kibananhukhu
JF-Expert Member
- Jul 6, 2009
- 366
- 165
CCM wanajua yote uliyoyasema,ubinafsi ndio tatizo lililopoNinajiuliza maswali mengi kuliko majibu.
1. Hivi ni kweli tatizo la Tanzania ni Katiba!?
2. Hivi ni kweli tunaamini watanzania wanataka mabadiliko?
3. Kama tuliweza kuanza mchakato wa mabadiliko "ccm" kwa kuruhusu mchakato wa katiba, ilikuwaje tusiyasimamie mabadiliko kuanzia hatua ya mwanzo, ninamaanisha kutambua aina ya mabadiliko na namna nzuri ya kuyaleta.
4. Ni "think tank" yupi alishauri kuhusu tume ya Rais Mkti Warioba? Alitarajia nini kutoka kwa tume hiyo?
5. Hatuoni kuwa wana ccm wenzetu walio kimya na wanadai kukipenda chama wanatuumiza kwa kuto wajibika? Mfano, kutochangia hoja na kutoshiriki bungeni kwa kupiga kura?
6. Kwa nini hatukuona makosa ya sisi kuwa wenyeviti katika bunge la katiba, tunaanza kuongea dk 40 hoja zetu kwa mbwembwe, halafu tunanywea mwishoni wakati wa kusoma maoni ya walio wachache, mnadhani ni picha gani tunaitoa kwa wananchi. Ni lazima kuona kuwa walio wachache wanakuja na hoja zenye nguvu, na wanacharge full time. Hatukuwa na sababu ya kupanga hivyo kwani inaonekana kama vile mashambulizi yanatoka upande mmoja tu, kwa walio wachache. Wao wanaonekana dhahiri kuwa wanashambulia, sisi au wenyeviti wetu wanaonekana dhahiri kuwa ni kama MA MC, yaani wanasoma maoni ya pande zote mbili. Si rahisi kubadili mwelekeo wa hoja bila kubadilika sura.
7. Ni kweli sasa hivi chama chetu ccm, hakina vipaji vya kuona mbali? Vision! Kwa nini tunaona kama vile kuna mapya mengi kutoka upande wa wachache.
8. Ni kweli tunaamini Watanzania wataweza wote, kuamini kuwa tume ya Rais na Jaji Warioba haina mahusiano na CCM? Naona kama vile tumerogwa au kuna wenzetu wanatukaanga kwa kutoa ushauri unaotuzamisha.
Pamoja na maswali mengi, tusikate tamaa. Kuna mambo ya kufanya haraka. Kwanza ni vizuri tukubali kuna makosa tumefanya. Pili, basi tujikosoe au tukosoane. Tatu, ni vizuri tukapanga timu mpya yenye kasi na kushughulikia mabadiliko yanayotakiwa na watanzania ili yasije yakatoka kwa watu wasio wa ccm.
Tusiogope kukubali jambo jema lolote kutoka kwa watanzania bila kujali limekuja kupitia wapi, iwe limepita CUF, CDM, NCCR au chama chochote cha siasa. Kukubali kosa, kukubali maoni kutoka pande tofauti ni afya. Na hili ni vizuri tukalifanya haraka kwani hata mwenyekiti wetu kuna badhi ya wosia ametuachia mfano, tuwe tayari kisaikolojia kukumbana na mabadiliko na akili ya kuambiwa changanya na ya kwako.
Nipo mitaani, ninatembea maeneo mengi, ninajichanganya na wengi, tunawakosa watu wengi ambao hawatuelewi. Ninajuta hata kufikiri kwanini tumeanza mchakato na inaonekana kana kwamba tunatumia nguvu mno?
Ni lazima tufanye yafuatayo pia.
i. Tusisite kuelezana ukweli
ii. Makosa ya watendaji serikalini yashughulikiwe haraka.
iii. Watendaji wasio na uwezo na wasio wabunifu watolewe haraka na tuwaweke watu wenye vipaji kwani wao kwa utendaji wao mbovu ndio wamekifikisha chama chetu hapa. Tuzingatie sana huduma za afya, elimu, kilimo, na ustawi wa jamii. Ki-uchumi napo hatujajipanga vizuri. Uchumi mpana sawa, uchumi wa chini pia ni vizuri ukaonekana mara moja miongoni mwa jamii. Fursa zifunguliwe na serikali kama facilitator.
Samahani sana kwa wana ccm wenzangu ambao nitakuwa nimewakwaza. Naona kama boti inakwenda mrama.
CCM ni gari kubwa wewe. Hayo malumbano ya bungeni Ni upepo utapita tu!
Yaani kama ulikuwa kichwani mwangu mm jambo hili nimefikilia kwa kina sana, iweje maoni ya wengi yasome kisha ufafanuzi utolewe na wachache ambao wao mawazo yao na ufafanuzi tayari umo kwenye randama za tume? Tumefanya kosa kubwa la kiufundi, lkn pia tuna watu ambao ni wasomi ambao wanauwezo mkubwa wa kufafanua mambo lkn hatuwatumii ,hii inaumiza sana , na inaonekana yanayosemwa na upinzani kama yanaukweli ingawa ni porojo tuu, ni wakati sasa kwa kamati zilizo baki tujipange kuvunja hoja zote na hatimae watanzania watuelewe,, Kuna watu kama Mwakyembe, Mzee Kingunge , Zambi, Kaijage , Simbachawene , Mama Migiro ,Saada Mkuya wanaweza kabisa kusimama hapo na kwa ufundi wao wa kuongea tunaweza kubadili upepo,, hata kilichotokea juzi wakati dr. Charles , Mh Ummy mwalimu na dr..Kigwangara wapinzani walihamaki kwa kuwa walijuwa mbinu hizo ndizo zinazoweza kuvutia mjadala na kupelekea Kuanza kuzomea wakidai kuwa kanuni zimevunjwa ili ilikuwa ni janja ya kuzuia mashambulizi. Nawasihi kuanzia Jumatatu ni kuongeza Mashambulizi .

Ni kweli, Wenzetu wana baadhi ya mambo mazuri. Lakini sisi tuna mazuri mengi zaidi na tuna mengi ya kujengea hoja japo kuna mangine yanataka utendaji. Katika hali tunayokwenda nayo, kuna hatari ya baadhi ya watu wakachoka. Tuna list mfano ya mambo mengi ya ki uchumi yaliyofanywa, lakini kwa kosa la kujipanga yanaweza yasionekane. Mfano, Miaka 50 ya muungano inasemwa na wachache kana kwamba ni bure kabisa wakati waheshimiwa wenyewe wapo dodoma pamoja, wakitoka wanalipana allowance pamoja, wanakwenda kula pamoja, wengine wanapendana pamoja, na wanafurahi pamoja. Hilo peke yake ni dalili ya afya ya kisiasa. Wanakaa Jengo Moja bila shida hadi Raha.
Mwanasheria mkuu mstaafu wa Kenya Wakko, alisema wanatuona kuwa mfano bora Duniani kwa mengi, sisi twajionaje? Ni kweli kuna makosa yamefanyika, tuyakubali. Tujisahihishe mapema kwani inawezekana. Na hapa ni kubadilka kweli kweli. Ni lazima mfumo wa utendaji ubadilike. Mbona nchi hii ina uwezo wa ku jiendesha kwa utalii tu!? acha tanzanite na gas, Tanzania ni nchi ya pili kwa vivutio Duniani. Kuna baadhi ya watendaji wamepewa dhamana na CCM lakini wanatuangusha. Hawawi wabunifu kiasi cha kuleta malalamiko.
Pamoja na yote, kuna mambo muhimu na makubwa sana yamefanywa na CCM Kiasi hata wenzetu wapinzani walio waungwana wanatucheka kuwa hatuwezi kuyasimamia.
Yaani kama ulikuwa kichwani mwangu mm jambo hili nimefikilia kwa kina sana, iweje maoni ya wengi yasome kisha ufafanuzi utolewe na wachache ambao wao mawazo yao na ufafanuzi tayari umo kwenye randama za tume? Tumefanya kosa kubwa la kiufundi, lkn pia tuna watu ambao ni wasomi ambao wanauwezo mkubwa wa kufafanua mambo lkn hatuwatumii ,hii inaumiza sana , na inaonekana yanayosemwa na upinzani kama yanaukweli ingawa ni porojo tuu, ni wakati sasa kwa kamati zilizo baki tujipange kuvunja hoja zote na hatimae watanzania watuelewe,, Kuna watu kama Mwakyembe, Mzee Kingunge , Zambi, Kaijage , Simbachawene , Mama Migiro ,Saada Mkuya wanaweza kabisa kusimama hapo na kwa ufundi wao wa kuongea tunaweza kubadili upepo,, hata kilichotokea juzi wakati dr. Charles , Mh Ummy mwalimu na dr..Kigwangara wapinzani walihamaki kwa kuwa walijuwa mbinu hizo ndizo zinazoweza kuvutia mjadala na kupelekea Kuanza kuzomea wakidai kuwa kanuni zimevunjwa ili ilikuwa ni janja ya kuzuia mashambulizi. Nawasihi kuanzia Jumatatu ni kuongeza Mashambulizi .
Haya ya uchumi na maendeleo ya jamii wala sio yanayotuangusha na kututia aibu bungeni. Linalotuangusha ni swala la muundo wa Muungano ambalo hata sisi wenyewe hatukubaliani nalo ila tu kama chama, wachache wameamua uwe msimamo wa chama na hatuna ruksa kuonyesha misimamo yetu. Ukweli pale tunashindwa kutetea sababu hatuna hamasa. Ni vigumu sana kushabikia jambo ambalo hulipendi. Tulio wengi Ndani ya CCM haturidhiki na msimamo wa chama chetu juu ya muundo wa muungano, tutatoa wapi wahka wa kupiga kelele kushangilia hoja za walio wengi? Hata katika vikao vya kamati hali ni mbaya sana, hatuna hoja kabisa, tumebaki na kura tu!