Wajitahidi kusoma historia na kujiandaa kisaikolojia. Tatizo kila wanapotaka kujitetea na kuinuka tena, ndiyo wanaharibu kabisa. Mfano Katibu mkuu wa chama (CCM) kuwaita wanaoshindwa kwenye vinyang'anyiro vya kuomba ridhaa ya kugombania Urais, Ubunge na Udiwani kuwa ni makapi. Wapo walioshindwa kweli sababu kama wanaogombania ni wengi lazima apatikane mshindi. Na vilevile wapo wanaoshindwa kwa hila, mpano wanaokatwa majina kinyume cha kanuni, wanaoibiwa kura zao vituoni (tumeshuhidia mengi) na wapo wanaoshinda kwa kutoa rushwa. Sasa ni wazi msimamo huu wa chama utazidi kuwagawa na kuwafukuza wengi ndani ya chama. Na je wananchi tutawachukuliaje hao makapi, mara wanapokuja kukinadi chama chao?.