CCM tusilaumiane


Kibadikisha jina ni kama shehe anayebadili kanzu huku akibakia yuleyule. Kimebadikisha jina toka TANU na kuwa CCM. Toka cha mapinduzi na kuwa cha Maneno.
 

Acha ujinga wewe muovu na shetani kama si msafi na ana kashfa zinazomkabili mbona asichukuliwe hatua?Njooni uwanjani 2015 tuwafyeke wote,mnachafua nyumba yetu na magamba yenu.
 
kweli hizo lugha za matusi ndo zitawamaliza ccm juzi kwenye kufunga kampeni mzee mkapa tena kwa msisitizo kawita wapinzani MAFEDHULI kweli ni lugha ya kutumia kwenye kampeni mbona hawamuigi mzee mwinyi.sasa imewacost unadhani kwa wakati huu MAFEDHULI ni nani kama sio wao wenyewe. wananchi wameamka hivi sasa twahitaji tanganyika yetu, na kama haitoshi tunawaomba waandae jeneza la kukizika chama chao
 
CCM imeshindwa vibaya arumeru mashariki katika kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo lililoachwa wazi na marehemu jeremiah sumari!kushindwa kwa ccm hakujatokea kwa bahati mbaya,kiukweli hata kura hizo walizozipata ni nyingi mno na inaonyesha ni namna gani nguvu kubwa ilitumika kuwashawishi wananchi!najenga hoja hii kwa sababu uwezekano wa ccm kushindwa ulikuwa mkubwa mno kuliko kupata ushindi!sababu za ccm kushindwa ni hizi

1. CCM imegawanyika pande kuu mbili ambazo zinapingana kwelikweli wakati chadema ni wamoja sana (msisahau maneno ya wazee" umoja ni nguvu....")

2. CCM wanatuhumiana wao kwa wao kupeana sumu, na wanawindana kwelikweli kati ya makundi hayo mawili yanayohasimiana sana huku kundi moja likiwa na nguvu kubwa ya pesa ilihali lingine likungwa mkono na wanamapinduzi ambao hawajapoteza muelekeo

3.ccm ilikwenda na pesa zake za mfukoni kuwashawishi wananchi wakati chadema walienda kuomba kuwatumikia wananchi

4. CCM hawakutakiwa kueleza namna watakavyotatua matatizo na kero za wananchi kwani wao ndio waliokuwa wakishikilia jimbo bali walitakiwa waseme wametatua kero ngapi na ni ngapi zingine ziko kwenye hatua gani

5. Ahadi hewa lukuki zisingeweza kukinusuru chama hiki kwani kimeshindwa kutekeleza ilani yake kwa vitendo

6. Kitendo cha kuifanya nchi hii kuwa ya kifamilia kimeigharimu mno ccm arumeru,nchi hii ina watu wengi sana wanaoweza kushika madaraka na hakuna sababu ya kurithishana hii sio nchi ya kifalme

7. Vijana hawana nafasi ya kutosha kwa usawa ndani ya ccm labda uwe mtoto wa kigogo tofauti na ndani ya chadema ambako vijana wana usawa bila kujali wewe ni mjukuu wa ndesamburo au mtei huu ni mwanzo wa safari ya kifo cha kudumu cha ccm, na kwa namna hii watu wamebaki kujiegesha ccm kwa sababu ni chama tawala tu, siku kikianguka hakitainuka tena!

Ni muda wa kufanya mabadiliko na kujirekebisha ili ccm itakapokuwa chama cha upinzani baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 kilete changamoto za kweli kwa chadema asanteni wadau
 
Wape vidonge vyaoooo! Haki ya baba, 2015 ccm mpinzan,
 
Ni kweli si vibaya kutoka tajiri wa kutupwa hadi masikini wa kutupwa yote ni maisha nainatakiwa CCM wayaishi hayo maisha. ilinishangaza kuona Mkapa akiwaahidi wana Arumeru kutatua tatizo la ardhi wakati yy alikuwepo miaka kumi madarakani na hakutatua tatizo hilo, ilitakiwa aeleza namna alivyoshughulikia na wapi aliishia katika kutatua tatizo hilo
 
Mi kweli lawa,yeye mwenyewe ni kati ya watuhumiwa wa kumiliki ardhi "kimipango" iweje akawasaidie arumeru mashariki
 

Napenda kusisitiza hapo kwenye rangi nyekundu kuwa , Mifano ya vyama vilivyotawala vikaanguka na kushindwa kuinuka iko mingi, michache ni hii
1. KANU - Kenya
2. UNIP- Zambia
3. CHAMA CHA OBOTE KULE UGANDA
 
Napenda kusisitiza hapo kwenye rangi nyekundu kuwa , Mifano ya vyama vilivyotawala vikaangakua na kushindwa kuinuka iko mingi, michache ni hii
1. KANU - Kenya
2. UNIP- Zambia
3. CHAMA CHA OBOTE KULE UGANDA
plus Wade senegal
 
Hawakujua.!..hawakujua!!...kumbe hawakujua!!!

Namkumbuka Mfalme Daudi alivyoonekana si chochote mbele ya Wafilipi wakiongozwa na Golliath lakin kumbe tayari Mungu alishamtia mafuta ya ufalme na ilivyofika muda wa vita tu kijana mdogo,mnyonge lakini jasiri akafanya kile ambacho hakikutegemewa na wengi na baada ya hapo ukawa ndo mwisho wa Wafilipi...Golliath hakujua,hakujua,kumbe CCM nayo haikujua,haikujua kama CDM inaleta ukomo wa wanyang'anyi na waonevu kuendelea kutawala.

Ama labda walijua? (Nyerere) ..hapana,hawakujua (Ben&JK) hawakujua.
 
"CDM wanachangiwa na wananchi,c.c.m tunawahonga wananchi" mkuu hapa nimepapenda sana.
 

Ninakubaliana na mawazo yako. Ninakushauri utafute website ya ccm halafu upost hayo mawazo kule. Yanaweza yakawafikia wakubwa wa chama haraka na labda wanaweza kuyafanyia kazi.
 
Ninakubaliana na mawazo yako. Ninakushauri utafute website ya ccm halafu upost hayo mawazo kule. Yanaweza yakawafikia wakubwa wa chama haraka na labda wanaweza kuyafanyia kazi.

Naomba kujua hiyo website address ya CCM
 

Unahangaika bure tu kujaribu kumchafua Dr Slaa, kungekuwa na tuhuma japo moja yenye ushahidi ambao una hata 1% ya ukweli magamba mngeshamfunga jela tayari. Wewe endelea na kujikomba kwako, lakini ukae ukijua kuwa kuna siku - na haiko mbali - hata watoto wako mwenyewe (assuming unao) watakuzomea hadharani!
 
Naombea ccm kifo chema, ife na jasho la watanzania na sio damu zao. Ccm inakufa huku ikiwa imeifilisi tanzania zaidi ya mkoloni mzungu aliyewatesa mababu zetu, ila itakuwa mbaya zaidi kama itakufa na damu zetu kwa kutumia green gad zao kuvuruga amani ya inchi. Raha ya milele uwanyime Ee Bwana, na mwangaza wa milele uwazimie wapumzike kwa hofu Amen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…