Uchaguzi 2020 CCM tumezidiwa sana na tunaweza tusimalize vizuri. Huyu mtu kasi yake ya ajabu

Mzee we unakwama wapi maana walipo JF ndo waliko mtaani na ni wapiga kura
 
Wanaccm woòoteeee
Someni Waraka wa Mtume Paulo kwa Wakolosai
Sura ya tatu , aya ya 25

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee we unakwama wapi maana walipo JF ndo waliko mtaani na ni wapiga kura
Uliwahi kuona post yoyote jamii forums ina likes milioni 1 ?!?... Ndo ujue wafuasi wa mitandaoni ni % ndogo sana. Halafu hata mkoa uliopo wote wampigie kura Lissu hawezi kuja kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. NEVER.
 
Law of the Universe haipo hivi, kuna mwisho wa kila kitu chini ya jua.
Kuhusu mitandao, kwa mujibu wa TCRA kuna watumiaji takribani 23 milioni hadi kufikia mwezi May 2020. Kwa sasa eneo la mitandao lina nguvu kubwa sana katika kutoa mwelekeo wa masuala mengi kwa jamii, taarifa ni silaha kubwa.

CCM haiwezi toka madarakani kwa usiku au asubuhi moja, ni suala la mchakato wa muda wenye hatua mbalimbali. Naweza kusema kwa sasa mchakato huo upo hatua nzuri, tunaona ukosoaji unaongezeka, makundi yenye ku-reason yanaongezeka, mawazo ya watu wengi yanapuuzwa, CCM inagawana mbao kadri muda unavyozidi kwenda. Niseme tu ni suala la muda, kama siyo CHADEMA basi umma utaitoa CCM madarakani au CCM itajitoa yenyewe kwa kugawana mbao kama KANU.

Haya ya helicopter ni mambo ya kawaida watu kufurahi na kushabikia kwenye kampeni wala siyo sababu ya chama kusahau kampeni. Kwa sasa swali muhimu kwa CCM ni Je KWA NINI UPINZANI UNAUNGWA MKONO KIASI HIKI?
 
Chadema pamoja na kubebwa jamii forum lkn hamna uwezo wa kumpigania mgombea wenu

Nyuzi za Ccm zinapigwa pin lkn Chadema ndio mpo hoi
 
Mnategemea NEC wawafaulishe ila ccm imekufa wamebaki wale wenye maslahi binafsi.
 

Shida ya Chama chetu ni wengine kujiona ndio wenye chama zaidi na kuwapuuza wengine. Badala ya kujibu hoja zinazotolewa na wapinzani wetu tumekuwa tukitumia vyombo vya dola, hususan jeshi la polisi, kuzikandamiza hoja hizo. Hilo halifai na kauli za kubeza sio silaha muafaka kwa wakati huu kwani watu wanweza kupambanua na kuona hatuna hoja.

Nashauri Sekretariet chini ya Komredi Bashiru ilipange sawa kwa kipindi kilichobaki kisichozidi saa 150 kufikia siku ya uchaguzi, kuja na mikakati thabiti ya kupenya mioyo ya wapiga kura badala ya kubweteka na kudhani tunapendwa "automatic".

Komredi Polepole aachane na vijembe vya waimba-taarabu. Havitusaidii sana tunapokumbana na watoa hoja makini wa upande wa pili kwenye vijiwe huku mtaani (site) waliko wapiga kura halisi.

Ma-DC kama Ole Sabaya wanafanya harufu ya chama chetu kuwa mbaya puani mwa jamii na kuonekana kina elements na ujasusi wa kipuuzi. Huyo akemewe mara moja na asiendeleze ujinga huo wa uhuni wa magenge ya kialifu. Ushindi wa damu sio ushindi.
 
Mwana UHONGO
 
Ukweli unauma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…