CCM Tabora wazomewa

CCM Tabora wazomewa

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,932
BAADHI ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tabora jana walipata wakati mgumu baada ya kuzomewa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.

Tukio hilo lilitokea kwenye mkutano wa hadhara ulifanyika viwanja vya stendi ya mabasi zamani ambako walihudhuria viongozi mbalimbai akiwemo mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage.

CCM ilifanya mkutano huo baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiongozwa na Naibu Katibu mkuu wake, Zitto Kabwe, kufanya mkutano katika eneo hilo na kuwachongea wabunge wa CCM Tabora kuwa hawatetei wapigakura wao.

Dalili za zomeazomea zilianza mapema kwani baadhi ya wananchi walianza kuibua vicheko na kejeli kwa viongozi wa CCM huku wengine wakisikika wakisema hawataki majigambo, matusi bali barabara za lami kutoka Tabora-Nzega, Tabora-Urambo na ile ya Itigi-Tabora na wengine wakisema 'Peoples Power'.

Wakati Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Idd Ame, akizungumza kwenye mkutano huo, wananchi wachache waliokusanyika walianza kuzomea kila kiongozi huyo alipokuwa akijaribu kuikejeli CHADEMA.

"Ndugu zangu wananchi hebu angalieni mnavyodanganywa, hivi hawa CHADEMA wanajigamba kujenga barabara wakati wao siyo watoaji wa fedha…fedha zinatolewa na serikali ya CCM, hao CHADEMA ni wanafiki na waongo," alisema Ame.
Alisema inashangaza kuona mtu anaacha jimbo lake Kigoma kwenda Tabora kuwafundisha siasa na kudai kuwa huo upumbavu.

Baada ya kauli hiyo, wananchi walipoanza kuzomea kwa nguvu na kudai wanataka sera na si matusi.
"Hapa tuko kamili endeleeni kuzomea tu…tutaumizana kwelikweli hapa msifikiri hatuwezi na tutawashitaki viongozi wa CHADEMA Tabora kwa kutufanyia fujo kwenye mkutano wetu," alisikika akisema Katibu huyo wa CCM.

Wakati katibu huyo akitamka hayo, Mjumbe wa NEC John Mchele alikwenda jukwaani na kumnong`oneza katibu huyo, ndipo ilizuka fujo kubwa huku Green Guard wa CCM wakitembeza mkong`oto kwa baadhi ya wananchi waliokuwa wakionesha ishara ya vema.

Tafrani hiyo ilidumu kwa dakika 20 na ndipo askari polisi walipoongezwa na mkutano kuendelea.

Baada ya vurugu kutulia huku wananchi wengine wakiondoka, mbunge Tabora mjini, Rage alipanda jukwaani na kutoa sh milioni 68 kwa kata 10 za manispaa hiyo na kila kata ilikabidhiwa hundi yake kwa ajili ya miradi ikiwemo ujenzi wa vyoo, umaliziaji nyumba za walimu na madarasa.

Aidha mbunge huyo alikabidhi chama cha waendesha bodaboda pikipiki mbili na kutoa ahadi ya kuendelea kusaidia.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa CCM Tabora mjini Moshi, Abdurahaman Nkonkota alilaani Jeshi la Polisi kutolinda mikutano ya CCM hadi wanafanyiwa vurugu.
 
kweli magamba kiboko 68m kwa kata kumi kila kata 6,800,000 kwahiyo ndio wataweka lami barabara zao na kumalizia nyumba za walimu?? kweli elimu ni muhimu sana kwa kila mtanzania yote haya yasinge tokea kama kila mtanzania angekua na huelewa wa kutosha
 
Viongozi CCM wazomewa katika mkutano wa hadhara
Ni baada ya kuanza kuwatukana viongozi wa Chadema

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tabora, juzi walijikuta katika wakati mgumu, baada ya kuzomewa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara. Tukio hilo la aina yake lilitokea wakati viongozi wa chama hicho ngazi ya mkoa, akiwemo Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage, walipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Stendi ya mabasi ya zamani mjini hapa.

Mkutano huo wa hadhara ulifanyika siku chache baada ya ule wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, ambaye aliwaeleza wananchi, kuwa wabunge wa CCM mkoani Tabora hawawakilishi vema wapigakura wao na kwamba kutokana na hali hiyo, wabunge wa Chadema wameamua kupigania haki zao.

Source: Mtanzania; Jumatatu, Mei 27, 2013.
 
Wananchi sasa wanajitambua, you can fool the people for sometime but you cant fool the people all the time.Alunta continua.........
 
chadema hakuna viongozi ni kikundi cha magaidi na wafanya biashara tu.
 
Mi ninachopenda kujua hizo fedha alizotoa Mbunge Tsh.68,000,000/= na kutamka kuwa ni kwa ajili ya kata 10 @6,800,000/= ninavyofahamu mimi fedha utolewa baada ya eneo husika kuwasilisha mpango unaoonyesha matumizi ya fedha hizo je kulikuwa na mipango hiyo? kama haikuwepo je Mbunge haoni kwamba inawezekana fedha hizo zikaishia mikononi mwa wachache na kuzitafuna kwani fedha zenyewe ni kidogo kulinganisha na tamko la kazi inayotakiwa ifanyike kwa fedha hizo.
 
Penye udhia penyeza rupia! CCM kwishnei!
 
Magamba hawana pa kushika, hata Wanyamwezi wameshtuka; Wakati wao wakiendelea na kuchonga bongo movies, CHADEMA tunasambaza elimu ya uraia . 2015 CCM hawana pa kuchomokea.

Hongera Tabora kwa kujitambua.

Mungu wabariki Makamanda.

Mungu ibariki CHADEMA,
 
Mi ninachopenda kujua hizo fedha alizotoa Mbunge Tsh.68,000,000/= na kutamka kuwa ni kwa ajili ya kata 10 @6,800,000/= ninavyofahamu mimi fedha utolewa baada ya eneo husika kuwasilisha mpango unaoonyesha matumizi ya fedha hizo je kulikuwa na mipango hiyo? kama haikuwepo je Mbunge haoni kwamba inawezekana fedha hizo zikaishia mikononi mwa wachache na kuzitafuna kwani fedha zenyewe ni kidogo kulinganisha na tamko la kazi inayotakiwa ifanyike kwa fedha hizo.

Hiyo ni Rushwa tu mkuu ! Huyo si amezoea kununua waamuzi kwenye Ligi kuu ya Vodacom ! Poor Aden Rage !
 
Hiyo mbona ni Rasha rasha tu , iko siku watatimuliwa jukwaani kabisa .
 
ninakusihi usiwe unatamka hayo maneno kila wakati.
maneno huumba na ni sumu.
siku moja huta amini kwenye macho yako utakapojikuta maneno yako yanakujeuka.
Hutaijua siku hiyo yatakapokujeuka.
Ni hayo tuu.

chadema hakuna viongozi ni kikundi cha magaidi na wafanya biashara tu.
 
....fedha inatolewa na CCM..kwi kwi kwi ..akili ndogo taaaabu kweli..kweli!!!
 
Da! Bila Chadema kufika hapo hizo 68m zisingetoka, kwahiyo Chadema wamefanya kazi kubwa ya kuwezesha 68m kutoka, big up CDM
 
chadema hakuna viongozi ni kikundi cha magaidi na wafanya biashara tu.

Pole sana, wananchi wanataka mabadiliko sio matusi.pole sana wewe kachukue vuku 7 uishi.
 
Back
Top Bottom