CCM: Tutachukua hatua kwa mbunge aliyeghushi sifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Tutachukua hatua kwa mbunge aliyeghushi sifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 26, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umesema mgogoro wa udanganyifu wa umri na elimu unaomkabili Mbunge wa Viti Maalum Wanawake kupitia UVCCM Zanzibar, Asha Muhamed Omar, umekabidhiwa kwenye kamati maalumu ili kutafuta ukweli na kuchukua hatua.
  Hayo yalisemwa juzi na katibu wa umoja huo, Martin Shigela, wakati akitokea Dodoma kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UV-CCM).
  Shigela alisema umoja huo unaufahamu mgogoro huo na imeundwa kamati ambayo hivi sasa imo katika kufuatilia suala hilo kwa karibu.
  Alisema hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kutokana na utendaji kazi wa kamati hiyo kwani watakapomaliza kazi hiyo kila mmoja atajua matokeo yake.
  "Pamoja na kwamba mimi ndiyo mtendaji mkuu lakini si vizuri kuilazimisha kamati hiyo ifanye kazi kama unavyotaka wewe …huo utakuwa ni udikteta, tusubiri ukweli utajulikana," alisema Shigela.
  Mgogoro huo umeibuka baada ya mgombea wa nafasi hiyo ambaye alishika nafasi ya pili katika uchguzi huo, Tarehe Khamis Hamad, kulalamika kuwa kumekuwa na ucheleweshwaji wa maamuzi ya kamati hiyo.
  Tarehe alisema kama ni vielelezo amekwishaviwakilisha kwa katibu mkuu huyo wa UVCCM na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Yusuf Makamba.
  Alisema katika malalamiko yake hayo, alifikia hatua ya kumuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, Oktoba 10 mwaka jana yenye Kumb.Na.CCM/OND/559/Vol.1/54. ambapo hata katika ofisi ya Katibu Mkuu wa UVCCM aliifikisha barua hiyo Septemba 13, mwaka huo huo wa 2010. "Ukiangalia kuna zaidi ya miezi mitano imepita sasa bila kuchukuliwa kwa hatua zozote ambazo zingemaliza tatizo hilo zaidi ya kuambiwa kila mara kuwa linashughulikiwa na kamati kitendo ambacho si ridhiki nacho," alisema Tarehe.
   
 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  Mungeanza na mawziri walio gushi vyeti ndo tuseme mko serious siyo kumuonea huyo mama.yeye kacopy kwa wakubwa zake
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wanachakachua kila mahala
   
 4. oba

  oba JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  It is bacause you value more politics than reality, hata mahali panapotakiwa kufanya maamzi papo kwa papo mnaleta siasa kwa sababu mmekuwa maswahiba mpaka kila mmoja anaogopa kitakachofuata maamzi yake hata kama yamefanywa kwa misingi ya katiba yenu!
   
Loading...