaisababishia nchi hii machafuko na wao CVM hawataepuka mkono wa vijana wa Bensouda wa kuburuzwa kupelekwa The Hague kujibu mashitaka ya uhalifu na kusababisha machafuko kwenye nchi hii.

Umesema vyema sana, barikiwa
 
Mkuu, miye sioni sababu ya kuwalazimisha watu kwa kuwauliza maswali kuhusu kukubali au kukataa matokeo. Maana ya neno "matokeo" ya uchaguzi ni kuwa yatakuwa wazi yakionyesha ni nani amepata kura nyingi, sasa hilo la kuktaa matokeo linatoka wapi tena. Nathani taasisi ya kuuliza swali ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa iko tayari kuendesha uchaguzi huru na haki. Hebu fikiria uchaguzi kama utaendeshwa kwa uhuru, uwazi na haki, zikahesabibiwa kwa uwazi na matokeo ya kila kituo kukubaliwa na mawakala wote kuanzia ngazi ya Kata, Majimbo hadi taifa. Sasa huyo atakayekataa matokeo ni nani tena.
 
Tutampata wapi wakati Haonekani kwenye media? Mwenzie ameshafanya interview na TV stations zaidi ya tano ila yeye hajafanya hata moja, ana kazi ya kusema tumwamini hatatuangusha.

Hivi ulisoma makala ya Jenerali Ulimwengu? Kuwa Magufuli alikataa mahojiano na akataka apelekewe Maswali lakini bado hakuyajibu?
Katika kipindi hiki, maswali na majibu yote hufanyika kwenye majukwaa ya kampeni!
Anyways, hujamsikia Magufuli amesema akishindwa atarudi Mwanza kivua samaki??
 
Asiekubali kushndwa si mshindani, na atakayeshinda ndo kapendekezwa na wananchi.
 
Mkuu, miye sioni sababu ya kuwalazimisha watu kwa kuwauliza maswali kuhusu kukubali au kukataa matokeo. Maana ya neno "matokeo" ya uchaguzi ni kuwa yatakuwa wazi yakionyesha ni nani amepata kura nyingi, sasa hilo la kuktaa matokeo linatoka wapi tena. Nathani taasisi ya kuuliza swali ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa iko tayari kuendesha uchaguzi huru na haki. Hebu fikiria uchaguzi kama utaendeshwa kwa uhuru, uwazi na haki, zikahesabibiwa kwa uwazi na matokeo ya kila kituo kukubaliwa na mawakala wote kuanzia ngazi ya Kata, Majimbo hadi taifa. Sasa huyo atakayekataa matokeo ni nani tena.
Lakini lazima ukumbuke kuwa mpambano huu mkali kati ya CCM vs Ukawa ni mpambano baina ya chama cha siasa Chadema/Ukawa na chama dola cha CCM.

Tujikumbushe mkwara mzito alioutoa IGP Mangu jana kuwa ni marufuku wananchi kuwashangilia hata madiwani na wabunge wao walioshinda ambao wasimamizi wa majimbo husika watakuwa wamewatangaza kushinda kwenye majimbo husika, hadi siku ambapo Rais wa awamu ya 5 atakapoapishwa!

Hivi ukiitafakari kauli hiyo ya IGP itakuwa na lengo zuri kweli kwa nchi yetu?

Kwa kuwa umekuwa utaratibu wetu tokea chaguzi za kwanza za mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 Madiwani na Wabunge kushangiliwa baada ya kutangazwa kushinda kwenye maeneo husika, kwa nini iwe TOFAUTI mwaka huu????????????
 
Mi kwa mtazamo wangu naona CCM wamejiandaa kupora ushindi wa UKAWA na si vinginevyo labda dola/jeshi lisimamie ili haki ya ushindi iweze tendeka. Rejea hutuba za JK, ''Tutashinda kwa namna yoyote ile''
 
Kwa kupngezea tu hapo ni kuwa JK alitamka kuwa CCM ni chama kikongwe na kina 'maarifa' mengi ya kushinda.

Hivi ni maarifa yapi hayo mengi ambayo CCM wanayo ambayo JK hakutaka kufafanua zaidi ya kutumia goli la mkono?
 
Swali hapo linatakiwa liwe UKAWA wako tayari kukubali matokeo?

Kwa jinsi wanavyozungumza inaonekana wameshayakataa hata kabla hata kabla kura hazijapigwa!

Wanapiga kura kwa mdomo na kuzihesabu wenyewe, kisha wanazikataa.
 
Umeshaambiwa kuwa tayari Lowassa ameeleza bayana alipohojiwa na Zuhura Yunus wa BBC kuwa iwapo atashindwa kwenye uchaguzi wa keshokutwa atarejea Monduli na kufuga ng'ombe wake.

Tunamtaka na Magufuli naye ajitokeze hadharani na kutamka bayana kuwa iwapo kura kwa upande wake hazitatosha hapo keshokutwa atakuwa naye tayari kurejea Chato na kujishughulisha na shughuli za uvuvi.

Iwapo Magufuli atashindwa kujitokeza hadharani na kulitamka hilo basi wananchi tutaamini kuwa CCM ina mpango wa kufunga goli la mkono kwenye uchaguzi wa keshokutwa.

Lowassa hayo maneno tu, we unadhani akikosa ataenda kweli kukaa kijijini? anapenda starehe yule jamaa mke wake ndo yule anapiga bia hawezi kubali kurudi kijijini, so wote tunajua ni mbwembwe tu, Mapadlock sio mtu wa fujo usidhani akikosa atakaa kulalamika, na watu wa ccm watayakubali matokeo kirahisi tu..

Tatizo ni vijana wa UKAWA, wana fujo sana, ndo walewale wanakaa kusema watalinda kura zao mita 200.. Hivi unadhani mita 200 ni distance ya kusema unasimama afu watu wasiweze kuiba kura? mtu akisimama 200m mbele yako anaweza fanya chochote na usimuone kwa hiyo ni useless, wastage of time, na watu wa ukawa wanapenda ugomvi tu coz wengi wao ni vibaka wa mjini.
 
Nashauri next time ujifunze kusoma na kuelewa kilichoandikwa kuliko kukimbilia kupost, inapunguza heshima na utu

Nimemaanisha vizuri tu nilichokisema, labda kiwe kimekuuma, sio lazima kureply kila post JF, ni social media tu kila mtu ana freedom of expression.
 
WanaJF sijamsikia Magufuli wala kamati ya kampen ya CCM, ikitangaza kuwa iwapo watashindwa, basi watakubaliana na matokeo.

Kama kweli CCM ni chama cha kidemokrasia, tunaomba Magufuli na Kamati yake watangaze kabla ya jumapili kuwa watakubali matokeo iwapo watashindwa.
 
Hilo swali alirushiwa ngombea fulani huko Zanzibar wa chama hicho alikataa kata kata kulijibu nadhani alikuwa anasubiri majibu kutoka Dodoma. Wakati ni huu tupewe majibu!
 
Lakini lazima ukumbuke kuwa mpambano huu mkali kati ya CCM vs Ukawa ni mpambano baina ya chama cha siasa Chadema/Ukawa na chama dola cha CCM.

Tujikumbushe mkwara mzito alioutoa IGP Mangu jana kuwa ni marufuku wananchi kuwashangilia hata madiwani na wabunge wao walioshinda ambao wasimamizi wa majimbo husika watakuwa wamewatangaza kushinda kwenye majimbo husika, hadi siku ambapo Rais wa awamu ya 5 atakapoapishwa!

Hivi ukiitafakari kauli hiyo ya IGP itakuwa na lengo zuri kweli kwa nchi yetu?

Kwa kuwa umekuwa utaratibu wetu tokea chaguzi za kwanza za mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 Madiwani na Wabunge kushangiliwa baada ya kutangazwa kushinda kwenye maeneo husika, kwa nini iwe TOFAUTI mwaka huu????????????
Mkuu hilo ni tatizo la chama tawala kuweka Makada wake katika ngazi nyeti za uongozi kama hizo kwa ajili ya kuwalinda. lakini inakuwa kinyume maana wanakiharibia na kusababisha wananchi wakichukie na Serikali nzima. Sheria inasema matokeo ya uchaguzi wa Diwani yatatangazwa ngazi ya kata, Mbunge ngazi ya Jimbo na Rais ngazi ya taifa katika eneo ambalo wataona linafaa. Katika hali ya kawaida, matokeo ya Rais yanaweza chukua siku mbili hadi tatu kutangazwa, matokeo ya Udiwani na Ubunge, yanaweza kutangazwa usiku wa siku hiyo hiyo baada ya uchaguzi au siku ya pili yake. Sasa hebu fikria Msimamizi wa uchaguzi atamgaze matokeo ya Udiwani au Ubunge tarehe 26 saa 4 asubuhi, watu tutulie mpaka tarehe 28 saa 8 mchana ndo tushangilie, hayo kweli nimaelekezo halali kutoka kwa Kiongozi halali ?
 
Back
Top Bottom