kibananhukhu
JF-Expert Member
- Jul 6, 2009
- 366
- 165
Ninajiuliza maswali mengi kuliko majibu.
1. Hivi ni kweli tatizo la Tanzania ni Katiba!?
2. Hivi ni kweli tunaamini watanzania wanataka mabadiliko?
3. Kama tuliweza kuanza mchakato wa mabadiliko "ccm" kwa kuruhusu mchakato wa katiba, ilikuwaje tusiyasimamie mabadiliko kuanzia hatua ya mwanzo, ninamaanisha kutambua aina ya mabadiliko na namna nzuri ya kuyaleta.
4. Ni "think tank" yupi alishauri kuhusu tume ya Rais Mkti Warioba? Alitarajia nini kutoka kwa tume hiyo?
5. Hatuoni kuwa wana ccm wenzetu walio kimya na wanadai kukipenda chama wanatuumiza kwa kuto wajibika? Mfano, kutochangia hoja na kutoshiriki bungeni kwa kupiga kura?
6. Kwa nini hatukuona makosa ya sisi kuwa wenyeviti katika bunge la katiba, tunaanza kuongea dk 40 hoja zetu kwa mbwembwe, halafu tunanywea mwishoni wakati wa kusoma maoni ya walio wachache, mnadhani ni picha gani tunaitoa kwa wananchi. Ni lazima kuona kuwa walio wachache wanakuja na hoja zenye nguvu, na wanacharge full time. Hatukuwa na sababu ya kupanga hivyo kwani inaonekana kama vile mashambulizi yanatoka upande mmoja tu, kwa walio wachache. Wao wanaonekana dhahiri kuwa wanashambulia, sisi au wenyeviti wetu wanaonekana dhahiri kuwa ni kama MA MC, yaani wanasoma maoni ya pande zote mbili. Si rahisi kubadili mwelekeo wa hoja bila kubadilika sura.
7. Ni kweli sasa hivi chama chetu ccm, hakina vipaji vya kuona mbali? Vision! Kwa nini tunaona kama vile kuna mapya mengi kutoka upande wa wachache.
8. Ni kweli tunaamini Watanzania wataweza wote, kuamini kuwa tume ya Rais na Jaji Warioba haina mahusiano na CCM? Naona kama vile tumerogwa au kuna wenzetu wanatukaanga kwa kutoa ushauri unaotuzamisha.
Pamoja na maswali mengi, tusikate tamaa. Kuna mambo ya kufanya haraka. Kwanza ni vizuri tukubali kuna makosa tumefanya. Pili, basi tujikosoe au tukosoane. Tatu, ni vizuri tukapanga timu mpya yenye kasi na kushughulikia mabadiliko yanayotakiwa na watanzania ili yasije yakatoka kwa watu wasio wa ccm.
Tusiogope kukubali jambo jema lolote kutoka kwa watanzania bila kujali limekuja kupitia wapi, iwe limepita CUF, CDM, NCCR au chama chochote cha siasa. Kukubali kosa, kukubali maoni kutoka pande tofauti ni afya. Na hili ni vizuri tukalifanya haraka kwani hata mwenyekiti wetu kuna badhi ya wosia ametuachia mfano, tuwe tayari kisaikolojia kukumbana na mabadiliko na akili ya kuambiwa changanya na ya kwako.
Nipo mitaani, ninatembea maeneo mengi, ninajichanganya na wengi, tunawakosa watu wengi ambao hawatuelewi. Ninajuta hata kufikiri kwanini tumeanza mchakato na inaonekana kana kwamba tunatumia nguvu mno?
Ni lazima tufanye yafuatayo pia.
i. Tusisite kuelezana ukweli
ii. Makosa ya watendaji serikalini yashughulikiwe haraka.
iii. Watendaji wasio na uwezo na wasio wabunifu watolewe haraka na tuwaweke watu wenye vipaji kwani wao kwa utendaji wao mbovu ndio wamekifikisha chama chetu hapa. Tuzingatie sana huduma za afya, elimu, kilimo, na ustawi wa jamii. Ki-uchumi napo hatujajipanga vizuri. Uchumi mpana sawa, uchumi wa chini pia ni vizuri ukaonekana mara moja miongoni mwa jamii. Fursa zifunguliwe na serikali kama facilitator.
Samahani sana kwa wana ccm wenzangu ambao nitakuwa nimewakwaza. Naona kama boti inakwenda mrama.