CCM waiba bendera za CHADEMA Singida

CCM waiba bendera za CHADEMA Singida

KALOKAZA

Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
95
Reaction score
135

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Ikungi kimelaani vikali vitendo vilivyofanywa na baadhi ya vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kata ya Puma ya kuiba bendera za chama hicho zilizokuwa zimetundikwa na kupepea kwenye milingoti yake.

Akithibitisha kutokea kwa wizi huo,Katibu mwenezi wa Chadema wa jimbo la Singida magharibi,Bwana Yohana Anthoni alisema kuwa tukio hilo lilitokea katika kata ya Puma,wilayani Ikungi usiku wa kuamkia mei,21,mwaka huu.

Aidha katibu mwenezi huyo alifafanua kuwa siku ya tukio

Usiku wa kumkia mei,21 watu wanaodhaniwa kuwa ni vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) kwa kutumiwa na viongozi wa chama hicho waliiba bendera mbili zilizokuwa zimetundikwa zikipepea kwa viongozi wa chama hicho kata ya Puma.

Kwa mujibu wa Bwana Anhoni bendera moja iliyokuwa imetundikwa katika Kijiji cha Nkuninkana,kwenye eneo la Maina lililopo katika kituo cha kuuzia miwa ilinusurika kung’olewa na vijana hao baada ya mlinzi aliyekuwa akilinda duka lililokuwa karibu na shina ilipokuwa bendera hiyo.

Hata hivyo inasemekana kwamba baada ya mlinzi huyo kuwaona vijana hao ingawa hakuweza kuwatambua kwa majina,walimwomba awaache waondoke nayo bendera hiyo,lakini mlinzi huyo hakuwa tayari kuwaruhusu vijana hao kufanya wizi na ukatili huo.

Anafafanua katibu mwenezi huyo kwamba baada ya mlinzi huyo kutokuwa tayari kuruhusu wizi huo na ambao ni uvunjaji wa sheria za vyama vya siasa vilivyosajiliwa kisheria,ndipo vijana hao wa chama tawala walipoamua kuondoka na kuiacha bendera hiyo ikipepea.

Hata hivyo alipotakiwa kueleza ni sababu zipi zilizowafanya hadi vijana hao wafikie maamuzi hayo,Bwana Anthoni alisisitiza kuwa hali hiyo ilikuwa ikitaka kumdanganya katibu mkuu wa CCM Taifa,Bwana Abdurahmani Kinana kuwa maeneo hayo hayana viongozi wa vyama vya upinzani zaidi ya ccm peke yake.

Katibu mwenezi huyo hata hivyo alisema mara baada ya tukio hilo wameshatoa taarifa kwenye kituo kidogo cha polisi Puma ambao nao wamewaahidi kuwachukulia hatua wahusika watakapobainika na kwamba baada ya kufanya mawasiliano na OCD wameshapandisha bendera zingine kwenye Kijiji hicho.
 
kwa hali niliyoiona jana ccm wanayo kazi kubwa sana
yasije yakawakuta kama yaliyomkuta Joyce Banda wa MALAWI
 
ccm ilishakufa kitambo,zimebaki kelele tu za hawa waganga njaa wa buk 7.
 
Ccm iacheni hiyo cdm ijifie yenyewe maana sasa wanatafuta visingizio lukuki
 
TOFAUTI YA CHAMA CHADEMOKRASIA NA MAENDELEO​​​​(CHADEMA) NA CHAMA CHA MAPINDUZI (C.C.M)
UTANGULIZI
Wazo la kuandika katiba mpya lilikuwa ni wazo la CHADEMA kupitia mgombea wake Dr. Willibroad Peter Slaa. Wala halikuwa wazo la C.C.M wala mgombea wake Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

1. Tofauti ya "kwanza" ipo kwenye jina la vyama hivyo,wakati CHADEMA ni chama cha Demokrasia namaendeleo. Wao C.C.M ni chama cha kupindua mambo yote mazuri a.k.a kuyakataa na kuunga mkonomambo mabaya (ufisadi).

2. Wakati CHADEMA tunaunganisha nguvu za viongozi wetu kupiga vita "UFISADI". Wao C.C.M wanaungisha nguvu za viongozi wao kuwalinda "MAFISADI".

3.Wakati CHADEMA tunalinda rasilimali za umma (madini, misitu na wanyama) zisichukuliwe na wanaojiita wawekezaji. Wao C.C.M wanawalinda wawekezaji (wachukuaji) iliwaendelee kuchukua rasilimali za umma.

4.Wakati wabumge wa CHADEMA walipopinga tozo ya line za simu ambazo zitaumiza wananchi. Wao C.C.M waliunga mkono tozo hizo za line za simu kwa mbwembwe.

5.Wakati CHADEMA tunataka haki za binadamu na maadili ya viongozi viingie kwenye katiba mpya inayoandikwa na wananchi. Wao C.C.M wanapinga haki hizo zisiingie kwenye katiba.

6.Wakati CHADEMA tunataka tume huru ya ukaguzi.Wao C.C.M wanasema tume hii tuliyonayo inafaa.

7.Wakati CHADEMA tunaunga mkono Rasimu ya katiba,yenye maoni ya wananchi yene muundo wa Serikali tatu. Wao C.C.M wanaipinga Rasimu hiyo yenye maoni yawananchi.

"Rais Kikwete ndiye aliyeanzisha mchakato na yeye ndiye aliyesaini Rasimu ya pili mwanzo wa Rasimu na mwisho wa Rasimu. Na Kikwete huyo huyo ndiye aliyekuwawa kwanza kukataa jambo alilolikubali kwa kusainimwenyewe".
 
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Ikungi kimelaani vikali vitendo vilivyofanywa na baadhi ya vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kata ya Puma ya kuiba bendera za chama hicho zilizokuwa zimetundikwa na kupepea kwenye milingoti yake.

Akithibitisha kutokea kwa wizi huo,Katibu mwenezi wa Chadema wa jimbo la Singida magharibi,Bwana Yohana Anthoni alisema kuwa tukio hilo lilitokea katika kata ya Puma,wilayani Ikungi usiku wa kuamkia mei,21,mwaka huu.

Aidha katibu mwenezi huyo alifafanua kuwa siku ya tukio

Usiku wa kumkia mei,21 watu wanaodhaniwa kuwa ni vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) kwa kutumiwa na viongozi wa chama hicho waliiba bendera mbili zilizokuwa zimetundikwa zikipepea kwa viongozi wa chama hicho kata ya Puma.

Kwa mujibu wa Bwana Anhoni bendera moja iliyokuwa imetundikwa katika Kijiji cha Nkuninkana,kwenye eneo la Maina lililopo katika kituo cha kuuzia miwa ilinusurika kung’olewa na vijana hao baada ya mlinzi aliyekuwa akilinda duka lililokuwa karibu na shina ilipokuwa bendera hiyo.

Hata hivyo inasemekana kwamba baada ya mlinzi huyo kuwaona vijana hao ingawa hakuweza kuwatambua kwa majina,walimwomba awaache waondoke nayo bendera hiyo,lakini mlinzi huyo hakuwa tayari kuwaruhusu vijana hao kufanya wizi na ukatili huo.

Anafafanua katibu mwenezi huyo kwamba baada ya mlinzi huyo kutokuwa tayari kuruhusu wizi huo na ambao ni uvunjaji wa sheria za vyama vya siasa vilivyosajiliwa kisheria,ndipo vijana hao wa chama tawala walipoamua kuondoka na kuiacha bendera hiyo ikipepea.

Hata hivyo alipotakiwa kueleza ni sababu zipi zilizowafanya hadi vijana hao wafikie maamuzi hayo,Bwana Anthoni alisisitiza kuwa hali hiyo ilikuwa ikitaka kumdanganya katibu mkuu wa CCM Taifa,Bwana Abdurahmani Kinana kuwa maeneo hayo hayana viongozi wa vyama vya upinzani zaidi ya ccm peke yake.

Katibu mwenezi huyo hata hivyo alisema mara baada ya tukio hilo wameshatoa taarifa kwenye kituo kidogo cha polisi Puma ambao nao wamewaahidi kuwachukulia hatua wahusika watakapobainika na kwamba baada ya kufanya mawasiliano na OCD wameshapandisha bendera zingine kwenye Kijiji hicho.

Like father, like son. Mwenyekiti mkuu anawadanganya wananchi, wasaidizi wake wanamdanganya yeye, katibu mkuu anawadanganya wananchi, mawaziri wanawadangaya wabunge, wabunge wanalala usingizi.......halafu mwisho kabisa kuleee...wananchi wanawadanganya viongozi...like father.....!
 
kwani bendera zinapiga kura siku hizi? mnakazania vitu ambavyo havina maana yoyote. kama kipo moyoni kwa mtu kipo tu bila hata ya bendera.
 
Back
Top Bottom