CCM vs Local Businesses (Entrepreneurs). What a Shame! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM vs Local Businesses (Entrepreneurs). What a Shame!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nitasemaukweli, Jun 18, 2011.

 1. n

  nitasemaukweli Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Madudu ya vigogo hadharani

  • Viongozi wa wizara wadaiwa kupora mradi na Ratifa Baranyikwa


  SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, imeingizwa katika mvutano wa kibiashara ambao unahusisha taasisi ya nchini Ubelgiji inayoidhinisha kutumia mifumo ya biashara ya utambuzi wa bidhaa za kimataifa GSI, kwa kutumia nembo za mistari inayojulikana kama ‘bar codes'.

  Habari zilizolifikia gazeti hili kwa siku kadhaa sasa zimebaini kuwa mzozo huo unatokana na kile kinachoonekana kuwa ni jitihada za viongozi wa ngazi za juu wa wizara hiyo kudaiwa kutumia jina la serikali ya Rais Kikwete kutimiza haja binafsi za kibiashara.

  Tukio hili ambalo linaweza kuchafua taswira ya Serikali ya Tanzania, limeibuliwa na Mtanzania mjasiriamali Ole Koimere, anayeinyooshea kidole serikali ya Rais Kikwete hususan Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo, kwa kile alichodai njama za kumpora mradi wake wa kutaka kuanzisha huduma ya kutoa ‘bar codes' hapa nchini, ambayo kwa sasa haipatikani hadi nchi jirani.

  Mjasiriamali huyo, Ole Koimere anasisitiza kuwa mradi huo aliporwa, kwa madai kuwa yeye ndiye aliyetoa wazo la kuuanzisha hapa nchini akiwa amefuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kupata hati ya usajili kutoka Brela.

  Akizungumza na Tanzania Daima juu ya kisa hicho, mjasiriamali huyo, alidai kuwa mwaka 2010 akiwa katika semina moja iliyohusisha wajasiriamali pamoja na maofisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara, aliibua wazo hilo la Tanzania kushindwa kutoa huduma ya ‘bar codes'.

  Alisema kuwa baada ya kuibua wazo hilo ndani ya chumba cha mkutano, wakati wa mapumziko, aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, D. Massawe, alimfuata na kumweleza kuwa ni wazo zuri na kumwambia aandike maombi wizarani kuomba kuwa wakala wa kazi hiyo hapa nchini. Kila nchi haitakiwi kuwa na wakala zaidi ya mmoja.

  Ole Koimere alisema kuwa, aliandika barua hiyo Februari 10, mwaka jana (tunayo) akiomba kuwa wakala kwa hapa nchini.

  Alisema katika hali ya kushangaza baada ya siku mbili tu, wizara iliijibu barua yake (nakala tunayo) ikiwa imesainiwa na Massawe ikimjulisha kuwa kuna jitihada zilizoanzishwa hapa nchini kwa lengo la kuanzisha utaratibu wa kutoa huduma hiyo, akieleza kuwa kwa wakati huo TPSF na TIRDO walikuwa wakikusanya maoni ya wadau kabla ya kuitisha kikao cha pamoja kupanga mkakati wa kufanikisha azima hiyo.

  Alisema kuwa wakati huo pia walikuwa wakiendelea na zoezi la kusajili Kampuni ya GS1 Tanzania, ambapo waliandika barua Brela Februari 26,2010 kuomba usajili na Machi 18, mwaka huo huo walipata hati ya usajili nambari 75537.

  "Kwa kuwa maombi ya leseni hutumwa Ubelgiji yalipo makao makuu ya GS1 na mwisho wa kupeleka nyaraka za maombi kila mwaka ni Machi 31, tuliona tumechelewa hivyo tukaamua tujiandae kwa mwaka huu wa 2011…lakini maombi yetu tulikuwa tumeishatuma Ubelgiji Desemba 18, 2010 wakati tukisubiri barua za kuungwa mkono na kampuni 250 kama tulivyoagizwa na Brela."

  "Tuliandika barua SIDO, Desemba 2010 tukiomba kupitia kwao watuunge mkono katika kuzipata hizo kampuni lakini tulikwama kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi," alisema.

  Alisema Januari 19 mwaka huu walipokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Joyce Mapunjo (nakala ya barua tunayo), akitaka kuonana na wakurugenzi wa kampuni hiyo ya GS1 Tanzania Ltd.

  Kwa mujibu wa Ole Koimere, waliitikia wito huo lakini cha ajabu, katibu mkuu huyo aliwajulisha kuwa alikuwa amewaita kuwaomba wamuachie jina la kampuni yao hiyo lakini hata hivyo walimkatalia.

  Alisema baada ya siku kadhaa ilisajiliwa kampuni nyingine Brela, inayotambulika kwa jina la GS1 (TZ) National Ltd ambayo ilipata hati ya usajili Januari 28, mwaka huu na siku hiyo hiyo walipokea barua pepe kutoka Ubelgiji kwa Meneja Mkuu wa huduma, Monica Walsh, akimtaarifu kuwa tayari wamepokea maombi kutoka kwa kampuni ya hiyo ambayo alidai kwamba inaungwa mkono na Serikali ya Tanzania na kwamba mchana wa siku hiyo hiyo alikuwa akienda kukutana na mwakilishi wa kampuni hiyo kutoka Tanzania.

  Kwa kuwa utoaji wa ‘bar codes' hufanywa na kampuni moja tu kwa kila nchi, lakini Brela inashutumiwa kwa kuzisajili kampuni mbili kwa shughuli moja.

  Habari zaidi zinaeleza kuwa Kampuni ya GS1 (TZ) Ltd inadaiwa kuundwa na watu walio karibu na wizara hiyo, kadhalika ikidaiwa kutumia rasilimali za serikali ikiwamo Brela (ushahidi wa hilo upo katika barua iliyoandikwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Cyril Chami, nakala tunayo).

  Kadhalika zipo nyaraka za vikao vya maandalizi ya uanzishwaji wa kampuni hiyo, zikionyesha gharama kubwa zilizotumika ambazo inasemekana zimekuwa zikitolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara.

  Moja ya vikao kilichofanyika Ubungo Plaza, kati ya Januari 24 au Machi 5, mwaka huu nyaraka hizo zinaonyesha kuwa kiasi cha zaidi ya sh milioni 46 zilitumika.

  Mbali na mjasiriamali huyo kuzungumza na gazeti hili, pia amepata kukutana na Waziri Chami na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumueleza juu ya hujuma hiyo inayodaiwa kufanywa na viongozi wa wizara dhidi yake.

  Alisema mara ya kwanza mbali na kukutana na Katibu Mkuu huyo, Mapunjo pia aliwahi kukutana na baadhi ya viongozi walioko Ikulu lakini hadi sasa hakuna alichojibiwa, hatua ambayo ilimfanya atafute nafasi ya kukutana na Rais Kikwete lakini bila mafanikio, ambapo sasa ameamua kumwandikia barua.

  Wakati Ole Koimere akilalamikia kupokwa mradi huo, Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mapunjo, ambaye sasa anahudhuria mkutano wa Agoa nchini Zambia, hivi karibuni alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu madai hayo alisema kuwa hajawahi kupokea malalamiko yoyote kutoka kwa watu hao.

  Katikati ya wiki hii Mapunjo aliitisha mkutano na waandishi wa habari kuutaarifu umma kuwa Tanzania imefanikiwa kuidhinishwa kutumia ‘bar code'.

  Katika mkutano huo ambao pia aliongozana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Esterian Mahingila, naye alipoulizwa kama kuna kampuni nyingine ilisajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma hiyo alikana madai hayo na kusema kuwa kampuni iliyosajiliwa ni moja tu.

  Madudu ya vigogo hadharani

  Analysis
  Nianze kwa kufafanua maana ya entrepreneurship.
  Entrepreneurship is the act of being an entrepreneur, which can be defined as "one who undertakes innovations, finance and business acumen in an effort to transform innovations into economic goods". This may result in new organizations in response to a perceived opportunity. The most obvious form of entrepreneurship is that of starting new Startup Company; however, in recent years, the term has been extended to include social and political forms of entrepreneurial activity. According to Wikipedia,
  Entrepreneurship - Wikipedia, the free encyclopedia

  Ukisoma hii article above, utaona vitu vingi vya serikali ya kikwete na ukajua wazi kwanini kikwete na watumishi wenzio hawataki ‘transparency' katika maswala yanayohusu nchi na taifa. Moja kwa moja hili tukio limenikumbusha testimonies nyingi sana ambazo unazisikia kila mahali unapotembea Tanzania. Wananchi na hasa wafanyabishara wengi ambao ndio back bone ya taifa katika kujenga uchumi wa Taifa na kuliingizia Taifa mapato ndio wa kwanza either kunyanganywa ideas and creativity ili waliopo serikalini (kundi lililoajiliwa na kikwete) wapate miradi na mapato ya juu. Hili tukio limenikumbusha jamaa mmoja aishie nje ya nchi na mara alipomaliza masomo ya udaktari na akapata nafasi ya kupata wadhamini wa kujenga health clinics Tanzania na ikamchukua miaka karibu miaka mitano kupata kibali cha kufungua hizi huduma, by the time serikali ilipompa hiki kibali wafadhili wengi walikuwa hawana hizo fedha tena. Hapa tunaona testimony hii ambayo ndio kwanza imeenza na tutaifuatilia kwa undani kila siku na kwamba tunampa huyu mama fisadi Joyce Mapunjo wiki mbili kujieleza na kufuta hii kampuni yake fake ya kutafuta retirement na kipato cha kihuni. Ushahidi upo kila mahali na ninaamini huyu entrepreneur Mr Ole Koimere apate justice. We have questions for you Joyce, why did you sign another company while the first person should be considered first? The records and response from the government office indicated that Mr. Ole already listed his company and he was the first to introduce this idea. Why you Joyce registered
  The major problem we have in Tanzania is incompetency na kufanya maamuzi purposely kujinufasisha ili hizi systems za kujigamba kuendelea kuwepo Tanzania. Why I am saying this? Tuangalie efforts za kuleta ‘transparency' katika serikali ambazo kwa upande mwingine ni sambamba na mapambano ya constitution Tanzania. Hawa ccm na makundi yao some how wanataka tuendelee kuwa na poor systems katika uandikishaji wa makampuni, poor and protective government records, na zaidi wanapinga any systems ya kuzuia njia za kulinda intellectual properties, ideas na innovations. Mfano mwingine ni jinsi gani national id project ilivyo jaa back door deals kila mahali kwa sababu they (ccm) knows there is a lot of money to be made. Tuangalie swala la upatikanaji wa leseni za kuendesha na biashara, upatikanaji wa passport, upimaji wa ardhi na utoaji wa hati za mashamamba, utoaji wa bidhaa bandalini na upatikanaji wa kazi sehemu kama BOT. Hii mifano na environment zilivyo zimejenga ukuta wa back door deals na corruption ya ajabu, Je Kikwete ajui haya au Mkapa alikuwa hajui haya? Au Mwinyi? Due the corruption culture, now we have wealth leaders everywhere. Most of these people (ccm) fighting to keep this system and culture. For us (Tanzanians), we have pull ourselves and organize to fight them and our future. The truth is today such a crime happened to Mr. Ole but tomorrow it can be you or your family.

  Why PCCB can't be government independent agency? Why kikwete and ccm keep interfering with PCCB? Why Bunge can't fund PCCB?
  Prevention and Combating of Corruption Bureau

  "The key to these problems is for us Tanzanians to continue fighting for social justice at the same time prosecuting those government officials who take advantages of the environment. We all know that people always win and let's make sure we fight for all and not only the few."
   
 2. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Serikali ya MAFISADI, WEZI, WATU WASIOWAJIBIKA NA WAKANDAMIZAJI!!! CORRUPT GOVERNMENT
   
 3. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,649
  Trophy Points: 280

  poshoooooooooooooooo!!!!!!!!!!
   
Loading...