Ccm: Tujifunze kutokana na makosa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm: Tujifunze kutokana na makosa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mundali, Apr 24, 2012.

 1. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Chama Cha Mapinduzi, mmekuwa mkifanya makosa sana ya kudhani adui wenu ni wapinzani. Kutokana na kufikiri mkiwa ndani ya sanduku mnadhani njia ya kudhoofisha upinzani ni kuwakwamisha kwa kuwazulia kesi mbalimbali, kuwazuia kutoa maoni yao, kuwafungia n.k. Hili ni kosa kimantiki, kwani mchawi wa CCM ni CCM. Anayeimarisha upinzani ni CCM yenyewe na inajipeleka kaburini yenyewe. Mifano: -
  1. Mlitumia hila mkamfungia Zitto Z. Kabwe baada ya kutoa hoja bungeni ya kuhoji mkataba wa madini kusainiwa Hotelini tena nje ya nchi, badala ya kutumia ofisi rasmi za serikali. Ukweli ulipobainika, jina la Zitto likavuma kama kimbunga mpaka leo anawasumbua kweli kweli. Laiti hatua zingechukuliwa na bunge kwa kuunda kamati kama ya Mwakyembe, mkataba ukafutwa, rasilimali za nchi zikalindwa, tungewaamini na umaarufu wa Zitto usingekuwa wa kiasi cha sasa.
  2. Mlizuia hoja ya ufisadi kujadiliwa bungeni, Dr. Slaa akashusha vitu pale mwembe yanga. Mkalazimishwa na wafadhili kufanya uchunguzi huru, ukweli ukadhihiri ikawakuta aibu, chati ya Dr. ikapanda vibaya sana, leo anawapa shida mpaka mkamnyang'anya ushindi wake.
  3. Mmetengeneza hukumu ya dhuluma kwa Godbless Lema, kwa ule ule upofu wenu kudhani tatizo la Arusha ni Lema, mkawatesa sana wanaarusha kwa mgao mkali wa umeme kwa kudhani watamchukia Lema, imekuwa kinyume chake maana hata wafuasi wenu wamewakimbia. Lema leo ni maarufu nchi nzima, mwaka jana tu kaingia bungeni, kapata umaarufu kwa ngazi ya CCM.
  4. Wakati bado hata chuki ya wanachi haijatulia, mnachemka tena kwa kuwalinda wezi wa mali ya umma kwa zilezile ahadi zenu hewa, ati tutafanya uchunguzi atakayebainika atawajibishwa. Uchunguzi wa matokeo ya uchunguzi au kusafisha waliochafuliwa? wananchi wanazidi kuwachukia.
  5. Kuna kosa la ziada mnaliandaa, kuwapiga chini Mnyika na Lissu. Mnazidi kujiangamiza. Ziacheni mahakama zifanye uamuzi kwa haki na uhuru, nanyi mtakuwa huru. Kinyume chake ni kufanya makosa yaleyale.
  Kushuka kwenu mvuto si kwasababu wapo akina Mbowe upinzani, bali ni kutokana na kwenda kinyume na katiba yenu wenyewe na kuikana ilani yenu wenyewe. Badilikeni akina Nape, tendeni mnachonena walau mnaweza kupata nusu ya wabunge 2015.
  Nawasilisha
   
 2. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Dah nape anaujua ukweli lkn hawezi kuusema anogopa kuwaudhi wakubwa, RIP magaaaaaaaaaaa
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  tatizo lao wagumu kuelewa
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  sisi ccm tunasema hivi CCM itadumu milele na hizo ni kelele tuu!
  tatizo la watanzania wengi mnawivu wa kike!!
  hahahaha inafurahisha sana!
   
 5. I

  Iramba Junior Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mdau nashukuru for clear analysis,ila nilishawahi kusema siku moja na narudia kwamba "It is too late for CCM to catch the train"wasubiri kimbunga cha mwisho 2015 hizo zote ni rasha rasha.
   
Loading...