Written by mzeekondo // 22/04/2017
Naomba kidogo niongelee haya matukio yanayo shamiri katika nchi hii,utekaji wa watu kiholela,uvamizi wa mikutano ya ndani ya kisiasa iliyoruhusiwa,kupotea na huenda kuuwawa kwa Ben Saanane mmoja kati ya viongozi wa juu wa chadema,uharamia wa kuwadhibiti waandishi wa habari na
kuvamia vyombo au studio zao,matumizi ya ovyo katika kulidhibiti bunge na kulitumia kwa kuinufaisha ccm na sio taifa.
Haya ni baadhi tu ya matukio ya kihuni ambayo kwa sasa huenda yakaonekana ya kawaida kwa kuwa ni ya kila siku,kama hujapata chai ya asubuhi iliyonona, basi unaweza ukadhani unasoma habari za Rwanda au somalia,kumbe la hasha, bado upo Tanzania mpya inayoongozwa na mtu anaitwa Magufuli,sielewi kumezidi nini kiongozi huyu anaetoka katika chama ambacho siku zote kinatawala ukipenda kinaongoza taifa hili leo imekuwa kama nchi hii haiongozwi na sheria au kanuni,utawala bora imekuwa nyimbo tu, kama ile ya “wapo” iliyoimbwa na yule mwana muziki wa bongo flava, ‘Ney wa mitego”fujo,piga uwa,teka,fukuza ukiweza tukana kwanza, huu ndio mfumo mpya wa taifa hili lililochoka kuishi kwa kujisifia “amani na utulivu”unaolindwa kwa mtutu.
Ni aibu na fedheha kubwa kuwa mwanachama wa chama hiki kwa sasa,sioni tofauti ya alshabaab alqeda,abu sayaf au lile kundi la zamani la kitaliano la kigaidi la miaka ya sabini likiitwa red brigade,makundi haya yote yalikuwa na bado mengine yanauwa,yanateka na yanaogopewa,sasa ccm kwa haya tunayofanya sisi sio chama cha siasa,hili ni pazia tu, sisi ni chama cha kigaidi,kama haya baadhi ya makundi yanayotumia dini kama pazia vile vile ,siasa imetushinda hatuiwezi na hili halina ubishi tena, kwa sababu kama ni demokrasia, kwenye siasa hakuna kunyimwa uhuru wa kuongea,hakuna utekaji,hakuna kuzuia bunge kutangazwa moja kwa moja ili wananchi wajue wawakilishi wao wanafanya kazi waliyowatuma?lakini ccm tunataka wawakilishi hao wafanye wanayotumwa na Rais sio ccm wala sio watu.
Mtukufu Magufuli ana mpango wa kukiuwa chama cha mapinduzi taratibu tena kwa makusudi,bado wana ccm hawajashtuka,mfumo uliopo sasa haumruhusu yeye kutawala anavyotaka, ndio maana analiuwa bunge,mahakama na ccm polepole,anakusanya nguvu zote ikulu “consolidation”ili wakati ukifika iwe rahisi na imezoweleka kupokea amri tupu, na sio katiba au sheria,anafukuza wale wote anao waona kuwa ni wakorofi ndani ya chama ambao anahofia watakuwa kikwazo kwa yeye kufanya atakavyo, kwa kisingizio cha kutumbua majipu katika chama kwa kuwa serekalini amerowa usaha kwa kuifanya kazi hiyo.
Rwanda ndio imekuwa mfano mzuri na wa pekee anaouona unafaa kuwatishwa Watanganyika,kuwa wameuwana kwa maelfu kisa kuna ukabila na vyama vilikuwa vingi,kumbe anaemuabudu yeye ni Kagame kwa kuwa amri zote ni za mtu mmoja katika nchi hiyo,mahospitalini hasa muhumbili akina mama wanajifungua na kulazwa chini,Magufuli anawanunulia wagonjwa ndege, wakati yeye anaiogopa kuliko ukimwi, anadhani usalama wake uko barabarani haijui kadhia ya Sokoine.
Upinzani ulishamiri sana uchaguzi uliopita, umeidhihirisha dunia na watanzania wote kuwa sasa ccm tumechokwa,ghafla marufuku kufanya mikutano ya kisiasa mpaka baada ya miaka mitano, yaani wakati wa uchaguzi tu,kwa kufanya hivi Magufuli anadhani ndio atashinda uchaguzi, na ccm watapendwa upya,wapi kasikia kuwa watu hawafanyi kazi kwa kuwa wanahudhuria mikutano ya siasa peke yake, ndio maana na sababu akaipiga marufuku,ikiwa hivyo ni kweli,basi ni ccm tuliokuwa tunaongoza kwa mikutano yao ovyo na ya kila siku, ndio maana mwisho tukampata mtawala anaitwa, John Joseph Pombe,wewe ni tunda la mikutano yetu isiyokwisha uliyoichoka, kwa kuwa umeshafika safari yako.
Zanzibar katika siasa sisi hakuna jipya linalofanyika Tanganyika likatushtua hivi sasa ambalo hatufanyiwa na ASP au ccm,hapa wazee wetu walitekwa kwanza halafu wakauliwa, hata makaburi yao hatujaonyeshwa bado, wengine wanasema yako pwani wengine kinu moshi, mazombi wanatusalimia kila wakikosa shughuli, vituo vya redio/ habari binafsi na maskani za cuf zinavamiwa na watu kupigwa bure kama tuko Afrika kusini kabla uhuru,wakati haya tunaambiwa ndio maendeleo ndani ya mapinduzi, sijui tushike lipi,almuradi tunatiwa vilema bila kisa, na ukienda polisi bado wanaifanyia uchunguzi kesi ya mtu aliyepigwa na waliouwawa wakati wa utawala wa Aboud jumbe hawajazimaliza, sijui hizi za leo zitakwisha au kusikilizwa lini.
Taifa hili haliweziki kupata barka za Mola kwa uaharamia huu na ule uliofanywa huko nyuma,sisi tutateseka mpaka siku ya mwisho kwa sababu hatujui wala hatuna jema katika ardhi hii,wachache wamekalia na kuushika mpini huku wakitesa na kuuwa wengi,kibri,dharau na kejeli ndio ajira zao.
Sisi raia wa mwenyezi Mungu hatuwezi kukosa pa kukimbilia,kwake ndiko tulitakiwa tuhamie kabla dhiki na dhulma hizi,lakini yeye ni mwingi wa rehma/kusamehe nk, basi sote turudini kwake na kumshitakia kesi hii,siasa imetushinda ccm sasa tunazidhulumu nafsi TU, hili ndilo tulilofuzu,nilisema sana kuwatahadharisha ndugu zetu wa Tanganyika hawakutaka kunisikia,Zanzibar ina bei,tena sio rahisi, ni lazima muiweze kama mnataka kututawala kwa nguvu,hamtoitawala bure,sasa mnauwana,mnatekana,hamuelewani tena na wapinzani wenu,ccm mmeigeuza chaka la magaidi na mnakatazana kuhutubia mikutano iliyoruhusiwa na katiba ya nchi yenu kisa ZANZIBAR.
KARIBUNI, ZANZIBAR NI NJEMA, ATAKAE NA AJE.