Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 879
- 969
CHAMA CHA MAPINDUZI KIMETOA ASANTE/SHUKURANI KWA WANANCHI WA TANZANIA KUCHAGUA CCM KATIKA UCHAGUZI MDOGO
Chama cha Mapinduzi katika Mkutano wake na waandishi wa Habari uliofanyika Ofisi ndogo za CCM-Lumumba jijini Dar es salaam leo, Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg,Humphrey Polepole amesema,”Chama cha Mapinduzi kinasema ASANTE SANA kwa wananchi kwa kuendelea kukiamini”.
Kauli hii imetolewa kutokana na Uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 22/01/2017 ambapo kulikuwa na Jimbo moja(1) la Ubunge ambalo ni Dimani Zanzibar na Kata 20 zilizopo sehemu mbalimbali Tanzania.
Katika uchaguzi huo mdogo Chama cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa kishindo katika Ubunge jimbo la Dimani Zanzibar na Kata 19 kati ya 20 ambapo kutokana na matokeo haya, Chama cha mapinduzi kimetoa ASANTE kwa wananchi walioendelea kukiamini na kukipigia kura chama hiki.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndug, Humphrey Polepole ametoa siri mbili za Ushindi wa Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi mdogo;
1. Chama cha Mapinduzi kuzaliwa upya(CCM Mpya).
2. Kazi mzuri ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya Rais WA Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Ahadi ya Chama cha Mapinduzi kuelekea 2020 ni ‘Kufanya Siasa safi inayojikita katika maendeleo’.
Chama cha Mapinduzi kinawaomba wananchi waunge mkono na kushirikiane kwa pamoja katika kuleta maendeleo ya Tanzania.
[HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Miaka40YaCcm[/HASHTAG]