CCM wamejiandaa kukubali matokeo?

CCM wamejiandaa kukubali matokeo?

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
61,202
Reaction score
99,941
Wanajamvi namshukuru Mungu kumekucha salama, nimefurahi pia kusikia kuwa Yericko Nyerere ni mzima lakini pia sijawahi kumuona ndugu yangu BAK ambaye kila siku hakukosa kupost kitu chenye maana, nilitamani sana pia kwenye kipindi hiki tumsikie ndugu yetu KAINERUGABA MSEMAKWELI, yupo salama?

Kwa mara nyingi sana tumesikia Wapinzani wakiulizwa utayari wao wa kukubali matokeo endapo yatatoka kinyume na matarajio yao lakini swali kama hili hili hua hawaulizwi CCM as if wao ndio wenye haki ya kushinda na wengine kushinda kwao ni bahati nasibu.

Leo niwaulize Makada wa CCM kwa mwendo huu tunaouona, je kama mambo yatakuja ndivyo sivyo CCM watakubali kushindwa? Je Jk atakua tayari kumkabidhi mikoba Lowasa? Je Jeshi la Polisi ambao kwa sasa wako kila mahali wakikamata vijana wasio hatia, watakua tayari kuwapa ushirikiano UKAWA!? Na kukiri kwao kutumika kwa ahadi za vyeo na nyongeza za mishahara?

Asanteni, safarini Njombe ndani ya Luwinzo.
 
Last edited by a moderator:
Swali lako ni zuri sana lakini uko biased kuliko maelezo. Mfano hayo ya vijana kukamatwa bila"hatia" ni ushabiki. Kwanza polisi hawakamati kwa hatia maana hatia inatamkwa mahakamani.
 
Mzeewenu amekubali matokeo na kusema kuwa atarudi Longido kuchunga ng'ombe kwa boma...watanzania wengi wamemuheshimu kwa hilo.
Ila swali ni, je hatakuwa na interest tena ya kujenga chama?
 
Asiyekubali kushindwa si mshindani.Aidha kwa usalama wa Taifa,amani na utulivu,ni vyema CCM ijiandae kisaikolojia,maana Wapiga kura wataamua kupitia sanduku la kura baada ya kupima madhila ya miaka 54 na ahadi zilizotolewa!!
 
Tunataka mshindi wa Kwenye Sanduku la kura kama alivyosema mdau hapo juu.Maamuzi ya wengi yaheshimiwe.Mgombea yeyote atakayashinda kwa kura halali akabidhiwe nchi.Hatutaki vurugu nchi hii.
 
Wanajamvi namshukuru Mungu kumekucha salama, nimefurahi pia kusikia kuwa Yericko Nyerere ni mzima lakini pia sijawahi kumuona ndugu yangu BAK ambaye kila siku hakukosa kupost kitu chenye maana, nilitamani sana pia kwenye kipindi hiki tumsikie ndugu yetu KAINERUGABA MSEMAKWELI, yupo salama?

Kwa mara nyingi sana tumesikia Wapinzani wakiulizwa utayari wao wa kukubali matokeo endapo yatatoka kinyume na matarajio yao lakini swali kama hili hili hua hawaulizwi CCM as if wao ndio wenye haki ya kushinda na wengine kushinda kwao ni bahati nasibu.

Leo niwaulize Makada wa CCM kwa mwendo huu tunaouona, je kama mambo yatakuja ndivyo sivyo CCM watakubali kushindwa? Je Jk atakua tayari kumkabidhi mikoba Lowasa? Je Jeshi la Polisi ambao kwa sasa wako kila mahali wakikamata vijana wasio hatia, watakua tayari kuwapa ushirikiano UKAWA!? Na kukiri kwao kutumika kwa ahadi za vyeo na nyongeza za mishahara?

Asanteni, safarini Njombe ndani ya Luwinzo.

Ni kweli kwaweza kua na shida,lakini kukili jambo fulani litatokea kesho na kesho yenyewe huijui ni tatizo,hatupendi vurugu inchi hii na ni kama naiona naishia kuomba MUNGU tu,kauli za wanasiasa zinawajaza watu hata visivyofikilika
 
Last edited by a moderator:
Swali lako ni zuri sana lakini uko biased kuliko maelezo. Mfano hayo ya vijana kukamatwa bila"hatia" ni ushabiki. Kwanza polisi hawakamati kwa hatia maana hatia inatamkwa mahakamani.

Hahahahaaa hahahaaa kabla ya kunihukumu kuwa niko biased, at least ungetumia busara chache ya kuniuliza kama nina evidence! Basi tuyaache hayo, jibu at least swali tu
 
Mzeewenu amekubali matokeo na kusema kuwa atarudi Longido kuchunga ng'ombe kwa boma...watanzania wengi wamemuheshimu kwa hilo.
Ila swali ni, je hatakuwa na interest tena ya kujenga chama?

Hapo ndio penye msingi wa swali langu kuwa "Mzee wetu " atakubali, je na nyie "kijana " wenu na nyie wenyewe mtakubali? Yeye amesha declare naomba na nyie mfanye vivyo hivyo. Msikwepe swali, mbona liko wazi swali langu?
 
Nionavyo mimi ni kwamba CCM haijawa tayari kupokea matokeo.
Wameandaa polisi wa kuwasumbua wananchi.
 
Natangaza ushindi wa kwa kihistoria kwa UKaWa na Watanzania wote!!!!!!!!!!!!!!!.

Natamka anguko kubwa la ccm na mamluki wake wote.

Ninasambaratisha na kuvuruga usemi wa vikundi vya wana ccm wachache waliosalia.

Ninaangusha kila nguzo wanayoitegemea kuitumia kughushi matokeo.

Ninaamuru viongozi wote wanaopanga, kuratibu na kudhamiria kutumia vyeo vyao katika kuhujumu matokeo halali ya uchaguzi, wasipate nafasi ya kufanya maovu hayo, nafasi zao ziondoke mbele ya washabiki wao, walilpe gharama ya dhamira zao mbovu kwa gharama yao wenyewe.

Natamka mauti kwa wachawi na wanaotumia uchawi katika uchaguzi.

Ninanena amani, haki, na ushindi mkubwa kwa taifa la Tanzania chini ya UKaWA.

Atakayedhamiria kufanya hujuma ama kutekeleza hujuma aanguke mbele ya wakuu wake na anaowategemea wamsaliti abaki katika giza lenye upweke bila mfariji.

NINABATILISHA KILA MPANGO ULIOKWISHA KUPANGWA, UNAOPANGWA AU UTAKAOPANGWA AMA KUFANYIKA WAKATI WOWOTE KATIKA UCHAGUZI HADI MATANGAZO YA KURA ZA UCHAGUZI HADI KUAPISHA WASHINDI, ULIO KINYUME NA KWELI NA HAKI. MIPANGO YOTE MIOVU IHARIBIKE NA KUFANYIKA AIBU JUU YA VICHWA VYA WAHARIBIFU ILI WAWE SOMO KWA BINADAMU WENGINE DUNIANI KWA UTUKUFU WA JINA LA BWANA YESU KRISTO ANAYEISHI MILELE.

WATU WOTE WASEME AMINA.

Big Amen, na CCM wote pia waseme Amen
 
Hapo ndio penye msingi wa swali langu kuwa "Mzee wetu " atakubali, je na nyie "kijana " wenu na nyie wenyewe mtakubali? Yeye amesha declare naomba na nyie mfanye vivyo hivyo. Msikwepe swali, mbona liko wazi swali langu?
Muulizeni muone kama atakwepa swali
 
Mzeewenu amekubali matokeo na kusema kuwa atarudi Longido kuchunga ng'ombe kwa boma...watanzania wengi wamemuheshimu kwa hilo.
Ila swali ni, je hatakuwa na interest tena ya kujenga chama?
Jaman tuwe na akili za kujiongeza kwan hawez kukijenga chama pia akawa mchungaji? Au ndo yaleyale ya sadam rais wa Kuwait?
 
shein amekataa kulijibu na makufuli hawezi kujibu wao ndio wamemilikishwa hii inchi
 
Nina taarifa za ndan kutoka kwa ndugu yngu mnyeti....ccm washaanza maandaliz ya kumuapisha magufuli so wananchi tutulie tu hii nchi hamna democracy ni maneno tu wanayatamka wapate misaada huko kwa wazungu.
 
Mzeewenu amekubali matokeo na kusema kuwa atarudi Longido kuchunga ng'ombe kwa boma...watanzania wengi wamemuheshimu kwa hilo.
Ila swali ni, je hatakuwa na interest tena ya kujenga chama?
Washindanapo fahari wawili ni lazima mmoja atashindwa.

Tayari Lowassa ameonyesha njia, alipohojiwa na BBC alieleza bayana kuwa iwapo atashindwa kwenye uchaguzi wa keshokutwa atarudi Monduli kwenda kufuga ng'ombe wake.

Tunamtaka Magufuli na CCM yake wajitokeze hadharani na wautangazie Umma wa watanzania kuwa iwapo wao nao watashindwa, watayapokea matokeo hayo na kuwa tayari kukabidhi madaraka kwa amani kwa Ukawa.

Iwapo Magufuli 'atagoma' kutamka hadharani kuwa iwapo na yeye atashindwa kwenye sanduku la kura basi atakuwa tayari kuyapokea matokeo, tutaamini kuwa lipo jambo nyuma ya pazia la goli la mkono ambalo maccm wamelipanga.

Itabidi CCM wasikilize ushauri wa busara sana alioutoa Goodluck Jonathan, aliyekuwa Rais wa Nigeria ambaye alikabidhi madaraka kwa amani kwa mpinzani wake Mohamed Buhari aliyeshinda uchaguzi huo. kuwa yeyote atakayeshindwa kwenye uchaguzi wa keshokutwa awe tayari kuyapokea matokeo hayo.

Kitendo chochote cha CCM kulazimisha goli la mkono kitaisababishia nchi hii machafuko na wao CCM hawataepuka mkono wa vijana wa Bensouda wa kuburuzwa kupelekwa The Hague kujibu mashitaka ya uhalifu na kusababisha machafuko kwenye nchi hii.
 
Wanajamvi namshukuru Mungu kumekucha salama, nimefurahi pia kusikia kuwa Yericko Nyerere ni mzima lakini pia sijawahi kumuona ndugu yangu BAK ambaye kila siku hakukosa kupost kitu chenye maana, nilitamani sana pia kwenye kipindi hiki tumsikie ndugu yetu KAINERUGABA MSEMAKWELI, yupo salama?

Kwa mara nyingi sana tumesikia Wapinzani wakiulizwa utayari wao wa kukubali matokeo endapo yatatoka kinyume na matarajio yao lakini swali kama hili hili hua hawaulizwi CCM as if wao ndio wenye haki ya kushinda na wengine kushinda kwao ni bahati nasibu.

Leo niwaulize Makada wa CCM kwa mwendo huu tunaouona, je kama mambo yatakuja ndivyo sivyo CCM watakubali kushindwa? Je Jk atakua tayari kumkabidhi mikoba Lowasa? Je Jeshi la Polisi ambao kwa sasa wako kila mahali wakikamata vijana wasio hatia, watakua tayari kuwapa ushirikiano UKAWA!? Na kukiri kwao kutumika kwa ahadi za vyeo na nyongeza za mishahara?

Asanteni, safarini Njombe ndani ya Luwinzo.

Lakini pia yapasa tuwaulize Ukawa iwapo watakubali matokeo,kama CCM itashinda
 
Last edited by a moderator:
Nionavyo mimi ni kwamba CCM haijawa tayari kupokea matokeo.
Wameandaa polisi wa kuwasumbua wananchi.
Hasa tukitilia maanani magari 399 mapya ambayo JK ameyakabidhi kwa Polisi wiki hii, pamoja na kauli ya IGP kuwa ni marufuku watanzania nchi nzima kumshangilia hata diwani au mbunge wake aliyeshinda, hata kama atakuwa ametangazwa na msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo husika hadi litakapokamilika tendo la kumuapisha Rais mpya wa awamu ya 5!!!!!!!
 
Back
Top Bottom